GE2025 Tunaposema Jeshi lichukue Nchi kwa sababu Taasisi zote zimejifia tueleweni jamani

GE2025 Tunaposema Jeshi lichukue Nchi kwa sababu Taasisi zote zimejifia tueleweni jamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwani kwa Sasa Kuna utawala wa kisheria au kikatiba?
Sasa kama mgonjwa anaumwa tiba yake ni kumuua kabisa?

Kwa nini unataka kutatua tatizo la utawala wa sasa kutofuata katiba kwa kuweka utawala wa kijeshi ambao kawaida yake ni ku suspend utawala wa kikatiba na kuweka baraza la kijeshi ambalo halilazimiki kufuata katiba?

Hivi mnaelewa utawala wa kijeshi ni nini?

Hizi nchi zote za Africa zilizopata matatizo mengi sana kwa sababu ya utawala wa kijeshi hamjajifunza kitu?

Mnaelewa kuwa mkishahalalisha wanajeshi kupindua nchi mmehalalisha si tu kumpindua huyo Samia na CCM ambao hamuwapendi, bali rais yeyote mwingine pia?
 
Upumbavu unaoendelea kwenye Taasisi za Umma umefikia kiwango cha kutisha hakika.

Watumishi wa Umma, badala ya kujikita kulitumikia Taifa ili Wananchi wawe na maendeleo sasahivi wamegeuka kuwa vijakazi na watumwa wa CCM. Kuwahudumia CCM badala ya kulihudumia Taifa.


Vitendo vilivyofanywa na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulipa watu kuandamana eti kumuunga mkono Samia na CCM ni ishara kubwa sana kuwa Taasisi za Umma nchini zimeshajifia na sasa zinafanya kazi kwa ajili ya CCM na sio Taifa tena.

Kwa hatua tuliyofikia Tanzania, ni dhahili kuwa Taasisi zote zimekuwa compromised na ujinga wa kisiasa ( Political Stupidity) na dawa pekee kulikomboa Taifa ni Jeshi kuchukua hii nchi na kuanza kuisuka na kuijenga upya.

View attachment 3490218View attachment 3490219

Updates
Uthibitisho mwingine wa namna Taasisi za hili Taifa zilivyojifia ni namna walivyomfanyia John Heche wakati anaenda Msibani jana ba hili tamko walilolitoa jana Uhamiaji wa Tanzania

Kwa akili za kawaida tu kila mwananchi ameona kilichotokea jana na nguvu ya Umma ilivyotumika kumuingiza Heche Kenya alafu hawa wapumbavu Uhamiaji kwa ajili ya kutumika kisiasa tu wamekuja na tamko hili la kipuuzi.
View attachment 3490570
Jeshi haliwezi kuchukua nchi bila ya nyie kutoka alafu wajichanganye na nyie
 
Hivi mkuu hao wanajeshi unawaamini kiasi gan? Una uhakika wataweza kuheshimu katiba ya nchi?
Tuache fikra za ajabu watanzania tubadilike. Hata mtoa mada ukipewa nchi leo, ni wazi utakuwa fisadi, maana naona ubinafsi mkubwa kwenye maandishi yako.
There are indeed some invisible forces dictating the throne.
 
Jeshi haliwezi kuchukua nchi bila ya nyie kutoka alafu wajichanganye na nyie
Mkuu,

Kwa nini Watanzania hawaelewi somo hili jepesi kabisa?

Ni kwa sababu ni wavivu na waoga wanalitegea jeshi lifanye kazi wanayotakuwa kufanya wao?

Ni kwa sababu ni watu wa kupenda shortcuts hawaelewi kuwa hata ukiwaweka wanajeshi, kama huna uwezo wa kuwasimamia viongozi hutabadili kitu, in fact ukiweka wanajeshi ndiyo utapata tabu zaidi kuwasimamia kwa sababu wao wata suspend katiba na kutawala kijeshi?

Ni kwa sababu ni watu wanaopenda kutumia nguvu kuliko akili na jeshi ndiyo linaonekana lina nguvu?

Kwa nini watu hawaelewi kuwa jukumu la msingi ni la wananchi?

