A
Anonymous
Guest
Kuna ugumu wa kupata Visa ya kwenda China kutoka hapa nchini, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa waombaji wengi.
Tunalazimika kuamka saa tisa usiku ili kuwahi foleni, lakini hata hivyo hatufanikiwi kupata huduma tunazotarajia, baadhi ya waombaji tumeomba kwa siku ya tatu mfululizo bila mafanikio yoyote, wao wanaishia kuhudumia takribani watu 20 pekee.
Hali hii inasababisha wengi kurudi bila kuhudumiwa licha ya kutumia muda mwingi na gharama kufika eneo la maombi.
Pia soma ~ Wizara: Ubalozi wa China umesema hakuna vikwazo vya kisera kwa Watanzania wanaoomba visa za China