Tunapopigania haki sawa, Tohara kwa wanawake, Ubaguzi wa rangi, nk. Tusisahau pia kupinga Utoaji wa Mahari

Tunapopigania haki sawa, Tohara kwa wanawake, Ubaguzi wa rangi, nk. Tusisahau pia kupinga Utoaji wa Mahari

Tunapopigania haki sawa, Tohara kwa wanawake, Ubaguzi wa rangi, nk. Tusisahau pia kupinga Utoaji wa Mahari​

Nina Uhakika,wapigania haki waliotajwa hapo juu, wanaona tamaduni zao ndizo bora kuliko za wengine. A typical of a Supremacy mindset society.
 
Tatizo ulilo nalo unadhani kila aliye kinyume na mfumo huu hana pesa

Swali kwako. Kwa nini wazungu walipiga marufuku kununua waafrika karne ya 19 ? Unadhani walikuwa hawana pesa za kuendelea kuwa nunua.
Tafuta hela bro ukalipe mahari,
Blah Blah Blah hazina maana
 
Subiri kwanza unijuze kitu.

Huko enzi za mababu hapakuwa na mahari? Mama zetu, bibi zetu hawakutolewa mahari?

Mahari ni utamaduni.
Ng’ombe watakuja kwetu na mie nitaenda kwa kina ng’ombe.
Kumbuka pia huko enzi za mababu hakukuwa na feminists
 
Kwa nini wazungu walipiga marufuku kununua waafrika karne ya 19
Cha ajabu kuwa wale walioona tohara kwa wanawake kuwa ni ukatili hawakuona ni Ukatili kutenganisha Familia za Kiafrika, hawakuona ni ukatili kuwachapa viboko Waafrika, wanawake na wanaume, wa 'toto' na wakubwa hawakuona ukatili wao mpaka pale waumini wa dini, tena baadhi, kuingilia kati biashara za watu zilizoakisiwa na kudhaminiwa na Serikali zao ambazo ndizo hizo hizo zilizowatumia-waumini wa dini- kuja kufanya mabadiliko ya kile walichokiita mabadiliko ya kiroho. Mabadiliko ya Tamaduni zilizopitwa na wakati.

Ni, uchungu, wa kile ambacho hawakutegemea kutokea Afrika(Ukatili wa hali ya Juu) dhidi ya jamii zake uliwaogopesha na kuanza kuona yale yanayowatokea Wazungu Ulaya kana Laana.(Umasikini, magonjwa na Vita) Walijadili haya kwa kina katika Bunge la Uingereza na kuona laana itawatafuna, kwa unafiki na unduminakuwili wao-haikuwa sababu ya wao wazungu kuona biashara za watu zina madhara, ila madhara wanayopata au waatakayopata wao kuwa hasi kwa Udhalimu wao, call it 'poetic justice' call it Laana, call it Karma ndicho walichokiogopa zaidi kuliko ukatili wao wenyewe wa Kuwabaka, kuwanyonga, kuwachapa viboko, kuwatenganisha, kuwanyanyasa na hata kuwaua kwa kile walichokiamini kuwa "wanawatendea haki" kwa kuwaondoa kutoka katika "Tamaduni zilizopitwa na wakati".

Wazungu walipiga marufuku biashara hiyo kwa sababu walikuwa wakiuana wenyewe kwa wenyewe.
 
Mahari ni sawa kuendelea kuwepo au sio sawa isitishwe ?
Swali kwako
Mahari ni Utamaduni wetu. It is our Custom and should be respected as is. Tatizo mnataka kuunganisha mambo mengi ya Haki kwa kuangamiza Tamaduni zetu za Kiafrika.

So, to answer...mahari iendelee kuwepo.

NB; Pamoja na kuwa mnadai ni kupigania...hiyo hak,i mnayo yadai sasa ndio Ubaguzi wa Rangi 2.0.....Kwani kusokomezea tamaduni zingine kwa wengine ni sawa na kusema Tamaduni zenu ni Kuu na zetu hazifai halafu mkiulizwa sababu na hila zenu, mnasema tulipiga marufuku utumwa basi tuwaamini hamna hila hasi! Huo ni Ubaguzi.
 
Utoaji wa mahari ni utamaduni ambao umekuwepo kwa muda mrefu katika jamii nyingi za Afrika na sehemu nyingine duniani. Hata hivyo, kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kufanya utoaji wa mahari kuonekana kuwa ni utamaduni uliopitwa na wakati.

Kwanza, utoaji wa mahari unaweza kuchukuliwa kama aina fulani ya biashara ya watu, ambayo inaweza kusababisha mawazo ya ubaguzi wa kijinsia na kudhalilisha wanawake. Katika baadhi ya jamii, mahari inaweza kuwa ya kiwango kikubwa sana, na hii inaweza kuzuia wanawake kuolewa na wanaume ambao hawana uwezo wa kulipa mahari hiyo.

