Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Sasa mimi ndio kiazi au huyo anayenielewa ? nadhani niite mimi kiazi badala ya wanaonielewa , napokea matusi ya aina zote .
Hawajitambui hawa. Na ndiyo maana hawajui ni kwanini dunia ni moja lakini waafrika tunaambiwa tupo dunia ya tatu. Na ndani yake kuna nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea. Na zingine hazijaanza hata kuhisi nini maana ya kuendelea. S. Sudan nk. Mataifa mengi ya Afrika yalipata uhuru 1960-. Kinyume cha uhuru ni utumwa, kutumikishwa na wazungu. Marekani ilikuwa huru 1776 kama skosei Tanganyika 1961 tofauti ya zaidi ya miaka 185, leo tunataka tufanane na marekani?. Aliyekuzidi amekuzidi tu. Tuendelee kuiba kura kwenye uchaguzi, na kuwauzia wazungu madini yetu. Pia waje wayachimbe maana hatuna zana za kuchimbia, tena waje kuona mbuga zetu watupe pesa. Mkuu Erythrocyte achana na hawa wanaoujua ukweli (kama kweli wanaujua) lakini wanajitoa ufahamu.
 
Unafahamu ni kampuni ngapi za kimarekani zilizopo hapa Nchini hasa zinazojishughulisha na Nishati na Madini?

Unafahamu kiasi cha fedha wanachotengeneza?

Unadhani USA ni wajinga ndani ya miaka 10,viongozi wao 2 wakubwa kiutawala wamekuja Tanzania.
 
.
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania , Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania .

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa , bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu .

Narudia tena , " Mungu Wabariki Wazungu"
........kabla hata hatujawaombea baraka tayari wameshabarikiwa, wanafanya kazi kwa bidii, wanalipa kodi na hizo Kodi wanatupatia sisi tule........basi watazidi kubarikiwa coz Mungu anabariki mkono utoao na sio upokeao, sisi tuendelee kula vya watu huku tukitumikia laana zetu......hakuna namna nyingine kama kila mwaka tunashindwa kujirekebisha kutokana na repoti mbovu za CAG.........lakini nawasihi ipo siku Mungu atatenda makuu juu ya hii race ya kiafrika, tutaamka kutoka usingizini, tuendelee tu kuelimishana tusichoke, Mungu ibariki Africa, na wote tuseme Amina.......
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania , Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania .

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa , bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu .

Narudia tena , " Mungu Wabariki Wazungu"
Na wewe ni miongoni mwa watu wanaopambania kweli upinzani

Daaaah kweli Taifa lina safari ndefu sana kama upinzani wenyewe ni wa aina hii.
 
Mungu nisaidie nitoke salama kwenye uzi huu yaani nisikorofishane na Moderators wa JF. Naomba msaada wako Muumba, huu uzi si salama kabisa kwangu.
Unatumia device ya wazungu halafu unadai uzi huu si salama !
 
Ndoto za CHADEMA hizi.
Nawaombeni sana Watanzania/Wananchi kupiga kura kwa Umakini mkubwa sana, tena, sana sana 2024-2025

**Hii bandiko limepata ridhaa CHADEMA, upo uwezekano mkubwa sana. *Sio siri * ...ndio itakuwa sera yao ya mambo ya Nje.





Na uhakika hata wazungu wanashangazwa na
wanashangazwa kweli na mtoa mada kwa sababu wao wanajua wanatoa Misaada kwa mambo mawili tu..

1. Kuondoa hatia ya uovu[guilty conscious] walioufanya mababu zao wa mababu na wenyewe yaani (laana ikiwa ni pamoja na uovu wanaoendelea kuufanya) ambao hauwaridhishi na kuwaacha na hatia zaidi na...

2. Kupata unafuu kwenye kodi.... Yaani, wako tayari kutoa msaada wa bilioni moja badala ya kutoa dola milioni moja kumsaidia mfanyakazi wao anayehangaika. Ilimradi wanalipa kodi ndogo sana ambazo zingeweza kumsaidia mfanyakazi wake....nje ya kazini kwake.

Sina hata sumni ya fikra kama za mtoa mada. I beg to differ.
 
... yaani Marekani awagawie ARV's za bure ili mumuunge mkono? Watu mnaharisha ukimwi mnamuunga mkono kwa lipi? That's just a humanitarian aid elewa hilo Mkuu.
Nab alikwambia arv zinatolewa bure. Wake up nyie watu ndo maana wazungu wanatuona wapumbavu
 
Back
Top Bottom