Hawa wananchi wasioelewa kanuni muhimu ya "civilian control of the military" ndiyo hawa wanataka jeshi lichukue madaraka, wanaelewa hili maana yake ni kujipunguzia uhuru wao wenyewe?
 
Sasa kama mgonjwa anaumwa tiba yake ni kumuua kabisa?

Kwa nini unataka kutatua tatizo la utawala wa sasa kutofuata katiba kwa kuweka utawala wa kijeshi ambao kawaida yake ni ku suspend utawala wa kikatiba na kuweka baraza la kijeshi ambalo halilazimiki kufuata katiba?

Hivi mnaelewa utawala wa kijeshi ni nini?

Hizi nchi zote za Africa zilizopata matatizo mengi sana kwa sababu ya utawala wa kijeshi hamjajifunza kitu?

Mnaelewa kuwa mkishahalalisha wanajeshi kupindua nchi mmehalalisha si tu kumpindua huyo Samia na CCM ambao hamuwapendi, bali rais yeyote mwingine pia?
Ili kila Rais atayefuata baada ya hapo awe anaongoza kwa kuzingatia sheria na katiba.

Yaani awe na tahadhari kuwa akifanya ujinga tu muda wowote anatolewa. Tunatamani kuwa na Rais ambaye hatakuwa na uhakika wa kesho yake, kwamba nitafanya lolote na hamna cha kunifanya.

Tunataka mtu atakayekuwa Rais ajue kuwa uhakika wa kesho yake ni kwa kufanya yale wanayoyataka waliompa kazi. Rais asiwe anafikiria kwa niaba yetu bali awe anatekeleza vile tunavyovitaka sisi kupitia wabunge wetu
 
Yakitokea Maandamano Makubwa ,JWTZ litachukuwa Mamlaka ya nchi Kwa mpito na Kufanya Yale wananchi wanacho andamanania, kama ni katiba au mambo mengine.......Mbona Nepal imewezekana......Najua humu watu wengine mmemezeshwa baadhi ya story za jeshi na CCM.....ila ngoja itoke uone Hatua zitakazo chukuliwa
 
Kutegemea jeshi lilete demokrasia, haki na uhuru ni contradiction.

Jeshi linatawala kijeshi na halina guarantee yoyote ya kuheshimu demokrasia, haki wala uhuru wa watu.

Watanzania wanaotajataja sana jeshi lichukue nchi wengi wana tabia hizi.

1. Wako desperate. Desperate people do desperate things. Mfa maji haishi kutapatapa. Mtu anayezama hata akiona unywele ataushika ili asizame.

2. Wavivu. Watu wavivu wanapenda kuwapangia wengine wafanye kazi wanayotakiwa kufanya wao. Badala ya wao kufanya wajibu wao kuitoa serikali wanayoona dhalimu madarakani, wanalisukumia wajibu huo jeshi.

3. Wanapenda shortcuts. Badala ya kufanya kazi kubwa na nzito ya kuelimisha jamii ili jamii ijue uhuru ni nini, ifanye mabadiliko ya kimsingi ya kijamii, wanakimbilia shortcut ya kutaka jeshi lichukue madaraka.

4. Wanapenda kutumia nguvu kuliko kutumia akili. Ni watu ambao wanaona jeshi ni alama ya kutumia nguvu. Wanaamini katika kutumia nguvu sehemu ambayo panatakiwa kutumia akili. Wanapenda show za kibabe. Ndiyo maana hata marais ambao hawamo jeshini ukiondoa vyeo vya kisiasa kama Commander In Chief, wanapenda kuvaa magwanda ya kijeshi. Wanasiasa washajua wakivaa magwanda ya kijeshi wananchi wanalainika. Just the projection of military power does it for most Tanzanians.

5. Hawana akili za kuangalia mambo kama unintended consequences, bad precedent, na madhara ya muda mrefu ya mapinduzi ya kijeshi. Kifupi ni watu wenye akili fupi sana ambao hawawezi kupima mambo kwa kina.
Huna akili pumbavu zako , yaani kwa haya yanayotendws na serikali ya CCM plus ubovu wa mfumo mbovu wakiutala bado hutamani kupata njia mbadala ya kulisalisha Taifa utakuwa na akili timamu sasa , hapa Ngoma imekaa vibaya hakuna namna nyingine CCM must go
 
Ili kila Rais atayefuata baada ya hapo awe anaongoza kwa kuzingatia sheria na katiba.

