MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mwaka 2020 kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kulikuwa na kauli maarufu sana ya CHADEMA kwamba wanataka maendeleo ya watu badala ya maendeleo ya vitu. Hoja yao ilimaanisha kwamba serikali ya awamu ya tano ilijikita kwenye miradi ambayo ilikuwa haimgusi mwananchi moja kwa moja.
Miradi kama ujenzi wa meli, barabara, SGR, majengo ya serikali na zahanati kwao ilikuwa haina maana. Walitaka miradi inayomgusa mwananchi direct. Hiyo kauli ilitokana na wao kukosa cha kusema kwasababu wananchi walikuwa na ushahidi wa wazi kwa kazi iliyofanywa na serikali ya CCM kwenye awamu ya tano.
Ni kama Mama Samia alichukulia kwa uzito kauli hii na kuamua kuifanyia kazi hadi kusababisha kusifiwa sana na wapinzani kwenye mikutano yao. Idadi ya miradi inayogusa wananchi moja kwa moja ni mingi sana kwa sasa ila hapa nitataja michache;
1. Ujenzi wa barabara toka Mpombwe hadi Kipwa wilayani Kalambo. Hiki kijiji kilikuwa hakina kabisa mawasiliano ya barabara kwa miaka mingi. Na sio barabara hiyo tu.. ipo ya Nyakanazi - Kasulu pia na zingine nyingi.
2. Ujenzi wa madarasa kwenye shule zote nchini Tanzania.
3. Miradi ya kilimo chini ya komredi Bashe. Hapa kwenye kilimo Bashe anaupiga mwingi sana kiasi kwamba muda sio mrefu tutakuwa na mamilionea wapya vijana kupitia kilimo.
4. Mikopo kwa vijana kupitia halmashauri inatolewa kwa kasi.
5. Mradi wa kupanua Demokrasia; Hapa ndio eneo lililolalamikiwa sana na upinzani ila tumeona Mama akipambana kuimarisha demokrasia nchini. Wafungwa wote wa kisiasa wameachiwa na mikutano ya hadhara kuruhusiwa. Sio hivyo tu bali uhuru wa watu kutoa maoni umeboreshwa.
Mimi nashauri CHADEMA na vyama vingine vya upinzani kuendelea kusifu jitihada za serikali ya awamu ya sita kupitia mikutano yao ya hadhara.