Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania , Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania .

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa , bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu .

Narudia tena , " Mungu Wabariki Wazungu"
Wake up acha ujinga marekani hajawahi kutoa msaada usio na faida kwake. So unataka kuniambia ile midege yote kaja kutoa msaada. Is a money trap wanataka kutafuta kuungwa mkono kwenye vita na urusi
 
Huyu jamaa ndie mpiga debe namba moja wa Chadema humu ndani. Usitake kukidhalilisha chama chako namna hii.
Unaposema kudhalilisha unamaanisha nini ? kwamba Chadema haitambui ziara ya makamu wa Rais wa Marekani au haitaki misaada ya Marekani ?

Kingine usichokijua ni hiki , tunapoandika humu tunalenga kutoa taarifa tu , hatulengi kumfurahisha yeyote yule .
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania , Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania .

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa , bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu .

Narudia tena , " Mungu Wabariki Wazungu"

Wale jamaa washashika calculator wanapiga hesabu waongeze ngapi kwenye Invoice, tunapigwa tu kila siku
 
$7.5b ya Power Africa ilikuwa kwa bara zima na nchi nyingi tu zilipata pesa kwa ajili ya sekta ya umeme. Pesa huwa zinatolewa labda tatizo huwa ni kuwafikia walengwa masikini.
Hapo wa kuwajibishwa ni serikali sasa.
Mkuu hizo ni ahadi hewa, marais wote US waliokuja Tanzania na waliishia kutoa ahadi hewa. Obama alipokuja aliahidi kutoa $7.5b kwa ajili ya powerpull kwa Tanzania ili iweze kuwa msambazaji mkubwa wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara. Usiwaamini sana hao matapeli.
 
Kama kuna mtu huwa anakuelewa basi huyo mtu ni bonge la kiazi
Ukweli husimama daima. Kwahiyo wewe unataka wazungu (wamarekani) walaaniwe? Chanjo mbalimbali mtapata wapi? ARV mtapata wapi? ona matangazo mbali2 kwenye tv mwisho utaona imekujia kwa ufadhili wa watu wa marekani (USAID) Huwezi ona urusi wala iran na wanaofanana na hao. Unakumbuka kuna mwaka wa-tz tulitaka kufa na njaa hawa jamaa wakaliokoa taifa kwa kuleta mahindi ya njano. Wewe wachukie wazungu huku ukiwa unafaidika na vitu vya wazungu.
 
Hawa vijana Wajinga hawawezi kukuelewa
 
Back
Top Bottom