GE2025 Tunatokaje? Huu utakuwa uzi maalum. Mihemko tuweke pembeni. Ila ukweli na suluhu tusiviache

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hamjambo wakuu!

Poleni wote kwa yote yaliyotokea. Waliopoteza wapendwa wao, waliopata majereha, waliopoteza mali iwe kwa kuibiwa au kuchomwa moto. Na zaidi Mungu awape pumziko linalowastahili waliopoteza maisha.

Upande wangu mambo yalikuwa magumu sana ukizingatia ninapoishi na karibu kabisa na barabara kuu ya Morogoro road ambapo hekaheka zilikuwa zikiendelea tangu siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho. Risasi, fataki na mabomu ya machozi vilirindima mara kwa mara katika nyumba yetu.

Hakika watoto walipata tabu hasa siku ya kwanza kwani ndio mapambano yalikuwa makali. Moshi wa mabomu ya machozi ulikuwa ukiingia ndani. Usiulize kuhusu vioo kwani unaelewa nini kilitokea.

Umeme ulikatika so siku tatu tangu tarehe 29-31 tulikuwa giza. Watu kadhaa walipigwa risasi nikiwa nashuhudia dirishani. Mmoja kati yao alifariki.

Haya yote nazungumzia ili kuonyesha hatari, matokeo au madhara ya mambo kama haya. Kwamba wapo walioathirika moja kwa moja tangu siku ya kwanza, wapo waliopoteza maisha, wapo walioibiwa, walioharibiwa mali na biashara zao, kisha na wale ambao wamelala njaa kwa kukosa pesa ya kula

Wapo ambao walikuwa wamefika stendi kutokea mkoani hawa nao moto uliwawakia kwa hapakuwa na usafiri. Barabara zilitawaliwa na doria ya kufa mtu zilizofanywa na polisi.

Nikiacha stori sasa maana kila mtu anastori yake na tutakesha hapa.

Mambo ninayoyaona;

1. Ni kweli bado watu wana hasira. Hilo nimefuatilia kwa kupita huku na huko.
Hizi hasira za hawa watu zinapaswa zitafutiwe suluhu bora yenye kulileta taifa pamoja.

2. Mbinu mpya zitafutwe. Mbinu za nguvu zinaonekana kugonga mwamba. Matumizi ya nguvu yanalundika chuki, hisia za maumivu katika mioyo ya watu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.

3. Kuna haja ya kutafuta maridhiano na suluhu ya kweli hasa inayogusa wananchi wa kawaida ambao wengi ndio walioandamana na kuleta machafuko.
Tusijidanganye kuwa tutawadhibiti siku zote

Kilichotokea wote tunakiri hakijawahi kutokea. Na limekuwa jambo kubwa sana kwetu.

4. Uundwe mkakati wa kuing'oa mbegu ya chuki inayomea baina ya Wananchi wa chini na Watawala ambayo naona inahamia kwa Polisi.

5. Kutunishiana misuli hakutakuwa na mshindi zaidi kila mtu atapoteza hasa taifa letu. Kwani itakuwa kama vita ya gangs ambazo hazinaga mwisho wala hazinaga mshindi.
Hekima na busara na muhimu sana.

6. Hekima na Busara ni zipi sasa?
Kuna njia mbili;
a) Haki itendeke.
Kwamba maovu yaliyofanyika na yaliyopitiliza lazima yalipwe kwa haki.

b) Kusubiri Watu wasahau ikiwa ni wasahaulifu.
Kikawaida watu wasio na haki ni wasahaulifu. Yaani hawana kisasi.
Mbinu ya kupoteza muda na kuwasahaulisha zikitumika tutarudi kama zamani.

Kutenda haki najua ni ngumu hasa kwa watawala wa kibinadamu. Kwamba mtu alikuwa kiongozi leo akanyee debe au afungwe kifungo cha maisha au kuhukumiwa kunyongwa. Kwa kweli ni binadamu wachache wenye nafasi ya mamlaka atakubali kitu kama hicho.

Kwenye biblia Binadamu aliyeweza kujihukumu akiwa na mamlaka tena hukumu ya kuuawa Baada ya kulala na mkwewe ni Yuda mtoto wa YAKOBO.
Na hiyo ndio Legacy kuu ya Yuda mpaka hivi leo na hata Yesu kuitwa Simba wa Yuda.

7. Ni kweli watu wamekufa. Tunafanyaje?
Tuwaache wafe kama panya? Kwa sababu tutasanganya mataifa mengine lakini vipi sisi wenyewe humu ndani tutajidanganya? Tutapuuza?
Hali iliyotokea tutaona ni kawaida?