Yaani awe na tahadhari kuwa akifanya ujinga tu muda wowote anatolewa. Tunatamani kuwa na Rais ambaye hatakuwa na uhakika wa kesho yake, kwamba nitafanya lolote na hamna cha kunifanya.

Tunataka mtu atakayekuwa Rais ajue kuwa uhakika wa kesho yake ni kwa kufanya yale wanayoyataka waliompa kazi. Rais asiwe anafikiria kwa niaba yetu bali awe anatekeleza vile tunavyovitaka sisi kupitia wabunge wetu
Ukisharuhusu mapinduzi ya kijeshi mara moja umeruhusu mapinduzi ya kijeshi mara zote.

Kwa marais wote, wanaofuata katiba na wasiofuata katiba.

Maana yake nyie mtampindua rais wa CCM mkamuweka wenu, na CCM nao watatafuta wanajeshi wao na kumpindua rais wenu.

Angalia nchi zote zenye mapinduzi ya kijeshi huwa na tabia ya kurudiarudia mapinduzi hayo, usijidanganye kuwa utafanya mapinduzi mara moja tu.

This is like the proverbial genie out of the bottle.

Once out, you can't contain it.

Huelewi wapi?

Unataka kumpanda Chui mgongoni akufikishe unakotaka kwa kasi, wakati ukishampanda huyo Chui huna namna ya kum control aende wapi, huna namna ya kumsimamisha kumwambia hapa nishafika ninapotaka kwwnda, na hata ukiweza huna uhakika ukishuka hatakuua.

Huelewi wapi?
 
Mkuu, huelezi hao wananchi wanatakiwa kufanya nini? Hilo jukumu lao la msingi huelezi walifanyaje. Toa ufafanuzi
Hili nalo ni tatizo la msingi.

Wananchi wasiojua wanataka nini ni tatizo.

Wananchi wanatakiwa kuwa na ownership ya mambo yao, kupanga wanachotaka.

Si kusubirisubiri waambiwe tu wafanye nini.
 
Sasa kama mgonjwa anaumwa tiba yake ni kumuua kabisa?

Kwa nini unataka kutatua tatizo la utawala wa sasa kutofuata katiba kwa kuweka utawala wa kijeshi ambao kawaida yake ni ku suspend utawala wa kikatiba na kuweka baraza la kijeshi ambalo halilazimiki kufuata katiba?

Hivi mnaelewa utawala wa kijeshi ni nini?

Hizi nchi zote za Africa zilizopata matatizo mengi sana kwa sababu ya utawala wa kijeshi hamjajifunza kitu?

Mnaelewa kuwa mkishahalalisha wanajeshi kupindua nchi mmehalalisha si tu kumpindua huyo Samia na CCM ambao hamuwapendi, bali rais yeyote mwingine pia?
Nimekuuliza katiba na Sheria zinafuatwa kwa Sasa? Jibu swali zinafuatwa au hazifiatwi ?

Kuna tofati gani kuwa na utawala wa Samia na wa kijeshi?

Kuwa na utawala kiini macho si ni Bora tuwe na utawa wa kijeshi tu tuishi kwa amri Basi

Kuliko kujodanganya kwamba tupo kwenye utawala wa kiraia wakati nchi inatawaliwa with no rules of law na ufisadi juu

Kwa sababu kwa Sasa sioni Sheria yeyote inayofuatwa Tanzania

Ila kimeongezeka utekaji na urawiti na mauaji ya watu

Bora jeshi lichukue nchi kwanza kuliko kuongozwa nanwahuni wavaa hijab na suti kumbe wezi na watekaji na majambazi!!
 
