Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Jaribu kuwaza,uwatangazie watu ni Ebola kumbe sio ni Maburg,wakajua kuwa ina chanjo,wakapata chanjo ya ebola wakidhani wamejikinga.Halafu mlipuko ukaendelea kusambaa,watu haohao wakadhurika na kupata Marburg...kwa ujinsi unavyoweza kuua kwa haraka..unadhani utakuwa umesaidia au umetengeneza tatizo zaidi?

Pia,mambo ya kisayansi,yanaendeshwa kisayansi.Huwezi tangaza Ebola wakati kuna Marburg.

Tumekubaliana ya professionals yanabakia kwa Professionals.

Kwanini Congo, Uganda, Gabon, Guinea, Sierra Leone, Liberia na kote kwingine serikali imekuwa ikisema ilikuwa ebola?

Kwamba tuna Ebola isiyo na chanjo haikuwa ndiyo njia sahihi ya kuufikisha ujumbe kwa jamii yetu ndani ya ufinyu wa lugha yetu badala ya kujifunza majina mapya?

Hatuna haki ya kujua maendeleo ya ugonjwa huu?
 
Ebola isiyo na chanjo sio Marburg.
 
Ni baada ya majibu ya maabara kuonyesha kiumbe anaehusika kuleta ugonjwa. Na hii haifanywi na nchi husika tu bali hufanyika chini ya usimamizi wa shirika la afya duniani.

Hii ni katika kuweka utayari wa kupambana na janga husika kwa kusaidia: utaalamu, resources na tahadhali kuchikuliwa.

Magonjwa ya mtindo huu huweza kuleta madhara makubwa ndani ya muda mfupi kwa eneo, nchi, ukanda na sunia kwa ujumla hivyo yanaangaliwa kwa umakini mkubwa.
 
Ebola isiyo na chanjo sio Marburg.

Hakuna popote niliposema Marburg scientifically ni ebola wala vice versa. Muda wote nimekuwa wazi:

"Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?"

Kwani issue ya Malaria na plasmodium ilikuwa ya nini ndugu?

Kulikuwa na haya pia, vipi hukuyaona?

Then, tukubali majibu yaliyotolewa labda tu kama tuna majibu mengine scientifically. Tusitengeneze theory anbazo wenzako wajikupa ushahidi wao wa ki-maabara wewe utabaki na maneno matupu.
Pamoja na uwezo wetu mzuri wa kufikiri.

Maendeleo ya ugonjwa: timu ya wizara na shirika la afya macho yao yako kule na yanaendelea kupokea mienendo na kila dakika, saa, siku nk.
 
Ni baada ya majibu ya maabara kuonyesha kiumbe anaehusika kuleta ugonjwa. Na hii haifanywi na nchi husika tu bali hufanyika chini ya usimamizi wa shirika la afya duniani.

Hii ni katika kuweka utayari wa kupambana na janga husika kwa kusaidia: utaalamu, resources na tahadhali kuchikuliwa.

Magonjwa ya mtindo huu huweza kuleta madhara makubwa ndani ya muda mfupi kwa eneo, nchi, ukanda na sunia kwa ujumla hivyo yanaangaliwa kwa umakini mkubwa.
SIna hakika kama mada umeisoma. Hakuna popote ninaposema kuwa Marburg ni Ebola au Ebola ni Marburg au kuwa iliyopo ni Ebola, professionally.

Msingi wa mda ni huu hapa:

"Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.

Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola."

Zaidi sana nimekazia:

Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?

Mwongozo wako tafadhali.
 
Msingi wa hoja: Kutangaza Marburg na si Ebola.

Maelezo: Marburg na Ebola ni ciumbe tofauti na magonjwa yao ni tofauti.

Ila kwa ujumla magonjwa yake yanajulikana kama HAEMORRHAGIC FEVER.

Ugonjwa upi utangazwe ni baada ya majibu ya maabara kuonyesha kiumbe husika.

Kuna magonjwa mengi bado hayajulikani lakini yapo kwenye vitabu na hayana majina ya kiswahili. Marburg inatokana na jina la mji ambao ugonjwa uligungulika huko Ujerumani. Sina uhakika kama tunaweza kubadili jina la mji kuwa kiswahili.

Ugonjwa hautajwi kwa jina linalofahamika au karibiana nao bali jina halisi.
 
