Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,521
- 4,381
Mtume Musa baada ya kuwatoa waisraeli Misri aliua sana. Mungu pia aliua sana, alifikia hatua akataka kuwaua Waisraeli wote akamwahidi Musa akisema nami nitakufanya wewe Taifa kubwa na lenye nguvu kuliko wao. Kwanini? Kwasababu walikuwako "hardliners" na waliobobea waliokuwa wakifaidi makombo ya Mafarao ndio waliokuwa wakiushawishi umma mara kwa mara kwamba NI AHERI TURUDI MISRI.
Hata nyakati zetu wapo wanaofaidi makombo ya wadhulumaji. Fikiria ACACIA inavuna makinikia yetu, inasomba utajiri wetu kupeleka nje ikituachia umaskini. Wapo waliotetea wakisingizia sheria za kimataifa na mikataba. Hawa ndio wala makombo. Kwamba wanyonyaji wanauza makinikia ya mabilioni ya dola kisha wakinyofoa dola milioni moja na kumpa Lawyer akili inamhama anatetea dhuluma.
Hayo makampuni yanaziingizia serikali zao mapato makubwa kiasi kwamba serikali hiyo ikitoa dola milioni 500 kuisaidia Tanzania Rais (omaomba) anaona amepata kitu kikubwa, amefadhiliwa na anawaona wanyonyaji mithili ya malaika akidhani wanamsaidia kwasababu wana huruma, kumbe wanamtupia makombo.
Hao wala makombo ndio wanaojifanya kuwa mstari wa mbele kutoa tafsiri za HAKI demokrasia na udikteta shame upon them.
SISI tutaendelea kusimama na Mungu wa kweli, tutasimama na Mungu wa haki hadi tutaufikia ukombozi kamili. Tanzania yenye neema yaja na italetwa na mashujaa siyo wala makombo ya ubeberu.