Tunasimama na Lissu, alipo tupo

Tunasimama na Lissu, alipo tupo

Katiba mpya italeta zaidi ya Ugali mezani amesikika Tundu Lissu leo Runzewe.
 
Naona Chadema kwa sasa sio tena sehemu sahihi kwake, kwani kuendelea kubaki Chadema na kuvunja taratibu kwa kusema mambo kinyume na msimamo wa chama, hata kama yanapendwa kusikiwa na wengi, ni mkaidi, anayestahili adhabu, bitter truth.
Mkuu denooJ Kwanza tambua fika Yale hayakuwa maridhiano ..

Hakuna maridhiano yanayofanywa kwa uficho Kati ya wenyeviti wawili ,Lisu alishaona kilichofanywa ni kukata kiu ya watu binafsi ndio maana Lisu humuoni akiunga mkono popote .

Muda utasema Tu stay tuned
 
Sidhani kama Chadema bado wana huo msimamo wa bila Katiba Mpya hakuna uchaguzi mkuu, wanavyoonekana kwa sasa majority wanaviwaza viti vya ubunge zaidi ya chochote kingine.

Hii ndio sababu iliyomsukuma Lissu kuwakumbusha wenzie bila KM hakuna uchaguzi mkuu, bahati mbaya kwangu ameenda kuwakumbushia kwenye jukwaa tofauti, sijui ni kitu gani kilichomfanya asiwatazame usoni awaambie straight wakiwa vikaoni.

Hapa ni either Lissu ameshakata tamaa amewaona wenzake ni watu wasio tayari kubadilika, kama hajawaambia basi ameamua kujikweza na kujiweka juu ya wenzie, au vyovyote vingine.

Muhimu kwa sasa kama Chadema bado wapo kwenye maridhiano, huku Lissu hayataki, na ikiwa ameshindwa kuvumilia au kuwaambia wenzake vikaoni, na kukaa kimya hawezi..

Naona Chadema kwa sasa sio tena sehemu sahihi kwake, kwani kuendelea kubaki Chadema na kuvunja taratibu kwa kusema mambo kinyume na msimamo wa chama, hata kama yanapendwa kusikiwa na wengi, ni mkaidi, anayestahili adhabu, bitter truth.
Huenda keshawaambia sana wenzie vikaoni kuwa ubunge na udiwani bila katiba mpya unanufaisha zaidi watu binafsi kuliko Chama na Taifa kiujumla.

Kwa sasa anachokiongea Lissu ni msiamamo rasmi wa kamati kuu ya chama ambao haujabadilishwa na kikao kingine cha kamati kuwa BILA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI CHAMA HAKITASHIRIKI UCHAGUZI WA 2025.

Sasa hao wengine wanotaka ubunge na udiwani ndo wana jukumu la kuwaambia watu, kwa nini badala ya kutangaza kushiriki uchaguzi wa 2025, kwa nini meseji yao kuu isiwe kusimamia maamuzi ya kamati kuu ya kutoshiriki uchaguzi huo mpaka katiba mpya ipatikane?
 
Baada Chacha Wangwe,Zito na Slaa inaweza kuwa zamu ya Lisu kuwa "msaliti" ndani ya Chama.
.
20230510_085215.jpg
 
Mkuu denooJ Kwanza tambua fika Yale hayakuwa maridhiano ..

Hakuna maridhiano yanayofanywa kwa uficho Kati ya wenyeviti wawili ,Lisu alishaona kilichofanywa ni kukata kiu ya watu binafsi ndio maana Lisu humuoni akiunga mkono popote .

Muda utasema Tu stay tuned

Kama mnauachia muda kwanini mnayalaumu maridhiano?

Tukubaliane, kama muda unaachiwa ili kujaribu kuonesha Lissu yupo sahihi, basi na muda huo huo yaachiwe maridhiano ili tuone mwisho wake utakuwa vipi.

Tusijichagulie wapi pa kuupa muda nafasi, hili ni vyema na Lissu alijue.
 