Jibu ni kuwa sio kawaida.

8. Huu sio muda wa kulaumiana kwamba nani kasababisha haya.
Upande wa serikali unasema waliosababisha haya ni wachochezi wa maandamano, na serikali inasema itachukua hatua kali. Lakini swali linakuja je hiyo ndio suluhu?
Tangu nimeanza kuona waandika mtandaoni wakifuatilia na kukamatwa mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita. Je imesaidia kuzuia kilichotokea. Jibu ni hapana! Zaidi sana imechochea.

9. Waandamanaji wao wanasema serikali na askari wapo responsible n kilichotokea kwa madai kwamba wao walikuwa wanadai haki ya kuzuia uchaguzi kwa kuhitaji reforms. Na kudai haki za waliotekwa na kuuawa.
Lakini bahati mbaya zaidi kwenye maandamano ambayo kwa hakika uhalifu ulitokea wa kuvunja, kuiba na kuchoma vilitokea. Jambo ambalo halikuwa sahihi kufanywa na waandamanaji.
Wakati upande wa pili askari nao wakifanya makosa kwa kutumia nguvu kubwa mpaka kupelekea kuua watu wengi..

10. Ni muhimu viongozi wakuu wa juu wakitoa matamko watao kwa uangalifu mkubwa sana tena ikibidi. Sio lazima wazungumze hasa kama wanajijua wanaweza kuzungumza kauli tata au zenye kuleta hisia za mihemko kwa wasikilizaji.

11. Tatizo la haki ni kuwa inakata yoyote. Watekaji na wauaji wapewe haki zao. Na waliofanya uhalifu kwenye maandamano wapewe haki zao kwa mujibu wa sheria.

12. Sishauri tujifanye kama hakijatokea kitu. Haitakuwa nzuri huko baadaye. Tusipuuze.
Tumeona huu mwanzo ulivyokuwa. Hatujui na haitabiriki huko mbele nini kitatokea.

13. Tusi-bet. Tusitumie mabavu. Tulipofikia sio sehemu ya kutumia mabavu tena.

14. Tunaweza kuwapa wananchi wanachotaka kwa makubaliano ya usalama. Najua ni ngumu lakini ndio njia salama ya kuokoa pande zote mbili.
Hapa kuna mambo kadhaa.
Baadhi ya viongozi wanahofia usalama wao na mali zao iwe walizichuma kihalali au kifisadi.
Wakati wananchi wao wanahitaji katiba mpya itakayowapa wananchi haki sawa hasa kwa upande wa vyama vyote vya siasa kuwa na haki sawa.

15. Maridhiano ya amani yanayohusu kusameheana yanatakiwa yawe ya dhati na kuwe na mabadiliko ya. Kikatiba yatakayozuia matukio ya utekaji na mauaji.
Kiburi kisiwe wala kushiriki katika meza ya mazungumzo kila mmoja afike akiwa na lengo la kutaka amani sio tuu ya utulivu wa nchi bali amani ya Moyo wake.

16. Unajua maandamano ya chuki ya kuhamasisha sijui nyumba ya fulani iko wapi, sijui mali ya fulani iko wapi, ni hatua kamili ya kufikia ugaidi. Kama taifa hatutakiwi kufikia huko. Ugaidi hauondolewi na vitisho.
Ugaidi ni imani iliyokomaa kwa mtu aliyeona hana njia nyingine zaidi ya kujitoa mhanga kufanya uhalifu bila kufuata Sheria za kiungwana.

17. Kilichotokea tumeona. Ule ni uhalifu ambao unadhuru watu wote. Waliomo na wasiokuwemo. Hata hatua ya kukabiliana na ugaidi ni hatari zaidi kwani lazima utajikuta unawapiga hata wasiohusika. Na kuongeza kama sio kupanua maadui.

18. Ninaomba watu washushe mioyo yao. Najua maumivu ya kuonewa yakoje, kudhulumiwa, kutekwa, na kuondokewa na mwenza. Serikali nanyi msikaze shingo mkifikiri kuwa nguvu mnayo. Jishusheni. Meza ya mazungumzo mkae.
Kisha mjadili haki itendekeje bila ubinafsi.

Hofu na mihemko ikiamua haki huleta madhara makubwa sana. Kwani kisasi kinachoendeshwa na mihemko na hofu kinadhuru wahusika na wasiohusika.

Hata hayo mambo ya utekaji ni matokeo ya kile kile kiitwacho hofu.
Sasa njia pekee ya kuondokana na hofu ni kukaa na kuzungumza kwa dhamiri.