Pili, utoaji wa mahari unaweza kuathiri haki za wanawake. Katika baadhi ya jamii, mahari inaweza kutafsiriwa kama kifuta jasho cha wazazi wa msichana, na hii inaweza kuwa na maana ya kwamba mwanamke anaweza kutazamwa kama mali au kitu cha biashara. Hii inaweza kusababisha wanawake kupata ubaguzi na kukosa haki ya kuchagua wenza wao.

Tatu, utoaji wa mahari unaweza kuchukua nafasi ya upendo na uhusiano wa kimapenzi kati ya wapenzi au wanandoa. Badala yake, mahari inaweza kuonekana kama kiwango cha thamani ya mwanamke, badala ya upendo na kujali. Hii inaweza kuathiri uhusiano wa ndoa, na kusababisha matatizo ya kifamilia na ndoa zenye shida.

Kwa hiyo, utoaji wa mahari unaweza kuonekana kuwa utamaduni uliopitwa na wakati kwa sababu ya athari zake hasi kwa haki za wanawake, uhusiano wa kimapenzi na familia. Ni muhimu kuhamasisha jamii kuondokana na utamaduni huu na badala yake kukuza haki sawa kwa wanawake na wanaume na uhusiano wa kimapenzi ambao unategemea upendo na kujali bila kuangalia thamani ya mahari

Kwa mtazamo huu mtazeeka bila ndoa
 
Mahari hata ukiambia utoe milioni 10 unachotakiwa kutoa hakizidi hata milioni.

Halafu mahari ni mila na desturi za kiafrika, kila jamii ya kiafrika wanayoprocess ya mahari, South Africa hapo wazulu wanaita LOBOLA.
 
Fikra zako kuhusu tamaduni za kishenzi( mahari ) hazina tofauti na wale wazungu na waarabu wa kale walio kuwa na fikra za kishenzi kuhusu tamaduni za kununua na kuuza watu( utumwa )

Zingatia sio kila tamaduni mlizonazo zinapaswa kukumbatiwa kwa kigezo kuwa ni tamaduni zenu na muachwe na tamaduni zenu
Haya sasa, mnaanza matusi na madharau. Ati ni Ushenzi.

Hapo ndipo linapokuja suala la 'Supremacy' haijalishi kudai nina fikra za Wazungu au la- naona unaanza kushindwa kujibu hoja sasa unanipandikizia na kuanza kutafuta njia za kunichefua.

Hamjalazimishwa wala kuombwa kukumbatia tamaduni zezote zile. Mziheshimu tu.
 
Ukitaka kupinga mahari na kupata picha mahusiano yatakuwaje pigia picha hali ya sasa ya mabinti kuzalishwa hovyo halafu kijana aliyezalisha anakuja kujulikana baadae sana mtoto ameshaanza kutembea.

Wazazi wanakubali tu maana watafanyaje maana binti yao kishazalishwa na huyo kijana ndie baba wa mjukuu wao na wameshaunganisha damu.

Sasa pigia picha mahari ikikataliwa tutakuwa katika hali gani kama jamii ya mwafrika. Kijana anayekataa mahari hofu yake sio pesa ya kulipia ile process yote ya posa bali hofu yake ni kurasimisha mahusiano yake na kutambulika ukweni kama mume wa fulani.

Vijana wengi wa sasa courtships hawaziwezi yaani hawawezi ile kitu inaitwa kufuata utaratibu wa mila na desturi zetu waafrika.

Kijana muhuni atataka akutane na binti wapelekane huko kwake walane hadi atosheke na ikibidi ampe na ujauzito kabisa huyo binti halafu akimbie kwa binti mwingine.

Ndio maana miaka hii kuna hizi story za kusikia binti anataka kuolewa na kijana mpya ila ana mtoto au watoto sasa anaomba ushauri afanyaje, au kijana anataka kuoa ila ana mtoto na mwanamke mwingine.

Haya yangepungua sana endapo utaratibu wa mahari ungeheshimiwa na kuboreshwa.
 
Mahari inawapandisha thamani hamjui tu.
Tatizo lenu nyie feminist huwa mnapigania kujimaliza wenyewe.
Bila mahari mtaolewa na kuachika hovyo.
 
Mahari hata ukiambia utoe milioni 10 unachotakiwa kutoa hakizidi hata milioni.
Huo ni mtazamo wa kigeni. Hakuna mohari iliyopewa thamani ya kifedha. Hilo hallikuwepo. Hayo ya milioni au mamilioni waliyoleta ni wageni. Hatahivyo nahisi lugha ya dhihaki.
Halafu mahari ni mila na desturi za kiafrika, kila jamii ya kiafrika wanayoprocess ya mahari, South Africa hapo wazulu wanaita LOBOLA.
Sasa tatizo lipo wapi kama ni mila na desturi za kiafrika?