Marburg na ebola wapo kundi moja la virus

Filoviruses (very long viruses ) na wote ni enveloped RNA viruses na wana present na symptoms Sawa na wote hawana dawa zaidi zaidi tunatumia monoclonal antibody kutibu Mfano ansumivabb hata vaccine yake ya kuunga haijulikani bado, Zmapp
Na wote wanapimwa na RT-PCR pamoja na ELISA

Hawa ni wabaya na si kama corona wa story nyingi Hawa ukileta masihara unakwenda na maji
 
Then, tukubali majibu yaliyotolewa labda tu kama tuna majibu mengine scientifically. Tusitengeneze theory anbazo wenzako wajikupa ushahidi wao wa ki-maabara wewe utabaki na maneno matupu.
Pamoja na uwezo wetu mzuri wa kufikiri.

Maendeleo ya ugonjwa: timu ya wizara na shirika la afya macho yao yako kule na yanaendelea kupokea mienendo na kila dakika, saa, siku nk.
Post #87 imejielekeza. Mada Ina tofautisha taarifa kisayansi na kijamii kwa matumizi yenye tija.

Malaria na plasmodium ni muhimu scientifically lakini usafi wa mazingira, kufukia madimbwi, malaria, dawa mseto na kumwona daktari ni mhimu kwa jamii Kwa akili ya tija.

Tofauti ya neno ebola na Marburg Ina tija gani kwa jamii inayokabiliwa na ugonjwa unaosababishwa na kula vitu vile vile, kumbukizwa vile vile, kujikinga vile vile, kuathirika vile vile, kufa vile vile, nk, kwa kirusi grupu lile lile ila jina jina tu?

Huku kuhodhi taarifa wakati tulio hatarini ni sisi nyie mnakuona je?

Kwani tukijua hali ikoje wapi hatuwezi nasi kuchukua hatua ndani ya uwezo wetu?
 
Marburg na ebola wapo kundi moja la virus

Filoviruses (very long viruses ) na wote ni enveloped RNA viruses na wana present na symptoms Sawa na wote hawana dawa zaidi zaidi tunatumia monoclonal antibody kutibu Mfano ansumivabb hata vaccine yake ya kuunga haijulikani bado, Zmapp
Na wote wanapimwa na RT-PCR pamoja na ELISA

Hawa ni wabaya na si kama corona wa story nyingi Hawa ukileta masihara unakwenda na maji

Watu wanafiri kusema Marburg ni kurahisisha maisha. Bado tunahitaji umakini na hatua madhubuti kusimamia hili.
 
Post #87 imejielekeza. Mada Ina tofautisha taarifa kisayansi na kijamii kwa matumizi yenye tija.

Malaria na plasmodium ni muhimu scientifically lakini usafi wa mazingira, kufukia madimbwi, malaria, dawa mseto na kumwana daktari ni mhimu kwa jamii Kwa akili ya tija.

Tofauti ya neno ebola na Marburg Ina tija gani kwa jamii inayokabiliwa na ugonjwa unaosababishwa na kula vitu vile vile, kumbukizwa vile vile, kujikinga vile vile, kuathirika vile vile, kufa vile vile, kujikinga vile vile nk, kwa kirusi grupu lile lile ila jina jina tu?

Huku kuhodhi taarifa wakati tulio hatarini ni sisi nyie mnakuona je?

Kwani tukijua hali ikoje wapi hatuwezi nasi kuchukua hatua ndani ya uwezo wetu?
Tatizo haujafahamu kuwa haya yote bado yamebeba uzito sawa(jifunze kuhusu HAEMORRHAGIC FEVER).

Ndio maana wataalamu wa afya wamehamia eneo la tukio. Ila hatuwezi kutumia jina tofauti kwa lengontofauti. Ukweli utabaki palepale kwa kilichopo.
 
Mbona naona katika wote mnaojadili hapa mnajizungusha au kukwepa kuzungumzia swala la kwamba miezi kadhaa nyuma Uganda walikuwa na hii changamoto na tukumbuke Uganda ni jirani tu hapo na tulishauriana tuchukue tahadhari.

Sio binadamu wote wana akili timamu. Kuna watu wanavichwa vigumu na vizito kuelewa hawa kuwaelekeza inabidi utumie hata viboko na kipigo ili wakikumbuka maumivu wajue mipaka yao ila sio kushika maelekezo ya mdomo.

Sasa nina mashaka muingiliano wa raia eneo la mipakani hapo wilaya za Bukoba wameruhusu watu wa Mataifa jirani kuingia na hatimaye wameleta maambukizi upande wetu.

