Upumbavu unaoendelea kwenye Taasisi za Umma umefikia kiwango cha kutisha hakika.
Watumishi wa Umma, badala ya kujikita kulitumikia Taifa ili Wananchi wawe na maendeleo sasahivi wamegeuka kuwa vijakazi na watumwa wa CCM. Kuwahudumia CCM badala ya kulihudumia Taifa.
Vitendo vilivyofanywa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulipa watu kuandamana eti kumuunga mkono Samia na CCM ni ishara kubwa sana kuwa Taasisi za Umma nchini zimeshajifia na sasa zinafanya kazi kwa ajili ya CCM na sio Taifa tena.
Kwa hatua tuliyofikia Tanzania, ni dhahili kuwa Taasisi zote zimekuwa compromised na ujinga wa kisiasa ( Political Stupidity) na dawa pekee kulikomboa Taifa ni Jeshi kuchukua hii nchi na kuanza kuisuka na kuijenga upya.
View attachment 3490218View attachment 3490219
Kutegemea jeshi lilete demokrasia, haki na uhuru ni contradiction.
Jeshi linatawala kijeshi na halina guarantee yoyote ya kuheshimu demokrasia, haki wala uhuru wa watu.
In fact jeshi likipindua nchi kitu cha kwanza lina suspend katiba na kutangaza a military council, martial law, curfews and rule by military decrees.
Watanzania wanaotajataja sana jeshi lichukue nchi wengi wana tabia hizi.
1. Wako desperate. Desperate people do desperate things. Mfa maji haishi kutapatapa. Mtu anayezama hata akiona unywele ataushika ili asizame.
2. Wavivu. Watu wavivu wanapenda kuwapangia wengine wafanye kazi wanayotakiwa kufanya wao. Badala ya wao kufanya wajibu wao kuitoa serikali wanayoona dhalimu madarakani, wanalisukumia wajibu huo jeshi.
3. Wanapenda shortcuts. Badala ya kufanya kazi kubwa na nzito ya kuelimisha jamii ili jamii ijue uhuru ni nini, ifanye mabadiliko ya kimsingi ya kijamii, wanakimbilia shortcut ya kutaka jeshi lichukue madaraka.
4. Wanapenda kutumia nguvu kuliko kutumia akili. Ni watu ambao wanaona jeshi ni alama ya kutumia nguvu. Wanaamini katika kutumia nguvu sehemu ambayo panatakiwa kutumia akili. Wanapenda show za kibabe. Ndiyo maana hata marais ambao hawamo jeshini ukiondoa vyeo vya kisiasa kama Commander In Chief, wanapenda kuvaa magwanda ya kijeshi. Wanasiasa washajua wakivaa magwanda ya kijeshi wananchi wanalainika. Just the projection of military power does it for most Tanzanians.
5. Hawana akili za kuangalia mambo kama unintended consequences, bad precedent, na madhara ya muda mrefu ya mapinduzi ya kijeshi. Kifupi ni watu wenye akili fupi sana ambao hawawezi kupima mambo kwa kina.