Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Wilaya ya Mvomero ni Wilaya yenye mito mingi sana.Hata hivyo Wilaya hii bado imeendelea kuwa na changamoto kubwa ya maji.Wananchi waliio wengi bado wanatumia visima vya wazi na mabwawa ambayo si salama kwa Afya zao,kwa kuwa mara nyingi wanachangia na mifugo.Maji haya kwa hiyo si salama na ni hatari sana kwa maisha yao. Kimsingi imekuwa kawaida sasa wananchi wa Mvomero kukumbwa na magonjwa kama kichocho na magonjwa ya matumbo kama vile Cholera,Typhoid,Amoeba,Dysentry nk.
Hata hivyo haionekani kama changamoto ya maji Wilaya ya Mvomero ipo karibu kutatuliwa wakati wowote karibuni,kwa kuwa tatizo bado ni kubwa sana,ingawa zipo juhudi za serikali zinazoendelea.
Nimeleta mada hii ili kama kuna mtu yeyote ambaye anajua shirika lolote mbalo linaweza kutoa msaada wa visima vifupi kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero au hata virefu tuwasiliane,ili tuweze angalau kupunguza tatizo hili ambalo ni kubwa sana. Inauma kuona wananchi wakichangia maji na mifugo.Naomba ujisikie huru kuni-inbox, ili tuone jinsi ya kuwasaidia wananchi wa Mvomero katika suala hili.