Yeah mimi nimemaliza. Unajua labda mtu ataona tu Hilo la mwanangu lakini Kuna jumbe mbili ndani yake.
1. Kuna watu wanaotupa watoto wakiwazaa.
2. Kuna wale ambao watoto wanao lakini hawawajali.
Kuna siku nilikuwa naenda sehemu kwenye dalalada nikakutana na dada mmoja yupo na mwanae kamuweka kiupande upande hajampakata vizuri ana miaka kama 5 hivi, yule mtoto akawa anasinzia anamuegamia mama yake, mama mtu sasa akaanza kumsukumiza na kumfokea.
"Aaahh!! Ndo mbona sipendagi kutembea na wewe , embu Kaa, usilale lale".
Yeye cha maana afanyacho Hana yupo bize na simu anachat , nikapotezea mara ya kwanza , mara ya pili eehh yatatu ikanishinda , nikamwambia hebu mlete hapa, nikampakata vizuri , nikamwambia yule mtoto haya lala. Nia na madhumuni ilikuwa natoa somo mama mtu aone kwa vitendo mtoto sio wa kusukumwa sukumwa hovyo.
Kwahiyo Kuna watu Wana watoto lakini kuwalea kwa mapenzi hawawezi kbsaa.
Kwahy ndugu yetu kaona ujumbe wa kufiwa tu na kukariri kusikitika, ni maoni yake nayaacha kama yalivyo.