Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Ukweli husimama daima. Kwahiyo wewe unataka wazungu (wamarekani) walaaniwe? Chanjo mbalimbali mtapata wapi? ARV mtapata wapi? ona matangazo mbali2 kwenye tv mwisho utaona imekujia kwa ufadhili wa watu wa marekani (USAID) Huwezi ona urusi wala iran na wanaofanana na hao. Unakumbuka kuna mwaka wa-tz tulitaka kufa na njaa hawa jamaa wakaliokoa taifa kwa kuleta mahindi ya njano. Wewe wachukie wazungu huku ukiwa unafaidika na vitu vya wazungu.
Umejitutumua sana hapa.

Hoja yako inahitaji jibu, sijui nani atajibu ili umuelewe vizuri.
Mimi shaweka mabandiko yangu hapa mfululizo, sasa sijui kama itasaidia chochote kuongeza bandiko lingine.

Ngoja nitumie mfano mfupi: Unajua hadi sasa hivi kiasi cha pesa alichotoa rafiki yetu huyu kwa nchi ya Ukraine? Zaidi ya bilioni 30 ya pesa yake, na bado anaendelea kutoa misaada.

Basi tuseme anawapenda zaidi watu wa huko kuliko waTanzania ambao manusra wafe kwa njaa wakati ule alipotoa msaada, na karibu kila mwaka anatoa vimisaada! Kama bado hujaona maana ya swali langu, sina njia nyingine ya kukufafanulia zaidi ila kusema ni "maslahi" tu.

Ni hivi: hapa hupewi msaada utakaokuwezesha kujiondoa kwenye utegemezi, bali hivi ni vimisaada vya kimkakati tu, huku tukiendelea kuwa wategemezi kwa hao watu.
Na kwa bahati mbaya sana, hawa "wazungu wanaotupenda sana" kama ulivyosema wanaijua vizuri kabisa tabia yetu, hasa ya viongozi, kwamba hatuwezi kujiondoa katika hali ya utegemezi kwa hivi vimisaada tunavyotupia mara moja moja.

Ngoja nimalize na swali: Hivi watu wa Zimbabwe, ambao wamo kwenye vikwazo vya kudumu vya hawa wanaotupenda sisi, waafrika wenzetu hawa kosa lao la kudumu ni lipi hasa?

Mkuu "Erythro" nimejitahidi kukujibu wewe pamoja na huyu mkuu hapa 'Stonecutter', kwa sababu umetoa hoja inayovuruga akili za watu wengi kuhusu 'wapenzi' wetu hawa.

naomba unisome pia hapo juu, kuhusu sababu inayofanya tupendwe zaidi kwa sasa hivi kutokana na kazi kubwa tuliyofanya kujificha vichakani, katikati ya Jiji la New York, ili tusijitokeze kupiga kura yetu UN.
Fuatilia ripoti ya CAG
Hii mada yako hapa inakinzana sana na ripoti ya CAG. Kwa njia moja au nyingine, marafiki zetu hawa wazungu ndio wanufaika wakubwa wa hayo anayoripoti CAG, kwa sababu inawapa mwanya wa kuendelea kutusaidia sisi.

Naomba unisome hapo juu kuhusu kujificha kwetu kichakani ili tupate msaada huu tuliopata leo.

Usidhani ni utani, hiyo ndiyo hali halisi tulikofikia kama nchi chini ya uongozi wa Samia. Kaweka historia mpya.
 
Sidhani kama hizo hela zinatoka kwao za walipa Kodi wao,wanatulainisha tu ila watuibie vizuri........sisi Africa tumekosa viongozi tu .............wangekuwa na huruma wangewasaidia homeless huko kwao maana wapo kibao......
Tuna nini hasa cha kuibiwa,kitakachoifanya USA ishindwe kuishi?
Maskini mko na chuki sana&kwenu hakuna jema,wala shukrani.
 
Tuna nini hasa cha kuibiwa,kitakachoifanya USA ishindwe kuishi?
Maskini mko na chuki sana&kwenu hakuna jema,wala shukrani.
Ndugu yangu unajua tatizo linakuja, kwa watz kuwa bado wengi wao, huwa bado Wana 'hangover za mawazo ya kijamaa' na kushabikia umaskini jeuri' na umwamba usio na faida, kama ule wa Mugabe, hadi kusababisha total collapse ya uchumi na maisha ya watu wake..........kaazi kwelikweli.
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania, Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania.

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa, bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu.

Narudia tena, " Mungu Wabariki Wazungu"
Misaada haiji bure
 
Waarabu kazi yao ni valisha watu baragashia,kuwalisha mitende,huku wao wakibeba wanyama na mbuga zetu.
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania, Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania.

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa, bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu.

Narudia tena, " Mungu Wabariki Wazungu"
Marekani si nchi ya wazungu, hata huyo Makamu wa Rais si mzungu.
 
Hawa wajinga wameharibiwa na siasa za kitapeli za viongozi wetu kuwe nchi yetu ni tajiri sana. Eti wazungu wanaitamani nchi kutokana na mali tulizo nazo. Wakati uhalisia ni hakuna kitu.
Chama Cha mapinduzi kimetengeneza kizazi Cha wajinga kabisa!!
 
Kama kuna mtu huwa anakuelewa basi huyo mtu ni bonge la kiazi
Humuelewi kwa sababu wewe ni zaidi kiazi mbatata yaani unashindwa kujua nini mleta uzi amekusudia kuandika?

