Tunatafuta sababu za kuinvoke Martial Law, serikali ikobize na Kuwepo kwa "Foreign Element"

Tunatafuta sababu za kuinvoke Martial Law, serikali ikobize na Kuwepo kwa "Foreign Element"

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Ghafla tumeanza kusikia Yada Yada za maneno mapya kwenye vyombo vya habari na mitandaoni, Eti "Kuna foreign Element" zinataka kuleta machafuko," "Watu waliovuruga OKtba29 si Watanzania," "Tutafanya demokrasia yetu bila shinikizo la mtu yeyote," "Kuna waasi wa M23 wanaandaliwa kuvuka mpaka," na habari ya hivi karibuni kwamba "Askari wa Kimarekani mwenye asili ya Kenya amekamatwa mpakani na mabomu manne ya M68."

Swali la kila mtu mwenye akili timamu ni hili: Kwa nini maneno haya yanatoka sasa hivi, wiki chache kabla ya maadhimisho ya D9 , siku ambayo Wananchi wametangaza kuwa kuna maandamano makubwa ya kitaifa? Hii si mara ya kwanza katika historia ya kisiasa ambapo serikali hutumia "tishio la nje" kama kisingizio cha kushikilia madaraka, lakini wakati huu, inaonekana kama huu umekuwa mkakati wa moja kwa moja ili kuzuia maandamano na kuepuka kuwajibika kwa ukiukaji wa haki za binadamu uliofanyika kipindi cha uchaguzi.

Jibu lipo wazi kwa anayetazama kwa jicho la kina: Huu ni mkakati wa kutafuta sababu ya halali ya kuinvoke Ibara ya 32 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani, kutangaza hali ya hatari au kwa lugha rahisi, Martial Law. Ibara hii inamruhusu Rais kutangaza hali ya dharura na kutoa mamlaka za ziada kwa jeshi, lakini kama inavyoeleweka katika muktadha wa kimataifa, inaweza kuwa chombo cha kukiuka haki za msingi, hasa ikiwa inatumika kisiasa badala ya kiusalama.

Martial Law Ni Nini na Inamaanisha Nini Kwetu?
Martial Law ni pale Rais anapotangaza rasmi kwamba jeshi linachukua mamlaka yote ya utawala, hii inafanyika katika hali ya dharura kama vita, ghasia za ndani, au vitisho vya usalama. Katika hali hii, haki za kiraia zinasitishwa mara moja. Kanuni za kimataifa kama Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), Ibara ya 4, zinahitaji kuwe na derogation (kutoa ruhusa ya kusitisha) rasmi, ambapo haki zisizoweza kusitishwa (non-derogable rights) kama haki ya kutotesa watu, uhuru wa dini, na haki ya kuishi lazima ziendelee kulindwa. Tanzania, kama nchi iliyosaini ICCPR, inaweza kutangaza derogation tu ikiwa kuna "hali ya dharura inayotishia uhai wa taifa," na hii lazima iwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndani ya siku chache na kuwasilishwa kwake lazima kuambatane na maelezo yenye viashiria vya kutaka kutokea machafuko ili umoja wa mataifa ukubari suala hilo, nadhani sasa tupo pamoja kwanini hizi Yada yada zinakuja sasa, ndio inatafutwa sababu ya kupata kibali cha kuinvoke Ibara ya 32 ya Katiba ya Tanzania, kitu ambacho wa Tanzania hawapasi kukubali kifanyike hata kidogo kwani kina madhara makubwa sana, yani hiyo ibara ikiwa invoked kunakuwa;

Hakuna uhuru wa kujieleza, kukusanyika, wala wa kuandamana , japo hii inakiuka Mkataba wa 4 wa Geneva (1949), ambao hulinda raia dhidi ya matamshi ya moja kwa moja au vitisho hata katika hali ya dharura, lakini haki hizo zinawezwa kubanwa sana katika kipindi cha tahadhari.

Mahakama za kiraia zinaweza kufutwa au kupunguzwa mamlaka, na raia kuhukumiwa na mahakama za kijeshi, ambazo mara nyingi hukikiuka Ibara ya 14 ya ICCPR inayotaka kuhakikisha kesi zianendeshwa kwa haki na bila upendeleo. Kama nchi ikiwa kwenye Martial Law Ibara hiyo haifanyikazi tena.

