Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Emancipate Yourself from Mental Slavery....

Anyway kama unapenda kujisomea tafuta story au angalia hata movie au google kuhusu trojan horses....

At best watu wanatafuta quid pro qou lakini when push comes to shove ni numero uno...
Mental Slavery ni ngumu sana kuisha.
Kwa uthibitisho mdogo ni namna wale waliopewa nafasi serikalini kwa niaba yetu wanavyojipigia pesa hadi mama anatamani kulia. Kama pesa yote inyotolewa kwa ajili ya maendelea ingetumika hata kwa asilimia 75 misaada hii tusingeihitaji. Bado tuna akili za kitumwa tukiwa tumevaa suti.
 
Kwa Ile mihela ya jana no wonder wamachinga wa masoko yote ya mjini na wale wa vijijin waliitana wakakubaliana kila mtu apite mtaani kunadi bidhaa zake
Ili yule mgeni aje atoe hizo ela alafu watajua wanalindanaje
Soma tena ulichoandika
 
kitu usichokijua kwa mtazamo wako wa kawaida unaona hivyo kwa uhalisia hizo pesa wanakuja kuzirudisha kwa mtindo mwingine kwa mfano mdogo tu umesikia mama akilala mika kampuni inayotuuzia ndege ya mizigo boing imetuongezea pesa nyingi tofauti na makubaliano ya awali ,hiyo kampuni ya boing ni kampuni ya kimarekani na hizo pesa wakitupiga zinarudi marekani na wananufaika wamarekani zaidi achilia mbali makampuni ya madini ya kimarekani yaliopo nchini na yanayokuja yataendelea kutupiga laki na wanatupa 20 elfu kama masaada .tustuke
Jiwe lazima alaaniwe kwa kutuingiza kwenye hasara kubwa kwenye biashara ya ndege na bwawa la umeme na sgr
 
Hapana.sikukubaliana na maoni yako huko juu na unavyotaka kulazimisha mambo sasa. Nilihisi una hoja dhaifu kwanini nikuelewe unaposema mungu awabariki una maanisha nini.

Na kwahayo majibu yako naamini huna sababu halali za kunilazimisha kufanya nikuelewe ikiwa na pamoja na kunitaka sasa kuomba kwa kutumia alama au ishara ya msalaba kwa sababu hukufurahishwa na majibu niliyotoa. Umetoa wapi nyodo hiyo?

Kwanza kuna ukinzani na haki za za wazungu, "haki ya msingi ambayo kila mtu yuko huru kutafuta na kupokea taarifa kutoka kwa maoni yote bila kizuizi" Unachovimba ni nini?

Usinilazimishe kunyenyekea na kuwapigia mabusu miguu wazungu


Nyie CHADEMA ndio mpumzike na amani, kwani mkileta za kuleta tuwawafirigisa hakuna mfano, hatutaki mtulazimishe na siasa za mlengo wa kulia wa wahafidhina wa kizungu.

Nenda umpigie ishara hiyo ubeligiji wanahitaji zaidi uwaambie wapumzike kwa amani. Wazungu wanahitaji hilo kwa laan waliyokuwa nayo.

BTW situmii ishara hiyo. Usinilazimishe.
Chadema haihusiki na ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani
 
Sasa hebu kila Mwanajf aainishe mwenyewe vitita vya pesa ambavyo Makamu wa Rais wa Marekani ameahidi Nchi yake itaichangia Tanzania, Sasa jioneeni wenyewe huruma waliyonayo Wazungu kwenu Watanzania.

Pamoja na kwamba wanatambua kuwa baadhi ya viongozi wenu waliokosa maono wanawaita Mabeberu lakini hawajawakatia tamaa, bado wanaendelea kuwasaidieni kiroho safi kabisa , tena wala hawakusema hatuwapi hela kwa vile Ripoti ya CAG imedai kwamba tuna viongozi wezi , wametoa tu kiroho safi kabisa , kazi ibaki kwenu wenyewe na wizi wenu.

Narudia tena, " Mungu Wabariki Wazungu"
No free lunch wakupe wewe Nani upewe bure

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Umejitutumua sana hapa.