Kwa sababu bila kufanya hivyo wote tunajua kuwa tutaumizana sana hata kama wengine wataumia kwa kuchelewa lakini kila mtu atafikiwa na maumivu kwa wakati wake. Ni suala la muda bila kujali ni mkubwa au mdogo. Muonewa au unayeonea.

Kwa sababu ugomvi unatanuka na wahusika wanaongezeka.

Kufikia hapa sina la ziada.
Tulinde nchi yetu.
Tutende Haki.
Tupendane.
Tusikamiane na kuviziana. Hakunaga mshindi kwenye vita za ndugu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Wewe ni shabiki wa muuaji Samia hebu tuache🚮🚮🚮🚮
 
Kilichoniacha hoi ni kuwa siku zote Mbogamboga walikuwa wanatumia "Substitution method" tu ili kufanikisha uchaguzi ila this time around wameamua kuongeza na "Elimination method".

Wametumia njia zote mbili ila hii ya "Elimination method" ni mbaya mno. Wangebaki na ile ile ya substitution tu.

Kwa wale magwiji wa mahesabu mtakuwa mnaelewa vyema zaidi😂!
 
Kuna haja ya watu kuweka mambo sawa.
Haya mambo hayaishi hivihivi bila hatua za haki na maelewano kuchukuliwa.
 
Ushauri mzuri .... NAJIULIZA TU UNAMSHAURI NANI ? Kama uliwasikia watawala wameshatoa statement kuwa waandamanaji hawakuwa wa Tanzania, ni vifo tu ndiyo zimetokea kwa wa Tanzania.. tulipofika sasa hatuna msaada zaidi ya MUNGU wa Mbinguni .
 
Hamjambo wakuu!

Poleni wote kwa yote yaliyotokea. Waliopoteza wapendwa wao, waliopata majereha, waliopoteza mali iwe kwa kuibiwa au kuchomwa moto. Na zaidi Mungu awape pumziko linalowastahili waliopoteza maisha.

Upande wangu mambo yalikuwa magumu sana ukizingatia ninapoishi na karibu kabisa na barabara kuu ya Morogoro road ambapo hekaheka zilikuwa zikiendelea tangu siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho. Risasi, fataki na mabomu ya machozi vilirindima mara kwa mara katika nyumba yetu.

Hakika watoto walipata tabu hasa siku ya kwanza kwani ndio mapambano yalikuwa makali. Moshi wa mabomu ya machozi ulikuwa ukiingia ndani. Usiulize kuhusu vioo kwani unaelewa nini kilitokea.

Umeme ulikatika so siku tatu tangu tarehe 29-31 tulikuwa giza. Watu kadhaa walipigwa risasi nikiwa nashuhudia dirishani. Mmoja kati yao alifariki.

Haya yote nazungumzia ili kuonyesha hatari, matokeo au madhara ya mambo kama haya. Kwamba wapo walioathirika moja kwa moja tangu siku ya kwanza, wapo waliopoteza maisha, wapo walioibiwa, walioharibiwa mali na biashara zao, kisha na wale ambao wamelala njaa kwa kukosa pesa ya kula

Wapo ambao walikuwa wamefika stendi kutokea mkoani hawa nao moto uliwawakia kwa hapakuwa na usafiri. Barabara zilitawaliwa na doria ya kufa mtu zilizofanywa na polisi.

Nikiacha stori sasa maana kila mtu anastori yake na tutakesha hapa.

Mambo ninayoyaona;

1. Ni kweli bado watu wana hasira. Hilo nimefuatilia kwa kupita huku na huko.
Hizi hasira za hawa watu zinapaswa zitafutiwe suluhu bora yenye kulileta taifa pamoja.

2. Mbinu mpya zitafutwe. Mbinu za nguvu zinaonekana kugonga mwamba. Matumizi ya nguvu yanalundika chuki, hisia za maumivu katika mioyo ya watu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.

3. Kuna haja ya kutafuta maridhiano na suluhu ya kweli hasa inayogusa wananchi wa kawaida ambao wengi ndio walioandamana na kuleta machafuko.
Tusijidanganye kuwa tutawadhibiti siku zote

Kilichotokea wote tunakiri hakijawahi kutokea. Na limekuwa jambo kubwa sana kwetu.

4. Uundwe mkakati wa kuing'oa mbegu ya chuki inayomea baina ya Wananchi wa chini na Watawala ambayo naona inahamia kwa Polisi.

5. Kutunishiana misuli hakutakuwa na mshindi zaidi kila mtu atapoteza hasa taifa letu. Kwani itakuwa kama vita ya gangs ambazo hazinaga mwisho wala hazinaga mshindi.
Hekima na busara na muhimu sana.

