Tunataka kurudishwa Misri tulipolishwa makombo na mifupa huku nyama ikiliwa na wachache

Pale mwanaume sifa yako inapokuwa ni uongo na umbea.
 
Nadhani hukucheki statistics za mikopo mwaka 2015 -2020. Serikal haijawahi kuacha kukopa. check your facts again
Hakusema kukopa....kasema "kuomba" kukopa unarudisha ukiomba unapewa kwa matashi ya anayekupa...
 
Usiogope Mungu aliye hai yupo.
Simama tu kwenye zamu yako,maana anahitaji mtu Wala si watu wa kusimama palipo bomoka.
 
Sawa Mhubiri!
 
Wenye akili tu ndio wanaoweza kujadili mada hii kwa hoja za msingi wengine wote wataleta matusi tu apa
 
Rais Samia anakwenda kuifanyia rebranding Tanzania, hana uoga wa kujichanganya na watu wa mataifa mbalimbali. Anatumia nguvu ya diplomasia katika kulikuza jina la nchi hii iliyojaliwa utajiri wa rasilimali za kila aina.

Anayo thinking tofauti na ile ya marais wa kiume na hii ni added advantage. Anakuwa na aina ya uongozi wenye kujishusha na dunia ikikuelewa namna hiyo maana yake mipango yako mingi ni lazima iwe na matunda yanayomfikia mwananchi wa kawaida.

Mleta uzi jitahidi kuondokana na mwili kuwepo leo halafu akili zote zikabakia jana. JPM ni shujaa lakini amekwisha kulala usingizi wa milele.
 
Umeandika ujinga.

Hivi kuna nini kilicho tofauti sasa na zamani kuhusiana na biashara ya makinikia? Marehemu was a good president for the fools kama huyu. Hawa ndio aliowaharibu akili, akaalisha uwongo na ujinga, wakaupokea na wameamua kuishi nao.

Nataka nikuhakikishie, hakuna kilichobadilika. Makinikia toka mwanzo yalikuwa yanaenda nje, yanalipiwa kodi, na ndivyo inavyofanyika sasa. Ila sasa hivi, tofauti na mwanzo, kwenye mkataba waliosaini Barrick na Serikali, Serikali hairuhusiwi kusimamisha uchimbaji wala usafirishaji dhahabu au makinikia, hata kukiwa na dispute.
 
Inakuwa vigumu sana kuunga mkono hoja zako, kwa sababu unaziegemeza kwa mtu ambaye mambo yake mengi yameumiza watu.

Mada kama hii isimamie mwenyewe, huna lazima yoyote ya kuiegemeza kwa huyo mtu wako. Tupo tunaoweza kushiriki kuunga mkono mawazo ya namna hii kama ndio msimamo wako.
 
Uko sahihi, kuna mamluki wa kufaida keki, na hao wako radhi kufanya upotoshaji kuliko kusimamia haki.
Mbaya zaidi wengi wao ndio walikuwa wakimsaidia musa ili tufike nchi ya maziwa na asali leo wamegeuka kina Kora na dothani. Shame on you.
 
Sawa Mhubiri!
Mpotoshaji tu huyo, anatumia maandiko out of context, hajui maandiko wala nini! Anahalalisha maovu ya awamu ile kwa ku-quote Kwamba Musa ailiuwa na Mungu aliuwa! Hawa ndo wale walioliabudu jiwe wakalisababishia hukumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…