CCM na genge lao wanalojiita serikali (of which mimi nakataa) wameshindwa kuweka mikakati ya tahadhari tokea siku taarifa ya kwanza ya outbreak huko Uganda imetokea je, walituma hata makachero wa usalama wa taifa kwenda kutazama hali ipo vipi na kuja na mikakati ya kuweka lile eneo chini ya uangalizi ikiwamo kuweka vipimo maeneo yote ya jumuiya na kufanya vipimo kwa raia wanaosafiri kuja mikoa mingine?!

Hapa nina wasi wasi kuna watu wanaingia kila siku kutoka mataifa haya jirani na kuja bila kukaguliwa na hatimae tutakuja shituka outbreak imesambaa mikoa mingine ya katikati.

Mkoa wa bukoba unatakiwa kuwa under quarantine kuanzia sasa tukizungumza. Asiruhusiwe mtu yoyote kutoka huko kuja mikoa jirani wala kwenda nchi jirani hadi pale amefanyiwa vipimo mara kumi kumi ili kujiridhisha kuwa hana hizo changamoto.

Hii inchi muda mwingine mtu unajiuliza inaendeshwa na watu wa aina gani mbona hata wanafunzi wa chuo kikuu wangepewa serikali basi wangekuwa na maamuzi serious sana kuliko hawa wadudu tulio nao.

Wao kazi yao ni kufuatilia nani kamtukana raisi, nani anaponda serikali hizo ndizo shughuli ambazo hawa wanaojiita usalama wa taifa wanazimudu ila mtu anapita kwenye mipaka na virus wa ugonjwa hatari sana ambao unaua kwa haraka sana mara tu ukimpata muhanga, huyu mtu anapita kwenye mipaka bila kikwazo chochote na kuleta madhara kwa raia.
 
Atakuwa ni yule shujaa wa awamu Ile akiungwa mkono na kina Ngorunde. Hayo yakiendelea:

"Mabasi ya Happy Nation, Majinja, Abood, Travelers, Frester nk, yakipeleka mabasi mawili mawili tokea huko njia nzima kupitia Kahama, Singida, Dodoma, Morogoro hadi Dar kila siku."

Hii achilia mbali Mwanza, Musoma, Arusha, Moshi hadi Kigoma.

Ila tuko busy kuondoa taharuki.
Aiseee mimi hapa hadi naogopa yaani. Unajua tokea outbreak watu wanakwenda na kurejea hiyo mikoa masaa 24.
 
Watu wanafiri kusema Marburg ni kurahisisha maisha. Bado tunahitaji umakini na hatua madhubuti kusimamia hili.
Uzuri hawaambukizwi kwa hewa ni bodily fluids hata semen inaambukiza Hawa Sasa Dada zetu wanaojiuza shida inakuja hapa 😂
 
Mbona naona katika wote mnaojadili hapa mnajizungusha au kukwepa kuzungumzia swala la kwamba miezi kadhaa nyuma Uganda walikuwa na hii changamoto na tukumbuke Uganda ni jirani tu hapo na tulishauriana tuchukue tahadhari.

Sio binadamu wote wana akili timamu. Kuna watu wanavichwa vigumu na vizito kuelewa hawa kuwaelekeza inabidi utumie hata viboko na kipigo ili wakikumbuka maumivu wajue mipaka yao ila sio kushika maelekezo ya mdomo.

Sasa nina mashaka muingiliano wa raia eneo la mipakani hapo wilaya za Bukoba wameruhusu watu wa Mataifa jirani kuingia na hatimaye wameleta maambukizi upande wetu.

CCM na genge lao wanalojiita serikali (of which mimi nakataa) wameshindwa kuweka mikakati ya tahadhari tokea siku taarifa ya kwanza ya outbreak huko Uganda imetokea je, walituma hata makachero wa usalama wa taifa kwenda kutazama hali ipo vipi na kuja na mikakati ya kuweka lile eneo chini ya uangalizi ikiwamo kuweka vipimo maeneo yote ya jumuiya na kufanya vipimo kwa raia wanaosafiri kuja mikoa mingine?!

Hapa nina wasi wasi kuna watu wanaingia kila siku kutoka mataifa haya jirani na kuja bila kukaguliwa na hatimae tutakuja shituka outbreak imesambaa mikoa mingine ya katikati.

Mkoa wa bukoba unatakiwa kuwa under quarantine kuanzia sasa tukizungumza. Asiruhusiwe mtu yoyote kutoka huko kuja mikoa jirani wala kwenda nchi jirani hadi pale amefanyiwa vipimo mara kumi kumi ili kujiridhisha kuwa hana hizo changamoto.

Hii inchi muda mwingine mtu unajiuliza inaendeshwa na watu wa aina gani mbona hata wanafunzi wa chuo kikuu wangepewa serikali basi wangekuwa na maamuzi serious sana kuliko hawa wadudu tulio nao.

Wao kazi yao ni kufuatilia nani kamtukana raisi, nani anaponda serikali hizo ndizo shughuli ambazo hawa wanaojiita usalama wa taifa wanazimudu ila mtu anapita kwenye mipaka na virus wa ugonjwa hatari sana ambao unaua kwa haraka sana mara tu ukimpata muhanga, huyu mtu anapita kwenye mipaka bila kikwazo chochote na kuleta madhara kwa raia.
Tujitahidi kusoma vyema: historia hutumika, dalili na vipimo.

Maabara imethibitisha yale ya Uganda si haya tuliyonayo. Hivyo, tunayaweka kando.
 
Msingi wa hoja: Kutangaza Marburg na si Ebola.

Maelezo: Marburg na Ebola ni ciumbe tofauti na magonjwa yao ni tofauti.

Ila kwa ujumla magonjwa yake yanajulikana kama HAEMORRHAGIC FEVER.

Ugonjwa upi utangazwe ni baada ya majibu ya maabara kuonyesha kiumbe husika.

Kuna magonjwa mengi bado hayajulikani lakini yapo kwenye vitabu na hayana majina ya kiswahili. Marburg inatokana na jina la mji ambao ugonjwa uligungulika huko Ujerumani. Sina uhakika kama tunaweza kubadili jina la mji kuwa kiswahili.

Ugonjwa hautajwi kwa jina linalofahamika au karibiana nao bali jina halisi.

Hata ebola si kiswahili. Bali ebola ni jina la mto huko Congo lenye kuhusianishwa na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa ulioko Kagera hauwezi kuachwa kufungamanishwa na ugonjwa uliomalizika majuzi Uganda.

Why is Uganda's Ebola outbreak so serious? - BBC News

Kwamba Uganda ilikuwa ebola ni mwenda wazimu pekee anaweza kuamini Leo kuwa kagera Kuna ugonjwa mwingine Marburg ambao si ebola wenye dalili hizo hizo.

Hivi Kwa kutuona je ndugu?

Nyie si mna historia ya kupima mbuzi, oil, mapapai na hata mafuta ya kula na majibu yanapatikana?
 
Uzuri hawaambukizwi kwa hewa ni bodily fluids hata semen inaambukiza Hawa Sasa Dada zetu wanaojiuza shida inakuja hapa 😂
Kazi ipo, ukipata mtu wa kutoka huko kwa sasa. Na incubation period 21 days. Post illness viral availability??😣
 
Hata ebola si kiswahili. Bali ebola ni jina la mto huko Congo lenye kuhusianishwa na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa ulioko Kagera hauwezi kuachwa kufungamanishwa na ugonjwa uliomalizika majuzi Uganda.

Kwamba Uganda ilikuwa ebola ni mwenda wazimu pekee anaweza kuamini Leo kuwa kagera Kuna ugonjwa mwingine Marburg ambao si ebola wenye dalili hizo hizo.

Hivi Kwa kutuona je ndugu?

Nyie si mna historia ya kupima mbuzi, oil, mapapai na hata mafuta ya kula na majibu yanapatikana?
Ulianza kulifahamu kwa mtindo huu na Marburg utalielewa pia. Nadhani tunaanza kutengeneza roundabout.
 
Hata ebola si kiswahili. Bali ebola ni jina la mto huko Congo lenye kuhusianishwa na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa ulioko Kagera hauwezi kuachwa kufungamanishwa na ugonjwa uliomalizika majuzi Uganda.

Why is Uganda's Ebola outbreak so serious? - BBC News

Kwamba Uganda ilikuwa ebola ni mwenda wazimu pekee anaweza kuamini Leo kuwa kagera Kuna ugonjwa mwingine Marburg ambao si ebola wenye dalili hizo hizo.

Hivi Kwa kutuona je ndugu?

Nyie si mna historia ya kupima mbuzi, oil, mapapai na hata mafuta ya kula na majibu yanapatikana?
Ukija na majibu yako na huamini kwenye taratibu zilizopo na wakati huo hauna ushahidi ni hisia utasaidiwaje?
 
Back
Top Bottom