6. Hekima na Busara ni zipi sasa?
Kuna njia mbili;
a) Haki itendeke.
Kwamba maovu yaliyofanyika na yaliyopitiliza lazima yalipwe kwa haki.

b) Kusubiri Watu wasahau ikiwa ni wasahaulifu.
Kikawaida watu wasio na haki ni wasahaulifu. Yaani hawana kisasi.
Mbinu ya kupoteza muda na kuwasahaulisha zikitumika tutarudi kama zamani.

Kutenda haki najua ni ngumu hasa kwa watawala wa kibinadamu. Kwamba mtu alikuwa kiongozi leo akanyee debe au afungwe kifungo cha maisha au kuhukumiwa kunyongwa. Kwa kweli ni binadamu wachache wenye nafasi ya mamlaka atakubali kitu kama hicho.

Kwenye biblia Binadamu aliyeweza kujihukumu akiwa na mamlaka tena hukumu ya kuuawa Baada ya kulala na mkwewe ni Yuda mtoto wa YAKOBO.
Na hiyo ndio Legacy kuu ya Yuda mpaka hivi leo na hata Yesu kuitwa Simba wa Yuda.

7. Ni kweli watu wamekufa. Tunafanyaje?
Tuwaache wafe kama panya? Kwa sababu tutasanganya mataifa mengine lakini vipi sisi wenyewe humu ndani tutajidanganya? Tutapuuza?
Hali iliyotokea tutaona ni kawaida?

Jibu ni kuwa sio kawaida.

8. Huu sio muda wa kulaumiana kwamba nani kasababisha haya.
Upande wa serikali unasema waliosababisha haya ni wachochezi wa maandamano, na serikali inasema itachukua hatua kali. Lakini swali linakuja je hiyo ndio suluhu?
Tangu nimeanza kuona waandika mtandaoni wakifuatilia na kukamatwa mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita. Je imesaidia kuzuia kilichotokea. Jibu ni hapana! Zaidi sana imechochea.

9. Waandamanaji wao wanasema serikali na askari wapo responsible n kilichotokea kwa madai kwamba wao walikuwa wanadai haki ya kuzuia uchaguzi kwa kuhitaji reforms. Na kudai haki za waliotekwa na kuuawa.
Lakini bahati mbaya zaidi kwenye maandamano ambayo kwa hakika uhalifu ulitokea wa kuvunja, kuiba na kuchoma vilitokea. Jambo ambalo halikuwa sahihi kufanywa na waandamanaji.
Wakati upande wa pili askari nao wakifanya makosa kwa kutumia nguvu kubwa mpaka kupelekea kuua watu wengi..

10. Ni muhimu viongozi wakuu wa juu wakitoa matamko watao kwa uangalifu mkubwa sana tena ikibidi. Sio lazima wazungumze hasa kama wanajijua wanaweza kuzungumza kauli tata au zenye kuleta hisia za mihemko kwa wasikilizaji.

11. Tatizo la haki ni kuwa inakata yoyote. Watekaji na wauaji wapewe haki zao. Na waliofanya uhalifu kwenye maandamano wapewe haki zao kwa mujibu wa sheria.

12. Sishauri tujifanye kama hakijatokea kitu. Haitakuwa nzuri huko baadaye. Tusipuuze.
Tumeona huu mwanzo ulivyokuwa. Hatujui na haitabiriki huko mbele nini kitatokea.

13. Tusi-bet. Tusitumie mabavu. Tulipofikia sio sehemu ya kutumia mabavu tena.

14. Tunaweza kuwapa wananchi wanachotaka kwa makubaliano ya usalama. Najua ni ngumu lakini ndio njia salama ya kuokoa pande zote mbili.
Hapa kuna mambo kadhaa.
Baadhi ya viongozi wanahofia usalama wao na mali zao iwe walizichuma kihalali au kifisadi.
Wakati wananchi wao wanahitaji katiba mpya itakayowapa wananchi haki sawa hasa kwa upande wa vyama vyote vya siasa kuwa na haki sawa.

15. Maridhiano ya amani yanayohusu kusameheana yanatakiwa yawe ya dhati na kuwe na mabadiliko ya. Kikatiba yatakayozuia matukio ya utekaji na mauaji.
Kiburi kisiwe wala kushiriki katika meza ya mazungumzo kila mmoja afike akiwa na lengo la kutaka amani sio tuu ya utulivu wa nchi bali amani ya Moyo wake.