Suala la mahari linamuingiliano gani na Tohara, ubaguzi wa rangi n.k Je, ni haki gani inayovunjwa au kukandamizwa na mahari?
 
Ukitaka kupinga mahari na kupata picha mahusiano yatakuwaje pigia picha hali ya sasa ya mabinti kuzalishwa hovyo halafu kijana aliyezalisha anakuja kujulikana baadae sana mtoto ameshaanza kutembea.

Wazazi wanakubali tu maana watafanyaje maana binti yao kishazalishwa na huyo kijana ndie baba wa mjukuu wao na wameshaunganisha damu.

Sasa pigia picha mahari ikikataliwa tutakuwa katika hali gani kama jamii ya mwafrika. Kijana anayekataa mahari hofu yake sio pesa ya kulipia ile process yote ya posa bali hofu yake ni kurasimisha mahusiano yake na kutambulika ukweni kama mume wa fulani.

Vijana wengi wa sasa courtships hawaziwezi yaani hawawezi ile kitu inaitwa kufuata utaratibu wa mila na desturi zetu waafrika.

Kijana muhuni atataka akutane na binti wapelekane huko kwake walane hadi atosheke na ikibidi ampe na ujauzito kabisa huyo binti halafu akimbie kwa binti mwingine.

Ndio maana miaka hii kuna hizi story za kusikia binti anataka kuolewa na kijana mpya ila ana mtoto au watoto sasa anaomba ushauri afanyaje, au kijana anataka kuoa ila ana mtoto na mwanamke mwingine.

Haya yangepungua sana endapo utaratibu wa mahari ungeheshimiwa na kuboreshwa.
Hayo yote yangepungua mahari ingefutwa
 
Kwa aina ya wanaume tuliopo hii nchi mahari ni muhimu sana kuwepo,kwasababu inampa mwanamke thamani mbele ya mwanaume.ukiondoa mahari thamani ya mwanamke itaondoka kwasababu wanaume wakiafrika hawajali sana umuhimu wa mwanamke nje ya mapenzi na kuzaa.Kwahiyo wacha iwepo ili wanaume tuangaikie kile chenye thamani kwa nafsi yako.Ukioa bila mahari ata ndoa yenyewe inakua haina thamani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Wanawake Wa kuwapa thamani ndio hawa ma feminist uchwara?
 
Hakuna mwanamke mwenye thamani kama feminist
Feminist hawa hawa wanaotaka 50/50 kwenye maslahi yao Ila kwenye kwenye ishu zinazotaka majukumu na uwajibikaji wanalamba chocho.

Labda feminist Wa nyioko.
 
Mwanaume wa nchi hii akioa mzungu huyo mwanamke wa kizungu anakosa thamani kwa sababu mahari haijatolewa??
Kwa aina ya wanaume tuliopo hii nchi mahari ni muhimu sana kuwepo,kwasababu inampa mwanamke thamani mbele ya mwanaume.ukiondoa mahari thamani ya mwanamke itaondoka kwasababu wanaume wakiafrika hawajali sana umuhimu wa mwanamke nje ya mapenzi na kuzaa.Kwahiyo wacha iwepo ili wanaume tuangaikie kile chenye thamani kwa nafsi yako.Ukioa bila mahari ata ndoa yenyewe inakua haina thamani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Watanzania wanaooa wanawake wazungu wanawalipia mahari?
Thamani ya wanawake wazungu huwa inashuka kwa kutolipiwa mahari?
Mahari inawapandisha thamani hamjui tu.
Tatizo lenu nyie feminist huwa mnapigania kujimaliza wenyewe.
Bila mahari mtaolewa na kuachika hovyo.
 
Watanzania wanaooa wanawake wazungu wanawalipia mahari?
Thamani ya wanawake wazungu huwa inashuka kwa kutolipiwa mahari?
Kwani wanawake wakizungu huwa na thamani tofauti na wanawake weusi/wakiafrika?

Je, huyo mwanamke wa kizungu huwa anaolewa akiwa wapi, manake kama ni kwao pasipo kuwa na maadili au mila na desturi thabiti katika ndoa hilo suala la mahari haliwezi kutokea, sambamba na akiwa hapa Tanzania ndio kabisa anaolewa na Rastaman wa Arusha stendi na mchezo unaishia pale ,tena baada ya yeye kutoa aina ya mahari kwa mume wake.

Mwanamke wakizungu hajawahi kuwa na haki kama aliyokuwa nao Mwanamke Mwafrika. Tambua hilo.
 
Back
Top Bottom