Unaweza kukamatwa, kupekuliwa, au kufungwa bila sababu wala hati kukamatwa, Hii pia japokuwa ni kinyume cha Ibara ya 9 ya ICCPR, ila inaweza kutumika katika kipindi cha Martial law kwa "muda mfupi" na kufanya hivyo kunakuwa halali, japo Mkataba wa 4 wa Geneva unazuia kufungwa bila sababu kwa wafungwa raia, ila kukiwa na Martial law hii inaweza kutokea pia.

Hakuna RC, DC, Mbunge, Diwani, Mwenyekiti wa kijiji wala Mjumbe wa nyumba kumi anayebaki na mamlaka yeyote, serikali inakuwa Rais na Jeshi tu, na jeshi linadhibiti sheria, utawala, na usalama wa umma.

Tangu uhuru, Tanzania haijawahi kutangaza Martial Law rasmi, ingawa Operesheni Sangara ya 1983 ilikuwa karibu sana kufanania na Marrtial Law, ambapo jeshi lilidhibiti maeneo mengi na kufunga maelfu bila kesi, na hii ilichukuliwa kama ukiukwaji wa haki za binadamu na mashirika ya kimataifa kama Amnesty International.
Hizi sheria wanaziitaga Zombie Law ambazo zipo kama hazipo, ila hapa kwetu ipo, tena mikononi mwa Rais, ikiidhinishwa na Bunge ndani ya siku chache, kulingana na Ibara ya 32 ya Katiba yetu inaweza kutumika.

Kuna kesi za karibu kabisa juu matumi ya sheria hii, Korea Kusini inaweza kuwa Kioo cha Hali Inayoweza Kutokea Tanzania

Desemba 3, 2024, Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini alitangaza Martial Law usiku wa manane, akidai upinzani unashirikiana na Korea Kaskazini kuleta machafuko lakini hakufanikiwa. Siku za hivi karibuni ameongezewa mashatka mengine ya uhaini baada ya kugundulika kwamba alikuwa ameamrisha drone zirushwe kuingia Korea Kaskazini kuprovoke vita kati ya nchi yake na nchi hiyo, ili tu apate sababu ya kisheria ya kuinvoke Martial Law na kuzuia kupigiwa kura ya kutokuwa na imani. Jamaa alifanya hivi ilikiuka Kanuni za Siracusa (siracusa principles 1985) zinazoeleza kuwa derogation chini ya ICCPR lazima "kuwe nasababu za kiusalama ili kuinvoke hali ya hatari na si kwa ajili ya kujikinga kisiasa, jamaa alikuwa inataka kutengeneza uhitaji wa kuiweka nchi katika hali ya hatari lakini alishindwa saa sita tu baada ya kuitangaza hali hiyo, maelfu ya raia walivunja vizuizi vya jeshi, kunishinikiza wabunge waingia bungeni kupinga uamuzi huo, na Martial Law ikabatilishwa. Yoon sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini chini ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa. Je, hii inafanana na kile tunachokiona sasa Tanzania, ambapo "foreign elements" na mabomu yanatumiwa kama kisingizio?

Kwa Nini Sasa Hivi?

Kwa sababu serikali inajua haiwezi kuvuka D9 kwa amani ikiwa raia wana agenda ya amani. Ili kuzuia maandamano makubwa na kuepuka kuwajibika kwa mauaji ya waandamanaji wa awali, njia pekee iliyobaki ni kuunda tishio kubwa la nje ili ku-justify kutangaza Martial Law. Hii ni kinyume na Kanuni za Siracusa (siracusa principles 1985), ambazo zinasema kuwa "migogoro ya ndani au machafuko yasiyokuwa hatari kubwa kwa maisha ya watu na ustawi wa taifa hayawezi kuhalalisha derogation."
Sasa ndiyo maana tunaona hizi habari za mabomu ya Mmarekani mkenya, M23, na "foreign elements".
Ni Yada yada za kutafuta sababu.

