Aaaah!Ngoja kwanza , hapa sijakuelewa , nimeweka ya CAG ili kuonyesha uvumilivu wa Wazungu kwa uchafu wetu , yaani pamoja na kwamba ndani yetu wamo panya buku lakini wao hawachoki kutupa chakula .
Kwa hiyo hii ni sehemu ya "mapenzi yao kwetu", pamoja na ujuha tulionao?
Haya mapenzi yao mbona yanatulemaza vile.
Kama una mtoto, unampenda, unamlea kama yai na kumlemaza akili kabisa; haya ni mapenzi kweli, mkuu wangu Erythro'?
Huyu mtoto, si unamvurugia maisha yake moja kwa moja?