Hoja yako inahitaji jibu, sijui nani atajibu ili umuelewe vizuri.
Mimi shaweka mabandiko yangu hapa mfululizo, sasa sijui kama itasaidia chochote kuongeza bandiko lingine.

Ngoja nitumie mfano mfupi: Unajua hadi sasa hivi kiasi cha pesa alichotoa rafiki yetu huyu kwa nchi ya Ukraine? Zaidi ya bilioni 30 ya pesa yake, na bado anaendelea kutoa misaada.

Basi tuseme anawapenda zaidi watu wa huko kuliko waTanzania ambao manusra wafe kwa njaa wakati ule alipotoa msaada, na karibu kila mwaka anatoa vimisaada! Kama bado hujaona maana ya swali langu, sina njia nyingine ya kukufafanulia zaidi ila kusema ni "maslahi" tu.

Ni hivi: hapa hupewi msaada utakaokuwezesha kujiondoa kwenye utegemezi, bali hivi ni vimisaada vya kimkakati tu, huku tukiendelea kuwa wategemezi kwa hao watu.
Na kwa bahati mbaya sana, hawa "wazungu wanaotupenda sana" kama ulivyosema wanaijua vizuri kabisa tabia yetu, hasa ya viongozi, kwamba hatuwezi kujiondoa katika hali ya utegemezi kwa hivi vimisaada tunavyotupia mara moja moja.

Ngoja nimalize na swali: Hivi watu wa Zimbabwe, ambao wamo kwenye vikwazo vya kudumu vya hawa wanaotupenda sisi, waafrika wenzetu hawa kosa lao la kudumu ni lipi hasa?

Mkuu "Erythro" nimejitahidi kukujibu wewe pamoja na huyu mkuu hapa 'Stonecutter', kwa sababu umetoa hoja inayovuruga akili za watu wengi kuhusu 'wapenzi' wetu hawa.

naomba unisome pia hapo juu, kuhusu sababu inayofanya tupendwe zaidi kwa sasa hivi kutokana na kazi kubwa tuliyofanya kujificha vichakani, katikati ya Jiji la New York, ili tusijitokeze kupiga kura yetu UN.

Hii mada yako hapa inakinzana sana na ripoti ya CAG. Kwa njia moja au nyingine, marafiki zetu hawa wazungu ndio wanufaika wakubwa wa hayo anayoripoti CAG, kwa sababu inawapa mwanya wa kuendelea kutusaidia sisi.

Naomba unisome hapo juu kuhusu kujificha kwetu kichakani ili tupate msaada huu tuliopata leo.

Usidhani ni utani, hiyo ndiyo hali halisi tulikofikia kama nchi chini ya uongozi wa Samia. Kaweka historia mpya.
Ngoja kwanza , hapa sijakuelewa , nimeweka ya CAG ili kuonyesha uvumilivu wa Wazungu kwa uchafu wetu , yaani pamoja na kwamba ndani yetu wamo panya buku lakini wao hawachoki kutupa chakula .
 
Hivi tajiri anayewawezesha vijana wa mtaani kwake wasome na kupata kazi kila anapoona fursa ili wasimkabe kama panyaroad au kugeuza mtaa anaoishi kuwa wa mateja anakuwa amewapenda hao vijana au amejipenda yeye na familia yake?

Tajiri anayerekibisha barabara ya mtaani kwake bila kusubiria serikali ili aweze kupita vizuri na gari lake anakuwa amewapenda watu wa mtaani kwake na serikali yake au amejipenda wenyewe??

Nafikiri kuna wakati mwingine binadamu kwa kujipenda mwenyewe inapelekea kuusambaza huo upendo kwa wengine.
Dah!

Mkuu 'Yoda', nilijua utakuja tu. Mimi nilijizuia mara ya kwanza nilipoona mchango wako wa mwanzo kabisa katika mada hii kuku'quote'. Sasa tupo hapa pamoja.

Hiyo mifano uliyotoa hapo juu ni mizuri sana, ila hitimisho lake haliko sawa.

