Tunasimama na Lissu, alipo tupo

Tunasimama na Lissu, alipo tupo

Amekuwa wazi mwana halisi wa nchi hii, Rais wa mioyo ya wengi - Tundu Antipas Lissu:

Lissu: Maridhiano pekee ni Katiba

Hizi ndiyo kauli za watu sasa tulizokuwa tumezikosa mno.

Tumesema sana na tuko tayari.

Nisiwachoshe na wala tusichoshane:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Kwamba:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Tundu Antipas Lissu, ulipo tupo:

1. Uchaguzi huru, wazi na haki ndani ya CDM ndiyo njia ya kwenda.
2. Kama #1 hapo juu haiwezekani hata FORD ilizaa FORD Kenya na Ford Asili. Jahazi likasonga.

Aluta Continua!
Komaeni sana maana DJ kazima mziki nasi tuko pamoja nanyi CDM asilia sio hii ya akina Sugu
 
Komaeni sana maana DJ kazima mziki nasi tuko pamoja nanyi CDM asilia sio hii ya akina Sugu
Lisu kutakuwa na mchezo kaushtukia. Huyu mangi kwenye mambo yanayohusiana na pesa sio kabisa.😆😆
 
Lissu anaunga mkono maridhiano ya kweli haungi mkono "ushosti na danganya toto" katika maridhiano.

Hakuna mahali Lissu amewahi kutamka wazi kuwa hataki maridhiano, infact yeye ndo huwa anayatetea sana kila apatapo nafasi kuyazungumzia.

Ila Lissu ni mtu mwenye ufahamu, anapoiona danganya toto ya CCM huku ikijificha kwenye neno maridhiano anaitamka wazi.

Tena nikwambie, anachokifanya Lissu kinamsaidia Mbowe na timu yake ktk maridhiano kuwakabili vizuri CCM, maana pengine Mbowe hawezi kuja kuipiga spana CCM waziwazi kutokana na nature ya kazi yake, ila hiyo kazi inafanywa vizuri na Lissu.

Bila kuwasagia kunguni CCM na Samia kwa wananchi watatupiga danadana sana kwenye hii ishu ya katiba mpya
Tatizo mnampenda sana Lissu mpaka mnaanza kumrekebishia makosa yake.

Hiyo paragraph yako ya pili umeandika kinyume kabisa na msimamo wa Lissu, mtu anayepinga mambo mengi kwenye maridhiano iweje ayatake?!
 
Amekuwa wazi mwana halisi wa nchi hii, Rais wa mioyo ya wengi - Tundu Antipas Lissu:

Lissu: Maridhiano pekee ni Katiba

Hizi ndiyo kauli za watu sasa tulizokuwa tumezikosa mno.

Tumesema sana na tuko tayari.

Nisiwachoshe na wala tusichoshane:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Kwamba:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Tundu Antipas Lissu, ulipo tupo:

1. Uchaguzi huru, wazi na haki ndani ya CDM ndiyo njia ya kwenda.
2. Kama #1 hapo juu haiwezekani hata FORD ilizaa FORD Kenya na Ford Asili. Jahazi likasonga.

Aluta Continua!

Ninasimama na Lissi
 
Tatizo mnampenda sana Lissu mpaka mnaanza kumrekebishia makosa yake.

Hiyo paragraph yako ya pili umeandika kinyume kabisa na msimamo wa Lissu, mtu anayepinga mambo mengi kwenye maridhiano iweje ayatake?!

Mkuu Lissu hapendwi kwa uzuri wa uso wake. Lissu anapendwa kwa ubora, mashiko, uthabiti, dhamira nk ya hoja zake. Huyu ndiyo wale viongozi ambao wakituita tutamwagika barabarani.

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Lissu anabeba uelekeo tunaoutaka. Kama Lissu angeyapinga haya:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Tungemvaa kama yeyote ayapingaye.

Kama johnthebaptist, Pascal Mayalla , Tulia, Kibajaji, Nape, Wassira, Samia au hata shetani wakiliunga mkono hili la katiba mpya kabla ya uchaguzi tutawaunga na kumpinga Lissu kama atachagua kulipinga.

Kwani mnatuona je?

Habari ndiyo hiyo.
 
Zawadini ng'ambo za kule Zenji bar, denooJ pande za bara kule tuwaandae watu. Gari Moshi ndilo hilo ling'oa nanga.

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine

Mawili hayo yanakwenda pamoja.

Tutaelewana tu.
Asante Mkuu. Hili la katiba nasikiasikia eti lina mwelekeo ila hofu na wasiwasi wangu ni kuipata ile tuitakayo. Nadhani bado una kumbukumbu ya yaliyotokea kwa ile ya Warioba. Mimi bado ninayo nakala yake hivyo nasubiri ili nilinganishe.

Hili la CHADEMA, nina hamu ya kuiona hii na wala si nyingine ili tuelewane. Kinachonitia wasiwasi ni uwezo wa kuhimili vishindo vya nje na ndani ili kufikia hilo lengo. Bado nakumbuka namna ilivyopata mitihani kutokanje, na huenda hiyo mitihani ilisababishwa na ushawishi/vishindo vya nje. Tujitayarishe ktk hili.
 
Arudi makao makuu ya chama kwanza akapate dondoo za Nini akiongee na nn Ni mkakati wa chama chake. Anatupotosha sana
 
Asante Mkuu. Hili la katiba nasikiasikia eti lina mwelekeo ila hofu na wasiwasi wangu ni kuipata ile tuitakayo. Nadhani bado una kumbukumbu ya yaliyotokea kwa ile ya Warioba. Mimi bado ninayo nakala yake hivyo nasubiri ili nilinganishe.

Hili la CHADEMA, nina hamu ya kuiona hii na wala si nyingine ili tuelewane. Kinachonitia wasiwasi ni uwezo wa kuhimili vishindo vya nje na ndani ili kufikia hilo lengo. Bado nakumbuka namna ilivyopata mitihani kutokanje, na huenda hiyo mitihani ilisababishwa na ushawishi/vishindo vya nje. Tujitayarishe ktk hili.

Kabeni Zenji bar tunakaba bara. Agenda yetu moja katiba mpya kwanza. Chadema yenye katiba mpya kama kipaumbele ndiyo tunayoitambua. Siyo nyingine:

Tuna Imani na CHADEMA hii, wala si nyingine
 
Back
Top Bottom