Suala linatakiwa liwe akilini mwa watanzania ninamna gani wanaweza kupambana Martial law

Raia Wana Nguvu Gani?
Hata kama Bunge letu ni "Cuban Marimba Band" inayoongozwa Juma Kilaza wa Ilala na kazi yake ni kupiga makofi kwa kila jambo, Martial Law haiwezi kudumu dhidi ya raia walioamua. Historia inathibitisha, na kanuni za kimataifa ikiwemo Mikataba ya Geneva (1949) na ICCPR inawapa raia nyenzo za kisheria. Hapa kuna mikakati ya kupambana na hali hii
  • Kukataa kuitambua (Civil Disobedience), Endelea na maisha ya kawaida bila kuomba ruhusa ya jeshi, kama mikutano, biashara, mazishi, na harusi. Watu waendelee na kazi bila kutii amri za kijeshi. Hii inategemea kanuni ya "kukataa amri haramu" chini ya na kuwataka wanajeshi kuikataa amri chini Mkataba wa Geneva wa mwaka 1977 Ibara ya 86(2) ambayo inaweza kuwajibisha askari ambao amefuata amri haramu (unlawfull command) bila ya kisingizio kuwa alifuta amri ya mkuu wake, hii itawakumbushakuwa askari mmoja mmoja anaweza kuwa mharifu wa kivita na Mkataba wa 4 wa Geneva, ambao unazuia jeshi kutumia nguvu dhidi ya raia wasio na silaha.
    Halii hii ilitokea Poland 1981, Solidarity Movement iliendelea na migomo hata baada ya Martial Law; serikali ililazimika kujadiliana na raia na kurejesha utawala wa kiraia baada ya miezi michache, na hii kulingana na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECtHR) ni haki halali chini ya ICCPR.


  • Kugoma kwa wingi (Mass Strike / General Strike) Watu wote wagome kufanya kazi Hii inaleta mdororo wa kiuchumi kwa haraka; serikali haiwezi kulipa mishahara ya jeshi bila uchumi unaofanya kazi hii itawakumbusha waanajeshi bosi wa ni nani na kwa niini wanaitwa jeshi la wananchi. Kuna mikataba ya kimataifa ya Haki za Kiuchumi, Jamii na Kitamaduni (ICESCR) inayolinda haki ya kugoma kama sehemu ya uhuru wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi, na hata katika hali ya dharura, ICCPR inazuia kutoa adhabu kwa wafanyakazi. Mfano: Philippines 1986, madereva wa teksi, wafanyakazi wa bandari, na wafanyabiashara waligoma; Marcos alilazimika kuondoka baada ya wiki chache, na maandamano haya yaliungwa mkono Kimataifa kama yana uhalali kwenye kupinga dhidi ya ukiukwaji wa haki za raia.

  • Kuvunja kizuizi kwa wingi (Human Barricades), Hii ni mbinu muhimu sana, kama Jeshi litaamua kushirikiana na serikali kundamiza haki za raia basi mnalitengenezea mazingira lifanya uharifu wa kivita. Hapa Maelfu ya raia wajikusanye mbele ya majeshi bila silaha, wakiimba nyimbo, wakisali, na kubeba picha za familia zao. Wanawake na watoto wawekwe msatali wa mbele ili kuwafanya askari waogope kufyatua risasi, na hii inawaweka wanajeshi katika hali ya kufanya uhalifu wa kivita chini ya Mkataba wa 4 wa Geneva, ibara ya 33 ambao unazuia mauaji ya raia na kutoa adhabu ya pamoja (Collective Punishment). South Korea Desemba 2024, raia walivunja kizuizi cha jeshi na kuwasaidia wabunge kuingia Bungeni kubatilisha Martial Law, na Umoja wa Mataifa ulitambua hii ilikuwa haki halili kwa raia kuitumia kushinda ukiukwaji wa ICCPR.

  • Kutumia mahakama za kimataifa na vyombo vya habari, Wanasheria na wanaharakati wafunguee kesi Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu (ICJ) au African Court on Human and Peoples' Rights, ikitumia Mkataba wa 4 wa Geneva na Kanuni za Siracusa ili kuonyesha kuwa Martial Law si ya kisheria.

    Watu warekodi video na picha za ukiukwaji wa haki za binadamu na kuzituma moja kwa moja BBC, Al Jazeera, CNN, Amnesty International hususani kwenye mazingira kama yetu ambapo hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Tumia VPN au kama una Starlink( hii inapatikana TZ, ukiwa nayo iweke kwenye roaming itafanyakazi) ili kuepuka kukatwa mtandao. Ibara ya 19 ya ICCPR inalinda uhuru wa kujieleza, na hata katika dharura, video za ukiukaji zinaweza kusababisha uchunguzi wa Umoja wa Mataifa.