Huna akili pumbavu zako , yaani kwa haya yanayotendws na serikali ya CCM plus ubovu wa mfumo mbovu wakiutala bado hutamani kupata njia mbadala ya kulisalisha Taifa utakuwa na akili timamu sasa , hapa Ngoma imekaa vibaya hakuna namna nyingine CCM must go
Wewe ndiye unasumbuliwa na fikra finyu.

Kwa sababu badala ya kuchambua hoja umenishambulia mimi binafsi.

This is a logical fallacy, ad hominem logical fallacy.

Halafu pia una uwezo mdogo wa kufikiri. Hujui kusoma kwa ufahamu.

Umefanya logical fallacy nyingine ya logical non sequitur.

Kukataa utawala wa kijeshi si kukataa kupata njia mbadala, ni kukataa kupata njia mbadala ya utawala wa kijeshi. Kuna njia mbadala nyingine ambazo hazihusishi utawala wa kijeshi.

Hapa umefanya logical fallacy nyingine, false dichotomy.

Umefanya kuwa mambo yanayoweza kuwepo ni mawili tu, uongozi wa ufisadi huu tulionao au mapinduzi ya kijeshi. Mimi nakataa options zote hizi mbiki. Nakataa uobgozi wa sasa wa kifisadi na nakataa mapunduzi ya kijeshi pia.

Hujaweza kufungua akili yako na kuona kuwa, kwa mfano, watu wanaweza kuandamana mpaka kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa popular uprising isiyotumia mapinduzi ya kijeshi.

Kwa nini unalazimisha hii false dichotomy ya "uongozi wa kifisadi au mapinduzi ya kijeshi" tu?
 
Mimi sio muumini wa majeshi kuchukua nchi, jeshi kuchukua nchi maana yake ni kuziweka sheria kando kwa muda, hapa ni kutengeneza tatizo kubwa zaidi ya tulilo nalo. Majeshi yakionja utamu wa kutawala ni balaa jingine.

Kuhusu taasisi kujifia, nadhani tuna tatizo kubwa sana katika taasisi za umma, hata hao unaowalalamikia sidhani kama wanafanya huo upuuzi kwa kupenda, ni uchawa na kujitahidi kujipendekeza ili waendelee kupendwa na mamlaka za uteuzi.

Watumishi wa umma mimi huwa nashangaa sana wanapojiingiza katika vitendo vya uchawa na kupigania chama tawala. Wanashindwa kutambua kwamba, hata CCM ikiondoka leo na chama kingine kikachukua madaraka, wao wapo na wataendelea kuwepo katika utumishi wao. Hakuna chama kitakachopata madaraka halafu kije na watamishi wapya wa umma. Yaani uingie madarakani ufukuze polisi, uhamiaji, watumishi wa balozi zote, hili litawezekana vipi?

Labda ni kutokana na vile wanavyotumwa kuwanyanyasa wapinzani ndio wanadanganywa wakishika madaraka watawafukuza wote.
​
 
Nimekuuliza katiba na Sheria zinafuatwa kwa Sasa? Jibu swali zinafuatwa au hazifiatwi ?

Kuna tofati gani kuwa na utawala wa Samia na wa kijeshi?

Kuwa na utawala kiini macho si ni Bora tuwe na utawa wa kijeshi tu tuishi kwa amri Basi

Kuliko kujodanganya kwamba tupo kwenye utawala wa kiraia wakati nchi inatawaliwa with no rules of law na ufisadi juu

Kwa sababu kwa Sasa sioni Sheria yeyote inayofuatwa Tanzania

Ila kimeongezeka utekaji na urawiti na mauaji ya watu

Bora jeshi lichukue nchi kwanza kuliko kuongozwa nanwahuni wavaa hijab na suti kumbe wezi na watekaji na majambazi!!

Kama katiba haifuatwi sasa, utawala wa kijeshi ndiyo utafuata katiba?

Unaelewa utawala wa kijeshi ni nini?

Unaelewa maana ya "two wrongs do not make a right"?

Unaelewa maana ya false dichotomy logical fallacy?

Kwa nini unalazimisha vitu pekee vya kuchagua viwe utawala huu wa kifisadi au mapinduzi ya kijeshi?

Umeshindwa kuona kingine chochote zaidi ya njia hizo mbili?
 