16. Unajua maandamano ya chuki ya kuhamasisha sijui nyumba ya fulani iko wapi, sijui mali ya fulani iko wapi, ni hatua kamili ya kufikia ugaidi. Kama taifa hatutakiwi kufikia huko. Ugaidi hauondolewi na vitisho.
Ugaidi ni imani iliyokomaa kwa mtu aliyeona hana njia nyingine zaidi ya kujitoa mhanga kufanya uhalifu bila kufuata Sheria za kiungwana.

17. Kilichotokea tumeona. Ule ni uhalifu ambao unadhuru watu wote. Waliomo na wasiokuwemo. Hata hatua ya kukabiliana na ugaidi ni hatari zaidi kwani lazima utajikuta unawapiga hata wasiohusika. Na kuongeza kama sio kupanua maadui.

18. Ninaomba watu washushe mioyo yao. Najua maumivu ya kuonewa yakoje, kudhulumiwa, kutekwa, na kuondokewa na mwenza. Serikali nanyi msikaze shingo mkifikiri kuwa nguvu mnayo. Jishusheni. Meza ya mazungumzo mkae.
Kisha mjadili haki itendekeje bila ubinafsi.

Hofu na mihemko ikiamua haki huleta madhara makubwa sana. Kwani kisasi kinachoendeshwa na mihemko na hofu kinadhuru wahusika na wasiohusika.

Hata hayo mambo ya utekaji ni matokeo ya kile kile kiitwacho hofu.
Sasa njia pekee ya kuondokana na hofu ni kukaa na kuzungumza kwa dhamiri.

Kwa sababu bila kufanya hivyo wote tunajua kuwa tutaumizana sana hata kama wengine wataumia kwa kuchelewa lakini kila mtu atafikiwa na maumivu kwa wakati wake. Ni suala la muda bila kujali ni mkubwa au mdogo. Muonewa au unayeonea.

Kwa sababu ugomvi unatanuka na wahusika wanaongezeka.

Kufikia hapa sina la ziada.
Tulinde nchi yetu.
Tutende Haki.
Tupendane.
Tusikamiane na kuviziana. Hakunaga mshindi kwenye vita za ndugu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Umeongea mambo ya msingi sana!! Suluhisho ni kusikiliza madai ya wananchi na kutumia hekima na busara kupata muafaka!! Robert hao majeruhi na waliokufa ulivyowaona watakua wametoka Taifa gan la nje ya Tanzania? Ndivyo tumeambiwa ni raia wa nje ya nchi!!
 
Naona huko kachagua mwanasheria wa serikali chapu...anajua kinachoenda kutokea
 
Kuna watu ukiwaambia huu ni mwanzo wanaweza wasikuelewa. Jambo kubwa unaloweza kumtisha mwanadamu ni KIFO, Watanzania wamekiona kifo kilivyo, wamekinusa kifo. Mioyo yao haina hofu tena.

Hawa watu watapokuja wakati mwingine hawatakuja mikono mitupu.

Wito wangu kwa viongozi waendelee kushupaz shingo. Wameshinda pambano, hawajashinda vita.
Sahihi. Kitakachofuata watu watu watakuja vizuri mno wasichojua haya magobole yanatengenezwa kitaani tu na wawindaji... Watu wanajipanga
 
Kufanya suluhu na mtu kashika panga nyuma ni uchizi...Kwa ufupi tunaonekana sisi watz hatuna chetu na wala wa kututetea. Viongozi tumewaona wapo kwa ajiri ya maslahi yao ...Mtu anasema waandamaji sio watz ni watu kutoka nje ndo maana wakawa wanapiga risasi km wanapiga ukuta.Kuna mapandikizi ya masnich ndani ya vyombo vyetu na taasisi zetu ndo maana hawa wauaji wananguvu na jeuri watanzania inatakiwa tujipange hasa na sio kukurupuka tukikiamsha tukiamshe kweli..UZURI MASNICH WOTE TUMEWAONA LIVE TBC WAKIJIAPISHA hao si wa kuacha ili iwe fundisho
 
Hamjambo wakuu!

Poleni wote kwa yote yaliyotokea. Waliopoteza wapendwa wao, waliopata majereha, waliopoteza mali iwe kwa kuibiwa au kuchomwa moto. Na zaidi Mungu awape pumziko linalowastahili waliopoteza maisha.

Upande wangu mambo yalikuwa magumu sana ukizingatia ninapoishi na karibu kabisa na barabara kuu ya Morogoro road ambapo hekaheka zilikuwa zikiendelea tangu siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho. Risasi, fataki na mabomu ya machozi vilirindima mara kwa mara katika nyumba yetu.