Huenda keshawaambia sana wenzie vikaoni kuwa ubunge na udiwani bila katiba mpya unanufaisha zaidi watu binafsi kuliko Chama na Taifa kiujumla.

Kwa sasa anachokiongea Lissu ni msiamamo rasmi wa kamati kuu ya chama ambao haujabadilishwa na kikao kingine cha kamati kuwa BILA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI CHAMA HAKITASHIRIKI UCHAGUZI WA 2025.

Sasa hao wengine wanotaka ubunge na udiwani ndo wana jukumu la kuwaambia watu, kwa nini badala ya kutangaza kushiriki uchaguzi wa 2025, kwa nini meseji yao kuu isiwe kusimamia maamuzi ya kamati kuu ya kutoshiriki uchaguzi huo mpaka katiba mpya ipatikane?
- Ukisema huenda keshawaambia wenzie ndani ya chama hapo unaonesha hauna hakika na ulichoandika, na kama uhakika haupo, basi tukubaliane lawama asitupiwe yeyote.

- Anachokiongea Lissu kuhusu KM sina tatizo nacho, tatizo langu kwake ni yeye kuyapinga maridhiano ambayo chama chake bado kinashiriki, hiyo inaonesha huyu jamaa hayupo pamoja na wenzake.

- Kwanini unawataka hao wengine wakawaambie watu badala ya kwenda kusema hoja zao mbele ya Kamati Kuu? hii biashara itazidi kukivuruga chama, inaonesha vile hawa viongozi wa Chadema wameshindwana kwenye vikao, nataka warudi vikaoni wakazungumze "concern" zao huko, wakitoka wawe kitu kimoja, sio kila mtu na lake kama watoto wadogo.

• Tumeshaona baadhi ya harakati toka upande wa CCM, hasa serikali kuhusu Katiba Mpya, juzi wamesema wataanza mchakato, inawezekana hii pia ndio sababu inayowafanya hao jamaa waanze kelele za kuutaka ubunge, hii ni tofauti kabisa na msimamo wa Lissu asiyetaka maridhiano yanayoleta yote haya.
 
- Ukisema huenda keshawaambia wenzie ndani ya chama hapo unaonesha hauna hakika na ulichoandika, na kama uhakika haupo basi tukubaliane lawama asitupiwe yeyote.

- Anachokiongea Lissu kuhusu KM sina tatizo nacho, tatizo langu kwake ni yeye kuyapinga maridhiano ambayo chama chake bado kinashiriki, hiyo inaonesha huyu jamaa hayupo pamoja na wenzake.

- Kwanini unawataka hao wengine wakawaambie watu badala ya kwenda kusema hoja zao mbele ya Kamati Kuu? hii biashara itazidi kukivuruga chama, inaonesha vile hawa viongozi wa Chadema wameshindwana kwenye vikao, nataka warudi vikaoni wakazungumze concern zao huko, wakitoka wawe kitu kimoja, sio kila mtu na lake kama watoto wadogo.
Lissu anaunga mkono maridhiano ya kweli haungi mkono "ushosti na danganya toto" katika maridhiano.

Hakuna mahali Lissu amewahi kutamka wazi kuwa hataki maridhiano, infact yeye ndo huwa anayatetea sana kila apatapo nafasi kuyazungumzia.

Ila Lissu ni mtu mwenye ufahamu, anapoiona danganya toto ya CCM huku ikijificha kwenye neno maridhiano anaitamka wazi.

Tena nikwambie, anachokifanya Lissu kinamsaidia Mbowe na timu yake ktk maridhiano kuwakabili vizuri CCM, maana pengine Mbowe hawezi kuja kuipiga spana CCM waziwazi kutokana na nature ya kazi yake, ila hiyo kazi inafanywa vizuri na Lissu.

Bila kuwasagia kunguni CCM na Samia kwa wananchi watatupiga danadana sana kwenye hii ishu ya katiba mpya
 
Back
Top Bottom