Mimi sio muumini wa majeshi kuchukua nchi, jeshi kuchukua nchi maana yake ni kuziweka sheria kando kwa muda, hapa ni kutengeneza tatizo kubwa zaidi ya tulilo nalo. Majeshi yakionja utamu wa kutawala ni balaa jingine.

Kuhusu taasisi kujifia, nadhani tuna tatizo kubwa sana katika taasisi za umma, hata hao unaowalalamikia sidhani kama wanafanya huo upuuzi kwa kupenda, ni uchawa na kujitahidi kujipendekeza ili waendelee kupendwa na mamlaka za uteuzi.

Watumishi wa umma mimi huwa nashangaa sana wanapojiingiza katika vitendo vya uchawa na kupigania chama tawala. Wanashindwa kutambua kwamba, hata CCM ikiondoka leo na chama kingine kikachukua madaraka, wao wapo na wataendelea kuwepo katika utumishi wao. Hakuna chama kitakachopata madaraka halafu kije na watamishi wapya wa umma. Yaani uingie madarakani ufukuze polisi, uhamiaji, watumishi wa balozi zote, hili litawezekana vipi?

Labda ni kutokana na vile wanavyotumwa kuwanyanyasa wapinzani ndio wanadanganywa wakishika madaraka watawafukuza wote.
​
Mkuu,

Ni ujinga mkubwa sana kutaka jeshi lichukue madaraka ili upate haki, demokrasia na uhuru.

Kwa sababu jeshi linatawala kwa amri ya kijeshi bila kujali haki, demokrasia wala uhuru.

Nimeandika hapo juu kwa nini hii hoja ni ujinga.

Watu wanalilia utawala wa kijeshi hawajui hata utawala wa kijeshi maana yake nini.

Post #9

Post in thread 'Tunaposema Jeshi lichukue Nchi kwa sababu Taasisi zote zimejifia tueleweni jamani' Tunaposema Jeshi lichukue Nchi kwa sababu Taasisi zote zimejifia tueleweni jamani
 
Mimi napenda sana muziki.

Katika muziki ninaofuatilia, napenda sana muziki wa reggae. Na si reggae ya Bob Marley na Peter Tosh tu hii inayojulikana sana, nasikiliza reggae mpaka za wasanii ambao hawajulikani sana.

Napenda reggae kwa maudhui na dhima zake za mapenzi, za uanamapinduzi, za counter culture etc.

Ninaposikiliza reggae sisikilizi midundo na ala tu, nasikiliza mpaka mashairi. Nimesikiliza reggae sana mpaka naweza kusikia na kuongea Jamaican patois vizuri tu.

Katika kusikiliza reggae kuna wimbo mmoja wa mwanamuziki anaitwa Anthony B nimeupenda sana.

Wimbo unaitwa "Raid The Barn".

Katika wimbo huu, Anthony B anaanza kwa kuimba.

"Nobody wants to raise the corn
Everybody wants to raid the barn
Who are you going to blame it upon
When it's the next man you are depending on?"

Kimsingi Anthony B anahadithia hadithi ya watu wavivu ambao hawataki kupanda mahindi, hawataki kuvuna mahindi.

Wanasubiri mpaka mtu mwingine alime mahindi, avune mahindi, ayaweke kwenye ghala.

Halafu mahindi yakishawekwa katika ghala, hawa watu wavivu ambao hawajashiriki kulima wala kuvuna ndio wanakuja kwenye ghala na wao wanataka wapewe mahindi.

Kimsingi wimbo unaonya watu wavivu ambao hawataki kufanya kazi ngumu ya kutengeneza vitu vizuri kwa jasho, lakini wanakuwa wa kwanza kuachia wengine watengeneze, halafu wao waje kupata mazao ya kazi tu.

Watanzania wanaopenda kuliachia jeshi lifanye mapinduzi, kazi ambayo wanatakiwa kushiriki wao, kimsingi ndio kama hao aliowasema Anthony B hawataki kupanda mahindi wala kuvuna wanasubiri mahindi yawe kwenye ghala wao wapewe mazao ambayo yapo tayari tu.