  • Kuwagawanya wanajeshi (Fracture the Military) Familia za askari ziandamane mbele na ndani ya makambi: "Tuna njaa, mume wangu hayupo nyumbani." Wazazi wa askari waandike barua za wazi: "Mwana wangu si muuaji wa raia." Askari wa chini wagoma kutii amri kama ilivyotokea Romania 1989 wakati wa mapinduzi dhidi ya Ceaușescu, ambapo wanajeshi walikataa kufyatua risasi dhidi ya raia, na hii iliungwa mkono na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kama kutii amri haramu. Mkataba wa 3 wa Geneva unazuia hata askari dhidi ya kutoa amri za ukiukaji wa haki za raia.

  • Kuandaa serikali sambamba (Parallel Government) Wabunge wa upinzani, madiwani, na viongozi wa dini waunde “Baraza la Kitaifa la Ukombozi” na watoe tamko rasmi: “Serikali ya kijeshi si halali.” Hii inalindwa na Kanuni za Siracusa, ambazo zinasema serikali lazima iwe na uhalali wa umma. Mfano: Myanmar 2021, CRPH iliundwa na wabunge waliochaguliwa; ingawa haikushinda moja kwa moja, ilipunguza uhalali wa serikali ya kijeshi na mpaka sasa serikali hiyo haina nguvu na inahitaji kukaa kuzungumza na raia ambao bado wameshikria msimo wao waa kutotaka mazungumzi hali iliyo sababisha kuanza uchunguzi na ICJ juu utawala huo wa kiimla.

  • Kuwashinikiza wafanyabiashara na wamiliki wa mali, Wafanyabiashara wafunge maduka, benki, viwanda, serikali itapoteza mapato ya kodi haraka. Kila mtu agome kutoa ushirikiano wala huduma kwa jeshi. Hii inalenga kiuchumi, na ICESCR inalinda haki ya kufanya biashara bila kuingiliwa, hata katika dharura.


Kuifupi serikali imeingiwa na tamaa ya kuinvoke Ibara ya 32 ya katiba ya Tanzania, ilikuikwepa D9 AKA D-DAY, ila hata hiyo tamaa yao haitafanya kazi kama raia wataamua
Jeshi lina silaha,
lakini raia wana idadi, uchumi, na uhalali wa kimataifa chini ya mikataba ya Geneva na ICCPR, ambayo inalazimisha kuhesimu haki za kibinadamu kwa raia na zinazuia matumizi mabaya ya Martial Law.
Waache waendelee na hizo Yada Yada zao za mabomu za M68 sijui M23, sijui wakenya, lakini Hakuna Martial Law iliyowahi kudumu zaidi ya wiki kaza pale ambapo raia wameamua.
 
Inawezekana kabisa kwa Tanganyika kuwekewa martial law na huyu mzanzibar ila ajiandae na
Athari za kuweka martial law

- Kitaifa:
- Kuporomoka kwa imani ya wananchi kwa serikali.
- Uharibifu wa mali, vifo, na majeraha kama ilivyoshuhudiwa kwenye maandamano ya awali.
- Kuzorota kwa uchumi kutokana na hofu ya wawekezaji na machafuko.

- Kimataifa:

- Hatari ya vikwazo kutoka kwa jumuiya za kimataifa.
- Kupoteza msaada wa maendeleo au ushirikiano wa kimataifa.

🔍 Hitimisho

Ingawa Tanzania inaweza kuchukua hatua kali dhidi ya maandamano, kuweka martial law ni hatua ya mwisho kabisa na yenye athari kubwa, inayopaswa kuzingatia sheria za kitaifa na kimataifa. Badala yake, serikali inapaswa kuheshimu haki ya wananchi ya kuandamana kwa amani na kushughulikia malalamiko yao kwa njia ya
kidemokrasia.
 
Tz hakuna serikali kuna mbogamboga kama mchicha, matembele, spinach n.k. Halafu na wewe punguza mgazeti kusoma sana inachosha ubongo.
 
Ulivyotoa mfano wa mapinduzi ya Romania nimekuelewa sana
 
Andiko bora sana.
Hapa unatupa elimu wananchi.
Unatusanua kwa lugha ya mtaani.
 
Back
Top Bottom