Hakika watoto walipata tabu hasa siku ya kwanza kwani ndio mapambano yalikuwa makali. Moshi wa mabomu ya machozi ulikuwa ukiingia ndani. Usiulize kuhusu vioo kwani unaelewa nini kilitokea.

Umeme ulikatika so siku tatu tangu tarehe 29-31 tulikuwa giza. Watu kadhaa walipigwa risasi nikiwa nashuhudia dirishani. Mmoja kati yao alifariki.

Haya yote nazungumzia ili kuonyesha hatari, matokeo au madhara ya mambo kama haya. Kwamba wapo walioathirika moja kwa moja tangu siku ya kwanza, wapo waliopoteza maisha, wapo walioibiwa, walioharibiwa mali na biashara zao, kisha na wale ambao wamelala njaa kwa kukosa pesa ya kula

Wapo ambao walikuwa wamefika stendi kutokea mkoani hawa nao moto uliwawakia kwa hapakuwa na usafiri. Barabara zilitawaliwa na doria ya kufa mtu zilizofanywa na polisi.

Nikiacha stori sasa maana kila mtu anastori yake na tutakesha hapa.

Mambo ninayoyaona;

1. Ni kweli bado watu wana hasira. Hilo nimefuatilia kwa kupita huku na huko.
Hizi hasira za hawa watu zinapaswa zitafutiwe suluhu bora yenye kulileta taifa pamoja.

2. Mbinu mpya zitafutwe. Mbinu za nguvu zinaonekana kugonga mwamba. Matumizi ya nguvu yanalundika chuki, hisia za maumivu katika mioyo ya watu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.

3. Kuna haja ya kutafuta maridhiano na suluhu ya kweli hasa inayogusa wananchi wa kawaida ambao wengi ndio walioandamana na kuleta machafuko.
Tusijidanganye kuwa tutawadhibiti siku zote

Kilichotokea wote tunakiri hakijawahi kutokea. Na limekuwa jambo kubwa sana kwetu.

4. Uundwe mkakati wa kuing'oa mbegu ya chuki inayomea baina ya Wananchi wa chini na Watawala ambayo naona inahamia kwa Polisi.

5. Kutunishiana misuli hakutakuwa na mshindi zaidi kila mtu atapoteza hasa taifa letu. Kwani itakuwa kama vita ya gangs ambazo hazinaga mwisho wala hazinaga mshindi.
Hekima na busara na muhimu sana.

6. Hekima na Busara ni zipi sasa?
Kuna njia mbili;
a) Haki itendeke.
Kwamba maovu yaliyofanyika na yaliyopitiliza lazima yalipwe kwa haki.

b) Kusubiri Watu wasahau ikiwa ni wasahaulifu.
Kikawaida watu wasio na haki ni wasahaulifu. Yaani hawana kisasi.
Mbinu ya kupoteza muda na kuwasahaulisha zikitumika tutarudi kama zamani.

Kutenda haki najua ni ngumu hasa kwa watawala wa kibinadamu. Kwamba mtu alikuwa kiongozi leo akanyee debe au afungwe kifungo cha maisha au kuhukumiwa kunyongwa. Kwa kweli ni binadamu wachache wenye nafasi ya mamlaka atakubali kitu kama hicho.

Kwenye biblia Binadamu aliyeweza kujihukumu akiwa na mamlaka tena hukumu ya kuuawa Baada ya kulala na mkwewe ni Yuda mtoto wa YAKOBO.
Na hiyo ndio Legacy kuu ya Yuda mpaka hivi leo na hata Yesu kuitwa Simba wa Yuda.

7. Ni kweli watu wamekufa. Tunafanyaje?
Tuwaache wafe kama panya? Kwa sababu tutasanganya mataifa mengine lakini vipi sisi wenyewe humu ndani tutajidanganya? Tutapuuza?
Hali iliyotokea tutaona ni kawaida?

Jibu ni kuwa sio kawaida.

8. Huu sio muda wa kulaumiana kwamba nani kasababisha haya.
Upande wa serikali unasema waliosababisha haya ni wachochezi wa maandamano, na serikali inasema itachukua hatua kali. Lakini swali linakuja je hiyo ndio suluhu?
Tangu nimeanza kuona waandika mtandaoni wakifuatilia na kukamatwa mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita. Je imesaidia kuzuia kilichotokea. Jibu ni hapana! Zaidi sana imechochea.

