Robidinyo
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 4,043
- 8,686
Msanii Baghdad aliwahi kusema kuwa wazo la kipindi cha The Bartender lilikuwa ni lake na mwanzo wazo lilikuwa TheCounter au The Bartender na alilisajili COSOTA na kubaki na hatimiliki yake. Alishangaa kuona kipindi kinatangazwa wakati makubaliano hayakuwa yametimizwa na kukubaliana. Baghdad anasema kuwa makubaliano yalikuwa ni apate 13% ya mapato yatokanayo na show na idea zote ambazo ataziweka pale Wasafi kuliko kuajiriwa, yaani awe na life-time contract na Wasafi Media.
Baghdad anaendelea kusema kuwa wakiwa katika mchakato wa kusaini mkataba ambao ilionekana kuwa 13% ni kubwa na ishuke hadi 5% ghafla akashangaa kuona promo ya The Bartender, anasema aliamua kuwasiliana na Diamond, cha ajabu Diamond hakuwahi kupokea simu wala kujibu meseji zake. Anasema ilimstua na kuamua kumtafuta Babu Tale, Tale alimsihi sana Baghdad kuwa mtulivu wakati anaongea na Diamond juu ya hili. Alimsihi pia kutofanya chochote mathalani interview popote. Baada ya siku kadhaa Tale na Baghdad walichekiana na kumchana kuwa Diamond kasema fanya chocote unachoweza.
Baghdad aliamua kwenda COSOTA kutafuta haki yake kwa maana hata wazo la Jogoo ni miongoni mwa madini aliyoyatoa Wasafi. Anazidi kusema kuwa, COSOTA waliwaita ili kuwasuruhisha japo Diamond alikuwa akituma wawakilishi, mazungumzo yalifanyika kwa siku kadhaa bila mafanikio na Baghdad kuamua kwenda Mahakamani ili tu haki yake ipatikane.
Kwakeli huu ni utapeli wa kuaminika. Jamaa hawana ubunifu wowote ni wazee wa Kucopy na ku-paste. Walimsema sana Ruge hawa; sasa yule mtoto aliyekua analialia kuonewa kawa mtoto mbaya.