Jeshi likichukua nchi kuta kitu hata CCM watajifunza watanzania wengi wanataka tukose wote wanaotaka Jeshi lichukue nchi wanataka na CCM wakose wajifunze wana hoja
Tutakosa wote vipi wakati jeshi kwa kiasi kikubwa ni CCM?
Wewe huoni wanajeshi wanavyoingizwa kwenye siasa, tena wote CCM, wengine mpaka kinyume na kanuni za "civilian control of the military"?
Huelewi wapi?
Jeshi lenyewe jeshi gani wanajeshi wenyewe hawa wanafadhiliwa na kujazwa itikadi za CCM tangu enzi za chama kimoja?
Kwa nini mnataka kuwafanya wanajeshi wa Tanzania kuwa ni watu independent na exceptional sana?
Kwa nini hamuelewi kuwa jinsi nyie raia mlivyoshindwa kubadili kitu na wanajeshi nao wameshindwa hivyo hivyo?
Hamuelewi wapi? Hamuelewi kuwa ukiona wanajeshi wanalialia mitandaoni kama raia maana yake na wao wenyewe wana woga kama raia tu, nyie wote ni Watanzania mna tabia ya uoga ile ile tu, bila kujali mtu ni mwanajeshi au raia.
Wanajeshi Tanzania walishamkimbiza rais Ikulu, rais Nyerere akakimbilia Kigamboni na Kawawa na mlinzi wake Peter Bwimbo.
Wanajeshi kufika Ikulu badala ya kuchukua nchi, wakasema wao hawana nia ya kuchukua nchi wanapigania maslahi yao tu.
Hawa ndio wanajeshi unaotaka wachukue nchi?
Wanajeshi wa Tanzania wameshakuwa shaped kutii amri ya uongozi wa kiraia, uongozi wa CCM. Ndiyo maana Mabeyo alivyopewa mpango wa kumuweka rais tofauti na Samia baada ya Magufuli kufariki, alikataa, akasema atailinda katiba.
Hamuelewi wapi?
Wanajeshi wenyewe si ndio hawahawa kila siku tunasikia wanapiga vibaya raia kwa mambo minor tu?
Wanajeshi gani? Hawa wanaoongozwa na top brass wanaosema wao wanatetea katiba tu?
Wanajeshi gani mnawategemea ambao mnawaona wana integrity sana kiasi hawawezi kufanya vibaya hata zaidi ya hawa mafisadi wa sasa?
Hawa wanajeshi si ndio hawa wameingia kwenye scandal za kutapeli watu wakiwaahidi kuwapa kazi jeshini?
Hawa wanajeshi si ndio wamepiga hela kwenye scandals za radar mpaka Waingereza wakaturudishia pesa zetu, Claire Short akalazimisha kurudisha pesa kwa huruma tu ?
Unaijua scandal ya radar na BAE? Unajua jeshi lilivyohusika?
Unajua ufisadi jeshini? Unajua scandals za manunuzi ya silaha katika jeshi la Tanzania? Unajua wanajeshi wakubwa wanahusika? Unajua kuwa Watanzania wana utamaduni wa kuwaheshimu tu wanajeshi lakini na wao wengi ni mafisadi tu?
Hawa wanajeshi si ndio wamepiga hela za scandal ya Meremeta?
Ulifuatilia scandal ya Meremeta?
Sasa kama wanajeshi nao wanafanya ufisadi huohuo mnaotaka kuukataa CCM, mnategemeaje wanajeshi wamalize ufisadi?
Hamuoni kuwa mtakuwa mmeutoa ufisadi wa kina Samia nyoronyoro hawa, mnataka kuuweka ifisadi wa kina Sani Abacha wa mtutu wa bunduki?