Bure kabisa wewe kilaza wa mwezi kwa jf.
 
Hehehe kama vipi na ww uwafuate uko uko unatawaliwa kifikra na wazungu halaf unawapigia promo. Kwanza wamewalainisha kwny ile list ya mziki aliotoa Spotify anaosikiliza uyo Us vice president wanajua fikra zenu hazipo sawa kama ww hapo🤔 😅😂
Hamuwapendi wazungu Ila mnapenda ARV zao!
 
Kama kuna mtu huwa anakuelewa basi huyo mtu ni bonge la kiazi
Yaani hiki![emoji23][emoji23][emoji23]
IMG-20191201-WA0063.jpg
 
Hivi tajiri anayewawezesha vijana wa mtaani kwake wasome na kupata kazi kila anapoona fursa ili wasimkabe kama panyaroad au kugeuza mtaa anaoishi kuwa wa mateja anakuwa amewapenda hao vijana au amejipenda yeye na familia yake?

Tajiri anayerekibisha barabara ya mtaani kwake bila kusubiria serikali ili aweze kupita vizuri na gari lake anakuwa amewapenda watu wa mtaani kwake na serikali yake au amejipenda wenyewe??

Nafikiri kuna wakati mwingine binadamu kwa kujipenda mwenyewe inapelekea kuusambaza huo upendo kwa wengine.
Hata kama ingekuwa ni halisia yenyewe, kwamba wanatoa hela hiyo, wananunua nini kwetu?

Tuna kitu gani cha thamani wanachokitafuta kwetu hadi watoe hiyo pesa? Hapo ndipo penye jibu.

Hiyo hela haitolewi bure, kwa kujifurahisha tu, au "kwa kutupenda" kama Erythrocyte anavyodai kwenye mada yake.

"Wazungu watupende"? Tumekuwa mabinti wanataka watuoe?

Inakuwa mbaya zaidi, hata tunaposhindwa kuitumia hiyo inayoitwa "misaada" isaidie nguvu zetu tuondokane na huu utegemezi wa kujiuzauza kila mara.
Miaka zaidi ya 60, bado tunalilia misaada?
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania, Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania.

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa, bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu.

Narudia tena, " Mungu Wabariki Wazungu"
Siyo kila msaada ni msaada! Yaani wewe mpaka nakua napata wasi wasi wa umri wako au aina ya maisha yako
 
Sidhani kama hizo hela zinatoka kwao za walipa Kodi wao,wanatulainisha tu ila watuibie vizuri........sisi Africa tumekosa viongozi tu .............wangekuwa na huruma wangewasaidia homeless huko kwao maana wapo kibao......
Homeless wa kule ni sawa na mwalimu wa huku
 
Tayari!

Naomba mleta mada akusome vizuri na akuelewe.

Ngoja na mimi nimfafanulie zaidi.

Katika historia ya nchi yetu, tokea tupate uhuru, hapo mwaka 1961, hatujawahi kumwogopa mtu yeyote katika kueleza msimamo wetu katika jambo lolote.

Ni hadi juzi juzi tu, mwezi mmoja au miwili, kwa mara ya kwanza kabisa Tanzania ililazimika kujificha vichakani mjini New York, ili isipige kura kwenye azimio la kuilaani Urusi. hata kule kujitokeza na kupiga kura ya kutofungamana, na upande wowote tukaona haitoshi, bali tujifiche kabisa tusijulikane tupo wapi.

Sasa hii ndiyo zawadi ya tendo letu hilo la kusikitisha sana kwa nchi yetu.

Watu ni lazima waelewe kwamba dunia inajitoa kwenye mtindo wa 'unipolar' unaoendeshwa na mbabe huyu anayetununua sasa hivi. Dunia inaingia kwenye 'multipolar'; lakini mkubwa bado anataka ashikilie unyampara kwa dunia, kwa hiyo viumbe hafifu kama sisi (soma viongozi wetu), ndio sasa wanajiingiza humo humo.
Hovyo Kabisa.
1. Dunia imebadilika sana tangu mwaka 1961. Hakuna tena USSR, Ujamaa ulishazikwa, ukoloni umeondoka duniani kote n.k haya ni baadhi ya machache tu. Kutaka sera yetu ya kimataifa ifanane na ya wakati huo ni kushindwa kwenda na wakati.

2.Kama ulitaka sana Tanzania kutoa msimamo wake kuhusu uvamizi huko Ukraine, msimamo sahihi ulikuwa ni kupinga uvamizi wa Taifa huru, hata kwa historia ya taifa lako unayoihusudu sana, tumekuwa tukipinga uvamizi kote duniani ikiwa ni pamoja na kupigana vita dhidi ya mvamizi.

3.Kuwa unipolar au multipolar na uvamizi ni kitu kingine kabisa, dunia inaweza kuwa multipolar bila uvamizi wa kimataifa. Pia dunia kuwa multipolar tu haimaanishi kwamba ukiwa dhaifu utaepuka kufanyika "koloni". Mwisho unaweza kukuta hata hiyo unipolar au multipolar ni maneno tu ya kisiasa, katika global order lazima atakuwepo tu mwenye ushawashi zaidi au labda hata sio kitu kipya sana na tulichoshuhudia kipindi cha vita baridi wakati kulikuwa na West na East blocks.
 
Back
Top Bottom