Tunasubiri kuona Rais Samia atafanya nini kwenye sakata la Bandari

Tunasubiri kuona Rais Samia atafanya nini kwenye sakata la Bandari

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,994
Reaction score
24,902
Suala la mkataba wa kubinafsishwa kwa bandari za Tanzania limekuwa gumzo kubwa la kisiasa kuwahi kutokea hapa nchini. Sakata hili limewaamsha watanzania wengi kuhusu mikataba ambayo viongozi wetu huingia kwa niaba ya Taifa zima na umuhimu wa kuwa na viongozi wazalendo wenye kusimamia maslahi ya Taifa na sio maslahi yao wenyewe.

Ukimya wa baadhi ya viongozi wa kitaifa kuhusu sakata hili, na hasa ukimya wa rais Samia vimeonesha kuwa suala la bandari limewagusa na pengine kuibua hisia tofauti. Kuna waliokaa kimya kuogopa kukinzana na wakubwa wao, na kuna waliokaa kimya kwa kutokuwa na uhakika wa kipi ni sahihi na kipi sio sahihi.

Iwe iwavyo watanzania wanasubiri kuona Rais Samia atafanya maamuzi gani kuhusu suala la bandari baada ya wananchi wa kada mbalimbali kutoa maoni yao. Je, atafumbia macho maoni ya mamilioni ya watanzania wakiwemo wanazuoni, wajuvi na wasomi? Lolote atakaloamua kufanya Rais, ni muhimu na litamweka pahala flani katika historia ya nchi hii.

Tunajua upo ugumu wa Rais kusitisha mkataba huu ambao tayari hatua zake za awali zimeshasainiwa. Binafsi naona kuna umuhimu wa kuwa na uwazi zaidi katika suala hili. Itambidi rais kujitokeza na kuzungumza waziwazi msimamo wake. Palipo na makosa itakuwa busara kwa Rais kuruhusu marekebisho yafanyike kuepuka lawama siku zijazo. Watanzania tunahitaji maelezo mazuri na uzalendo wa juu kwenye hili jambo la sivyo suala la bandari laweza kuleta uharibifu mkubwa kwa uhuru wa nchi yetu na kutupeleka kwenye ukoloni wa kisekta ndani ya ukoloni mamboleo.
 
Hamna issue kubwa hapo watu wanaongea hivo kwasbb Raisi samia amewapa uhuru wa kuongea chochote wana chotaka, wengi wamamdhihaki wengine kumtolea matusi ubaguzi nk.

Hatukuona mkataba wa bomba la mafuta unajadiliwa na wananchi na wengi hakujua terms za ule mkataba, kwa yoyote anae jua watanzania walivyo na hili litapita hata bila mabadiliko yoyote na tutadandia jipya sema tu hili limepewa hamasa kubwa na viongozi wa kanisa ya RC
 
Back
Top Bottom