9. Waandamanaji wao wanasema serikali na askari wapo responsible n kilichotokea kwa madai kwamba wao walikuwa wanadai haki ya kuzuia uchaguzi kwa kuhitaji reforms. Na kudai haki za waliotekwa na kuuawa.
Lakini bahati mbaya zaidi kwenye maandamano ambayo kwa hakika uhalifu ulitokea wa kuvunja, kuiba na kuchoma vilitokea. Jambo ambalo halikuwa sahihi kufanywa na waandamanaji.
Wakati upande wa pili askari nao wakifanya makosa kwa kutumia nguvu kubwa mpaka kupelekea kuua watu wengi..

10. Ni muhimu viongozi wakuu wa juu wakitoa matamko watao kwa uangalifu mkubwa sana tena ikibidi. Sio lazima wazungumze hasa kama wanajijua wanaweza kuzungumza kauli tata au zenye kuleta hisia za mihemko kwa wasikilizaji.

11. Tatizo la haki ni kuwa inakata yoyote. Watekaji na wauaji wapewe haki zao. Na waliofanya uhalifu kwenye maandamano wapewe haki zao kwa mujibu wa sheria.

12. Sishauri tujifanye kama hakijatokea kitu. Haitakuwa nzuri huko baadaye. Tusipuuze.
Tumeona huu mwanzo ulivyokuwa. Hatujui na haitabiriki huko mbele nini kitatokea.

13. Tusi-bet. Tusitumie mabavu. Tulipofikia sio sehemu ya kutumia mabavu tena.

14. Tunaweza kuwapa wananchi wanachotaka kwa makubaliano ya usalama. Najua ni ngumu lakini ndio njia salama ya kuokoa pande zote mbili.
Hapa kuna mambo kadhaa.
Baadhi ya viongozi wanahofia usalama wao na mali zao iwe walizichuma kihalali au kifisadi.
Wakati wananchi wao wanahitaji katiba mpya itakayowapa wananchi haki sawa hasa kwa upande wa vyama vyote vya siasa kuwa na haki sawa.

15. Maridhiano ya amani yanayohusu kusameheana yanatakiwa yawe ya dhati na kuwe na mabadiliko ya. Kikatiba yatakayozuia matukio ya utekaji na mauaji.
Kiburi kisiwe wala kushiriki katika meza ya mazungumzo kila mmoja afike akiwa na lengo la kutaka amani sio tuu ya utulivu wa nchi bali amani ya Moyo wake.

16. Unajua maandamano ya chuki ya kuhamasisha sijui nyumba ya fulani iko wapi, sijui mali ya fulani iko wapi, ni hatua kamili ya kufikia ugaidi. Kama taifa hatutakiwi kufikia huko. Ugaidi hauondolewi na vitisho.
Ugaidi ni imani iliyokomaa kwa mtu aliyeona hana njia nyingine zaidi ya kujitoa mhanga kufanya uhalifu bila kufuata Sheria za kiungwana.

17. Kilichotokea tumeona. Ule ni uhalifu ambao unadhuru watu wote. Waliomo na wasiokuwemo. Hata hatua ya kukabiliana na ugaidi ni hatari zaidi kwani lazima utajikuta unawapiga hata wasiohusika. Na kuongeza kama sio kupanua maadui.

18. Ninaomba watu washushe mioyo yao. Najua maumivu ya kuonewa yakoje, kudhulumiwa, kutekwa, na kuondokewa na mwenza. Serikali nanyi msikaze shingo mkifikiri kuwa nguvu mnayo. Jishusheni. Meza ya mazungumzo mkae.
Kisha mjadili haki itendekeje bila ubinafsi.

Hofu na mihemko ikiamua haki huleta madhara makubwa sana. Kwani kisasi kinachoendeshwa na mihemko na hofu kinadhuru wahusika na wasiohusika.

Hata hayo mambo ya utekaji ni matokeo ya kile kile kiitwacho hofu.
Sasa njia pekee ya kuondokana na hofu ni kukaa na kuzungumza kwa dhamiri.

Kwa sababu bila kufanya hivyo wote tunajua kuwa tutaumizana sana hata kama wengine wataumia kwa kuchelewa lakini kila mtu atafikiwa na maumivu kwa wakati wake. Ni suala la muda bila kujali ni mkubwa au mdogo. Muonewa au unayeonea.

Kwa sababu ugomvi unatanuka na wahusika wanaongezeka.

