- Thread starter
- #361
Post #360 juu inahusika.
Yafuatayo ni kweli:
1. Magonjwa ya jamii ya yaliyo tukuta Kagera (Haemorrhagic fevers) si mara ya kwanza kutokea duniani au Afrika. Kote yalikowahi kutokea ikiwamo Congo, Uganda, Sierra Leone, Guinea, Liberia nk, tumekuwa tukitaarifiwa nchini kuwa ni Ebola.
Tukiambiwa ugonjwa huo asili yake ni kula nyani au popo. Kuambukiza kwake kuwa ni kwa hatari ikiwamo hata kwa kugusana tu na mwenye vimelea vya ugonjwa huo. Mortality rate ya juu kabisa, hadi 90%.
2. Jirani zetu Uganda wamewahi kukabiliwa na magonjwa kama haya kwa vipindi kadhaa vifupi vifupi katika kila kimoja. Hii ni 2007 na 2017 ya aina Marburg na nyingine ya Ebola miaka ya 2007, 2000, 2011, 2012 na 2023 ya juzi, iliyomalizika 11/1/2023.
Mara zote hizo serikali ikitufahamisha kuwa umekuwa ni ugonjwa ule usiokuwa na tiba, Ebola. Wenye dalili za mgonjwa kutoka damu mwilini, homa kali, maumivu makali ya mwili, kutapika na kuharisha ikiwamo damu, nk.
3. Jambo la kheri kuwa Ebola ilikuwa imepigiwa sana kelele nchini, siku zote. Tahadhali kabla ya hatari na heri ya kinga kuliko tiba.
Wananchi walio wengi wanautambua ugonjwa huo kwa maelezo, madhara, hatari na udharura wa kuchukua hatua. Maisha yanastahili kulindwa, maana thamani yake haina kipimo.
4. Zilipatikana taarifa za kuwepo ugonjwa wa ajabu Kagera tokea around 2/3/2023.
Kagera kuna hali ya hatari, kumezuka ugonjwa wa kutokwa damu puani na mdomoni. Watu 5 wafariki dunia 2 wako hospitali. Serikali ichukue hatua haraka
Hali ikaendelea kimya kimya:
Bwana Harusi alivyofariki kwa ugonjwa wa ajabu
Tarehe 16/3/2023 serikali ikathibitisha uwepo wa ugonjwa huo wa ajabu na kutaarifu kuanza uchunguzi.
Kukapiga kimya:
Ugonjwa wa ajabu Kagera uchunguzi siku ngapi?
23/3/2023 wazalendo wakaibuka na wakathibitisha kuwa ugonjwa ule wa ajabu ulikuwa ni Marburg:
Serikali: Ugonjwa ulioambukiza watu 8 na kuua 5 Mkoani Kagera ni Marburg
Marburg? Ugonjwa mpya? Mswahili na Marburg wapi na wapi? Bila shaka kama ilivyokuwa imelengwa na wazalendo, maisha yanaendelea kama vile hakuna jipya:
"Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili."
Wazalendo hawa ni wale wale wa kupima oil, mbuzi, mapapai nk enzi za corona. Hao hao ndiyo walioishangaza dunia wakiwamo WHO, CDC na wengine, kuwa hakukuwapo corona duniani bali vita vya kiuchumi dhidi yetu.
Wakapiga marufuku chanjo. Chanjo zikaitwa upigaji na njama za kutufuta watanzania duniani. Tukaaminishwa kwa nguvu kwenye maombi, matumizi ya matango pori na upigaji nyungu.
Tukahubiriwa mambo ya Bupiji, NIMRICAF na juice za kutokea Madagascar, Kinjekitile style.
Dunia nzima ikiwamo, WHO na CDC wakatushangaa, maisha yakaendelea. Wakufa wakafa na wa kuishi wakaishi. Tukiaminishwa kuwa ilikuwa ni mipango ya Mungu.
Wazalendo wale wale wa zama zile ni hawa hawa wa siku hizi. Kwamba ni nyani wale wale katika pori jipya.
Hawataki tuhoji kwanini ugonjwa ule ule, wenye kupatikana vile vile, kuambukizwa vile vile, dalili zile zile, madhara yale yale, kuuwa vile vile nk, kabla ya juzi mliuita ebola na sasa ghafla mnauita Marburg? Kwamba hamuoni athari zozote kwa jamii kwa kufanya hivyo?
Si kuwa keyword hii "taharuki" isiyokuwa na tija sana kwetu inaendelea kutuhatarisha zaidi na gonjwa hili kama ilivyokuwa na gonjwa lile?
Kulikoni kutokupeana taarifa zote za ugonjwa huu ili tukapigana nao sote kama nchi? Kwamba kama si muhimu sana wenye safari zao kwenda au kutoka kwenye maeneo yenye kuathirika wakachukua maamuzi mengine?
Ni uzalendo gani huu wa kuwekana hatarini kiasi hiki?