Hao matajiri "wanajipenda", lakini siyo sahihi kusema kwa vitendo vyao hivyo "wanasambaza upendo wao kwa jamii."

Ngoja hili niliachie hapa.
 
1. Dunia imebadilika sana tangu mwaka 1961. Hakuna tena USSR, Ujamaa ulishazikwa, ukoloni umeondoka duniani kote n.k haya ni baadhi ya machache tu. Kutaka sera yetu ya kimataifa ifanane na ya wakati huo ni kushindwa kwenda na wakati.

2.Kama ulitaka sana Tanzania kutoa msimamo wake kuhusu uvamizi huko Ukraine, msimamo sahihi ulikuwa ni kupinga uvamizi wa Taifa huru, hata kwa historia ya taifa lako unayoihusudu sana, tumekuwa tukipinga uvamizi kote duniani ikiwa ni pamoja na kupigana vita dhidi ya mvamizi.

3.Kuwa unipolar au multipolar na uvamizi ni kitu kingine kabisa, dunia inaweza kuwa multipolar bila uvamizi wa kimataifa. Pia dunia kuwa multipolar tu haimaanishi kwamba ukiwa dhaifu utaepuka kufanyika "koloni". Mwisho unaweza kukuta hata hiyo unipolar au multipolar ni maneno tu ya kisiasa, katika global order lazima atakuwepo tu mwenye ushawashi zaidi au labda hata sio kitu kipya sana na tulichoshuhudia kipindi cha vita baridi wakati kulikuwa na West na East blocks.
Hakuna hata moja la msingi hapa
1. Sijasema katika andiko lile kwamba yaliyokuwepo 1961 ndiyo tunatakiwa kubaki nayo sisi, tusibadilike kama dunia inavyobadilika. Kubadilika hakuna maana ya kujikabidhi kwa yeyote duniani akuendeshee maisha yako

2. Nilitaka Tanzania isijifiche vichakani kwa kuogopa kuwaudhi hao wanaotununua sasa hivi. Sisi ni taifa na tunao uamzi tunaoona unafaa kutokana na tunachoona kinafaa kwa msimamo wa nchi yetu, siyo kwa mshinikizo wa mataifa mengine.
Hilo swala la uvamizi ni mjadala mwingine ambao pia sikubaliani nawe; wewe unauita uvamizi, mimi ninautambua kama kujihami kwa wanaopigiwa hesabu kwa usalama wao.
Upofu wa akili unaanzia hapo, na kushindwa kujua kuwa dunia inabadilika, siyo kama unavyodhani wewe.

3. Kama unafikiri "Cold War" ilikwisha na sasa tujikabidhi kwa hao wanaojiona wana haki ya kuitawala dunia tena kwa misingi yao, utashangaa sana kama huoni kwamba vita mpya imezuka tena. Bado hutambui kwamba kelele zote hizi za kutuweka mifukoni mwa hao wakubwa ni sehemu ya vita hiyo?

Kwa taarifa yako: Ujamaa haukushindwa, upo leo na utakuwepo siku zote, kote duniani.
 
Hapo ulipo malizia, tupo pamoja. Hivyo tuendelee kuwashukuru wazungu, maana hatuna namna.
EeeenHeeeee!
Kuwashukuru wazungu ni hapo tutakapojitambua sisi wenyewe kuwa nasi ni binaadam wenye akili na utashi, na tunaweza kabisa kuishi maisha yetu bila ya kujiuza ili tupendwe.

Tuchukue hiyo misaada inayotolewa, iwe ni kwa kupendwa au vipi, lakini tuwe na akili ya kuitumia hiyo misaada kujijengea heshima yetu wenyewe.
 
EeeenHeeeee!
Kuwashukuru wazungu ni hapo tutakapojitambua sisi wenyewe kuwa nasi ni binaadam wenye akili na utashi, na tunaweza kabisa kuishi maisha yetu bila ya kujiuza ili tupendwe.

Tuchukue hiyo misaada inayotolewa, iwe ni kwa kupendwa au vipi, lakini tuwe na akili ya kuitumia hiyo misaada kujijengea heshima yetu wenyewe.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom