BEITO INTERNATIONAL COMPANY LTD tunajihusisha na shughuli za usafi na bustani (gardening)
Ofisi zetu zipo Dar es Salaam, Wilaya ya Kinondoni, Tegeta Nyuki jengo la Nyuki House, Floor ya kwanza ofisi namba 16.
SIFA TUNAZOTARAJIA KUTOKA KWA MUOMBAJI NI KAMA IFUATAVYO:-
1. Uaminifu wako ni sifa kubwa zaidi pia uwe na haiba na tabia njema isiyo na mashaka.
2. Mkweli, mcheshi na mkarimu
3. Uwe unaishi sehemu Dar es Salaam hususan maeneo haya ( Kawe, Mikocheni, Msasani, Kinondoni, Makumbusho, Mawasiliano Mwenge, Mbezi beach, Magomeni, Ubungo)
4. Ujue kusoma na kuandika
5. Mwenye experience ya kazi husika angalau kuanzia miezi (6) atapewa kipaumbele.
NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI
Fika mwenyewe katika Ofisi zetu zilizopo TEGETA NYUKI, Jengo la Nyuki House, Bagamoyo road kwa ajili ya usaili mfupi.
Fika kati ya Jumatatu hadi Ijumaa; muda kuanzia saa sita mchana - tisa mchana
Mawasiliano: + 255 742 417 677
Fika na nakala zifuatazo.
1.Barua ya maombi ya kazi, ikiainisha uweledi wako katika kazi.
Maombi yatumwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
BEITO International Company Ltd
S.L.P 391,
Dar es Salaam.
2. Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Mtaa
3. Uthibitisho kuwa haujawahi kuhusika na makosa ya jinai kutoka kituo cha Polisi unapoishi (Ni muhimu lakini siyo lazima).
4. Nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) au kitambulisho kingine kinachotambulika.
5. Barua ya mdhamini na mawasilino yake ( anaweza kuwa ndugu, mwenza au mzazi).
6. Cheti kama unacho (siyo lazima) chochote kinachoendana na aina ya kazi