Kufikia hapa sina la ziada.
Tulinde nchi yetu.
Tutende Haki.
Tupendane.
Tusikamiane na kuviziana. Hakunaga mshindi kwenye vita za ndugu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Matunda ya kuhubiri amani bila kuihubiri wala kuitenda HAKI
 
Lazima hatua zichukuliwe mkuu. Kujifunza tuu hakutoshi.
Mambo yaliyotokea ilikuwa kukomeshana vilivyo na maumivu yaliyopuuzwa, chuki iliyokosa tiba, hasira zilizokatizwa ndio zillilipuka
Tutatafuta silaha, wametuzidi si kwakuwa walikuwa sahihi, bali ni kwakuwa walikuwa na silaha. Safari hii hatuingii mikono mitupu. Madai yetu ya haki yako wazi. Zimeshatumika njia nyingi sana za kistaarabu kutaka mabadiliko, lakini wanaofaidi cake ya taifa wameweka pamba masikioni.

Kimsingi tulijikwaa wakati wa Magufuli, na sasa tumeangukia kwa huyu mama wa umwagaji damu. Utawala huu ulipoona Magufuli kapora uchaguzi 2020 tukashindwa kuandamana, wakaona inawezekana. Safari hii ikawa muendelezo. Tukiacha hivi vifo bila hatua, anayekuja naye ataua, maana anajua unaweza kuua na kuendelea na uongozi. Kwa sasa ni lazima tuingie kwenye meza ya mazungumzo, kitaingia kila kinachostahili kwenye mifumo ya haki na uchaguzi, na sio mambo kadhaa eti kubalance. Ikiwa hawatakubali tutasaka silaha, tutaipata haki kwa mtutu kama wao wanavyopata madaraka kwa mtutu. Weka hii kwenye record yako.
 
Ipo siku inawezekana hakatokea huko huko au upinzani watu wataenda jela, nachoshangaa polisi sio watu wakujifunza, yupo wapi Abdallah Zombe?
 
Tutatafuta silaha, wametuzidi si kwakuwa walikuwa sahihi, bali ni kwakuwa walikuwa na silaha. Safari hii hatuingii mikono mitupu. Madai yetu ya haki yako wazi. Zimeshatumika njia nyingi sana za kistaarabu kutaka mabadiliko, lakini wanaofaidi cake ya taifa wameweka pamba masikioni.

Kimsingi tulijikwaa wakati wa Magufuli, na sasa tumeangukia kwa huyu mama wa umwagaji damu. Utawala huu ulipoona Magufuli kapora uchaguzi 2020 tukashindwa kuandamana, wakaona inawezekana. Safari hii ikawa muendelezo. Tukiacha hivi vifo bila hatua, anayekuja naye ataua, maana anajua unaweza kuua na kuendelea na uongozi. Kwa sasa ni lazima tuingie kwenye meza ya mazungumzo, kitaingia kila kinachostahili kwenye mifumo ya haki na uchaguzi, na sio mambo kadhaa eti kubalance. Ikiwa hawatakubali tutasaka silaha, tutaipata haki kwa mtutu kama wao wanavyopata madaraka kwa mtutu. Weka hii kwenye record yako.

Kutunishiana misuli kila upande utaumia sana. Na huenda hakuna mshindi
 
..mambo yaliyofanywa na POLISI dhidi ya waandamanaji sio ugaidi?

..matukio ya kuteka na kupoteza wanaharakati sio ugaidi?

..Ni lazima watendaji wa vyombo vya dola, Polisi, Msajili wa vyama, Tume ya uchaguzi, Mahakama, waliotufikisha hapa wawajibike halafu ndio tutafute muafaka.
Huyo ''mwenda na upepo'' unapata muda wapi wa kumjibu? Huyu alindika andiko reeeefu eti ''akichambua'' hakuna mtu atatoka kwa maandamano. Hawa ni wazee wa kukariri. Hivi Tanzania ilivyo na unemployment rate kubwa tena ya vijana wa umri wa miaka 15 mpaka 25, unaweza kupuuza fujo kutokea? Dumb people.
 
Mkuu yote ongea ila ila ipatikane suluhu ya kweli.

Kwanza inapaswa wale wote waliotenda unyama kuanzia utekaji ,kushambuliwa tundu Lisu hadi unyama wa maandamano(tulioshuhudia tunaumia sana) ,mafisadi nk wawajibike kwa matendo yao wakamatwe na kufunguliwa mashtaka na ikowezekana kila mtu apate stahiki yake. Baada ya hapo CCM kama chama ambaye ndio kiini cha tatizo waombe radhi kwa moyo wa dhati na kuondoka virusi vyote kwenye chama chao halafu sasa ndo tukae mezani kama taifa tujenge nyumba moja.

Vinginevyo kusema tupate suluhu bila waliosababisha kuwajibika tunajidanganya na mimi binafsi sipo tayari kushirikiana na madhalimu.
 
Back
Top Bottom