View: https://youtu.be/1S8Ha__cJgY?si=s18Ri5r2zAp6ExF-

Raid the Barn

Song by Anthony B ‧ 1996

Yugguh Yoi, Yugguh Yoi, Yugguh Yoi
Emperor Selassie I
Jah Jah is the only way

Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who yuh a guh blame it on
When is a next man yuh a depend pon
Well yuh wrong
Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Haffi sing yuh owna song
Can't compete with careless John

I was looking a start, Just a likkle ease off
Noone would help me push that old hand caart
Dem a laugh, never tak mi serious
So many goals and thoughts as potholes I pass everyday
My Lord, I have to pray on my way
Dem never realise with a little cooperation
Wi coulda unify relieve the frustration
Instead dem want to ride upon dem bredda back
No tears or cares if him even did stop or drop

Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who yuh a guh blame it on
When is a next man yuh a depend pon
Well yuh wrong
Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Haffi sing yuh owna song
Can't compete with careless John

I feel pleased, when I take a likkle ease
From a long hard day of work
A sense of achieving, to know I'm contributing
Doing my part, oooowi dis is my comfort
I know there is a reward for every trying man
Who walk this land with an intention
To do good for his self and everyman
Just a meditation
Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who yuh a guh blame it on
When is a next man yuh a depend pon
Well yuh wrong

Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Haffi sing yuh owna song
Can't compete with careless John

Well Ive been up from early this morning
Never drink nuh tea, mi never eat nuh fry dumpling
Never see noone to strengthen me on mi journey
Now mi mek a change di whole a dem waan fi fren mi
Waan fi take it all, nuh mind if mi stall
Dem nuh business if mi back gainst the wall
Dis yah living sometime mek mi ball
Seems like there ain't no love afterall
Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who yuh a guh blame it on
When is a next man yuh a depend pon
Well yuh wrong
Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Haffi sing yuh owna song
Can't compete with careless John
I was looking a start, Just a likkle ease off
Noone would help me push this old hand caart
Dem a laugh, never tak mi serious
So many goals and thoughts as potholes I pass everyday
My Lord, I have to pray on my way
Dem never realise with a little cooperation
Wi coulda unify relieve the frustration
Instead dem want to ride upon dem bredda back
No tears or cares if him even did stop or flop

Nobody wannu plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who yuh a guh blame it on
When is a next man yuh a depend pon
Well yuh wrong

Source: LyricFind
Songwriters: Richard Bell
 
Hivi mkuu hao wanajeshi unawaamini kiasi gan? Una uhakika wataweza kuheshimu katiba ya nchi?
Tuache fikra za ajabu watanzania tubadilike. Hata mtoa mada ukipewa nchi leo, ni wazi utakuwa fisadi, maana naona ubinafsi mkubwa kwenye maandishi yako.
Kwahiyo ni bora kuendelea hivi hivi?
 
Kama katiba haifuatwi sasa, utawala wa kijeshi ndiyo utafuata katiba?

Unaelewa utawala wa kijeshi ni nini?

Unaelewa maana ya "two wrongs do not make a right"?

Unaelewa maana ya false dichotomy logical fallacy?

Kwa nini unalazimisha vitu pekee vya kuchagua viwe utawala huu wa kifisadi au mapinduzi ya kijeshi?

Umeshindwa kuona kingine chochote zaidi ya njia hizo mbili?
Ukweli ni kwamba Taasisi zote na mifumo yote nchi hii imekuwa compromised vibaya sana. Elewa neno vibaya sana.

Nchi hii sasahivi watumishi na mifumo inaiabudu CCM kuliko Katiba na Taifa.


Si Mahakama, Si Tume ya Uchaguzi, si TISS, si Polisi, si TAKUKURU, si Uhamiaji si Magereza si DPP si Mwanasheria Mkuu si Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora si Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Hakuna namna nchi hii inaweza kujengwa vizuri sasa bila kufanyiwa overhaul.


Na njia pekee iliyopo ya kufanya overhaul na kuanza kujenga mifumo na Taasisi upya inayoweza kufanikiwa lazima ilihusishe Jeshi.


Nchi hii imeoza
 
Back
Top Bottom