Tetesi: Tunashukuru kwa Serikali kumalizana kabisa na Mkulima wa ndege

Zimeshakamatwa na kuachiwa Mara ya ngapi hadi sasa na hamna kithibitisho mara zote hizo, makondoo mshafeli sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiona kitu kimekamatwa kwa kudaiwa kisha kikaachiwa pigia jibu mstari. Usingoje ushahidi kwa hao wasaka sifa maana wao kulipa baada ya kufanya ubabe wa kishamba ni aibu, hivyo lazima wapige kimya, habari ndio hiyo. Kama ww unaongoja ushahidi kwa hao wasaka sifa utasubiri sana. Hilo la kwamba sisi ni makondoo hasa nyie mashahidi wa mungu wa Tanzania halihitaji mjadala wa kitaifa.
 
U
Chakaza we mzee sasa, hizi lugha za UKATIWE waachie hawa wadogo zetu humu JF.
Umenisoma tofauti kabisa! Kwani we umeelewaje mzee mwenzangu? Mbona Tanesco kuna wakati walikuwa na tangazo hilo redioni likisisitiza kulipa malimbikizo ya madeni ya umeme (kabla ya LUKU) nakusema "ndugu mteja, kwa nini hulipi madeni yako ya Ankara za umeme mpaka ukatiwe?" Na sikusikia malalamiko hadi Leo hii ndio nakusikia mzee mwenzangu Phillipo?
 
Nchi ina pesa nyingi sana, hii nchi sio masikini

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini watu wake ni masikini na ambao wanakula mlo mmoja kwa siku. Forget about maisha ya mjini ambayo angalau tunabangaiza, think about wale wa kijijjini ambao hawana maji ya bomba, umeme, huduma za afya kilometa kadha(mbali), shule kilometa kadhaa na pengine ina mwalimu mmoja nk
 
Kama gharama au bei ya kilo ya nyama ya mbuzi kule ni sawa na nusu nauli ya mtu why tusizitumie vyema ndege hizi?? Mwanzoni mtashangaa lakini zikianza kurudi na watalii ndo mtaelewa nia nzuri ya serekali
Ndege ziwe zinapeleka mbuzi Dubai halafu zirudi na watalii ambao wakimaliza shughuli zao hapa warudi kwao na mbuzi wengine eti ndo biashara! Kweli ukiwa CCM unakuwa huna akili na unakuwa huna akili zaidi ukiwa pia Msukuma. Kwa kuwa wsmezoea kusafiri kwenye mabasi ya Musukuma pamoja na mbuzi, wanapanga kuunganisha safari na watalii ili ndege zijae zilete faida.
 
Tumsifu rais John p Magufuli kwa kitendo chake cha kiungwa
 
Alikuwa akilipwa kidogo kidogo mpaka huyu akaja kusitisha ghafla wakati akijua ni haki yake. Sio wote wajinga humu
 
Huo ndio ukweli,bora imekuwa hivyo kwani ndio dawa ya deni.
Ila fedha zimetoka wapi? zimetoka account ipi? mbona kuna usiri?
 
Halina mjadala pasipo kithibitisho? Au ni sababu ndio habari unayoipenda, as if ni makosa ya magu kumdhulumu huyo mzungu, haters mbona mtateseka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, usipate hasira bure. Magu ndialiyetufikisha hapa kwa sababu ni yeye aliyezuia malipo kidogo kidogo yaliyokuwa yakifanywa na watangulizi wake. Kama hata fact hii unaikataa - unakosa haki ya kujadili vitu objectively and factually. Kwa maelezo ya wakubwa ni kuwa hata balozi wa Canada aliitwa (ilikuwa ni diplomatic mistake). Wenzetu wanaheshimu mahakama - balozi au Canada wasingeweza kutia ushawishi mahakamani. Kama serikali ilituma "timu" kwenda kuokoa ndege, angalau basi iseme "timu" ilifanikiwa. Huwezi kuomba uthibitisho kutoka kwa mtu binafsi. Kama raia unaweza kuomba uthibitisho kutoka kwa serikali. Play your part!!
 
angekua mkulima mswahili keshazurumiwa, mkulima mzungu sio mchezo
 
What's is your suggestion? Badala ya kulaumu waliolipa kidogo kidogo miaka yote hiyo, unamulaumu aliyelipa na kuachana naye. Imefikia hatua tunapakuwa hasira zitokanazo na matatizo mengine tunaziweka kwa lolote lililoko mbele yetu. Hakuna uhusiano wowote wa kulipwa kwa miaka yote ya nyuma awamu 4 halafu iwe vibaya kulipwa deni lote. Halafu sasa liwe jambo la kuzomea!

Mbona makosa ya tawala za nyuma hapa munafumba macho na kujifanya hamjui? Tulikuwa na rais aliyeshindwa hata kujua kwamba katiba haipatikani kwa mijadala ya matusi bungeni! Mabilioni yakaliwa bureee!
 

Umechanganya mambo mengi kwa wakati mmoja.ushauri wangu ni kuwa dawa ya deni ni kulipa. Sina tatizo na aliyelipa kidogo kidogo bali nina tatizo na anayegoma kulipa kibabe kisa ana madaraka. Kwa taarifa yako hajalipa moja kwa moja ili aachane na hilo jambo kwa kupenda, bali amebanwa kwenye kona ambayo mamlaka yake anayotumia vibaya hayawezi kufika, laiti mamlaka yake yangefika huko asingelipa.

Tafuta popote ninapofumbia macho tawala zilizopita kwenye makosa eti kisa sikubaliani na jiwe. Kwangu JK alikuwa rais dhaifu na hilo halitatobadilika, na kitendo cha katiba kuharibiwa ni kutokana na udhaifu wake wa kuendekeza siasa za vyama kwenye jambo lile.
 
Eti pigia mstari, we jamaa bhana,[emoji16].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa watu wanajaribu kutumia kukisia na hisia kujua kilichotokea. Tunachojua ni kuwa ndege imeachiliwa; kama amelipwa hatujui kama amelipwa deni lote au walikubaliana "settlement" au kuna mtu wa tatu ambaye ameingilia kati na kuhakikisha deni limelipwa au ndege kuachiliwa wakati mipango ya malipo iendelee kulipwa (katika installment). Kwa vile hatujui kwa uhakika tuendelee kupigishana stori.
 
Hofu yangu ya kwanza ni kuwa bado hukumu nyingine nyingi tu zipo njiani. Akimaizana na huyu ataibuka mwingine.

Hofu yangu ya pili ni kuwa bado sisi kama taifa na serikali hatujajifunza chochote kwenye hii tafrani. Bado wanasiasa wamekalia kutufanganya kuwa kuna matapeli na mabeberu wanaotuhujumu badala ya kutueleza kweli.

Kadri tutakavyoendekeza ulaghai na uongo dozi za hukumu kama hizi zitaendelea kututafuna mpaka tutakaposalimu amri kwa huyu kiumbe anayeitwa RULE OF LAW.
 
We zarau tu ila yakianza kunoga utakuja ukichekelea
 
Hahaha, dah unajua kutunga story, watanzania ni noma,. Umeona hamna majibu ya serikali umeona uje kivyako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…