Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Ebola na Marburg ni ‘communicable diseases’ maana yake ni magonjwa ambayo yanasababishwa na viruses.Ulichoandika hakina ubishi na hakuna anayebisha hicho kiufundi.
Ila zingatia msingi wa mada ambao ni tofauti na wako:
Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.
Tambua kuwa:
Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?
Majibu kwa maswali 2 haya ingekuwa la msaada sana.
Hapa ilikuwa ni kukazia tu:
Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.
Mengine haya yakiwa ni maswali yatokanayo kama ikikupendeza:
1. Huu ugonjwa ni logical kudhani umetokea Uganda. Kweli?
2. Huu ugonjwa una dalili zile zile kama walioutokomeza Uganda majuzi. Kweli?
3. Ugonjwa uliotokomezwa majuzi Uganda karibu na kagera ulikuwa ni ebola. Kweli?
Ebola ni jina la virus; anaesababisha ugonjwa unaoitwa Ebola.
Marburg ni jina la virus; anaesababisha ugonjwa unaoitwa Marburg
Chacteristic za Marburg na Ebola virus sio sawa ndio maana wanamajina tofauti.
Virus wanaofanana wanaitwa variants. Ndio maana kuna 5 Ebola virus variants.
Kwa ivyo Ebola na Marburg sio kitu kimoja.