GE2025 Tunatokaje? Huu utakuwa uzi maalum. Mihemko tuweke pembeni. Ila ukweli na suluhu tusiviache

GE2025 Tunatokaje? Huu utakuwa uzi maalum. Mihemko tuweke pembeni. Ila ukweli na suluhu tusiviache

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tuanzie hapa upo upande gani kwanza??
MANGE KIMAMBI NA MARIA SARUNGI WAMEHUSIKA KUHUJUMU MAANDAMANO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kukosa Uongozi wa Kitaalamu na Kimaadili

Watu wenye tabia ya kuropoka au kutumia lugha ya matusi mtaani na mitandaoni mara nyingi hukosa uaminifu wa kijamii.
Wafuasi wanaposhuhudia matusi, kejeli, au hasira zisizodhibitiwa, hamasa hubadilika kuwa utani au hofu.
Kwa mfano:

Mange Kimambi amekuwa akitumia lugha kali dhidi ya watu tofauti, matusi ya nguoni hii imewafanya baadhi ya wafuasi na watu kumwona kama msemaji mwenye hasira na asiye na maadili badala ya kiongozi wa mabadiliko.

Uongozi wa maandamano unahitaji hekima, nidhamu, na heshima ya hoja; si kelele za hasira na matusi.

Kiongozi ambaye anaendana na culture ya jamii husika. Kutumia matusi mitandaoni na kutukana watu bila kujali ni mkubwa au mdogo inapunguza ushawishi wa mtu kwenye mambo ya maana.

2. Kuitisha Maandamano kwa Muda Mrefu (Zaidi ya Miezi Miwili)

Haya ni makosa ya kimkakati. Hili nilieleza kwenye post za nyuma.
Maandamano ni kama moto kwenye nyasi au mabua. ukichelewesha kuwasha, moto unazima kabla hujawasha kiberiti.
Watu hupoteza:
hamasa, imani, na kipaumbele (kwani maisha yao ya kila siku yanahitaji kuendelea). Na vipaombele vinabadilika. Zaidi ya yote unampa adui (ambaye hapa ni serikali) kujipanga namna ya kuyadhibiti.

3. Kukosa Muunganiko na Viongozi wa Ndani (Ground Movement)

Maandamano yenye mafanikio huhitaji muungano wa ndani: vyama, viongozi wa kijamii, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali n.k. Viongozi walioko nje ya nchi, na wanaharakati kama Mange, hukosa:
a) kugusa uhalisia wa hofu za wananchi.
Ukiwa nje ya nchi ukawa kiongozi wa maandamano hasa kwenye nchi kama Tanzania kisaikolojia utaonekana wewe sio mmoja wao. Ila unawasakizia wenzako.
na kuwajibika moja kwa moja iwapo vurugu au hatari ikitokea.
Matokeo yake wananchi wa ndani ya nchi hawaoni uhalisia wa uongozi huo, bali wanaona mtu aliyekimbia nchi anawaambia wapambane yeye akiwa salama.

4. Kuchonganisha Taasisi za Ulinzi (Jeshi na Polisi)

Uongozi wa maandamano unahitaji mkakati wa kisaikolojia na diplomasia. Kusema maneno yanayochonganisha jeshi, polisi, au taasisi za dola ni sawa na:

a) kuamsha tahadhari za usalama,
Hapa ni sawa na kushawishi jeshi liasi na lipindue serikali kwa kudhibiti Polisi. Hivyo serikali lazima ichukue tahadhari kubwa kukabiliana na uchonganishi huo.

b) kupunguza uhalali wa maandamano, Kupindua serikali ikiwa ni sehemu ya agenda za kuandamana kabla hata ya maandamano automatically yanapoteza uhalali.

Hata kama kungekuwa na mpango wa kuipindua serikali haikupaswa usemwe waziwazi hivi. Ingepaswa ifanyike wakati maandamano yanafanyika na yamekolea.
Kutaka kupindua serikali ni kosa la uhaini.

c) Kutoa nafasi ya serikali kutumia nguvu kwa uhalali wa kisheria.
Hivyo, badala ya maandamano kuwa sauti ya umma, yanaonekana kama uchochezi wa kuvuruga amani.

5. Kufeli kwa MANGE zaidi ya mara mbili katika kuhamasisha maandamano. Kwenye siasa na utawala kuna msemo usemao Once a loser, Always a Loser.
Ukikubali kushindwa mara moja kwenye siasa upo kwenye nafasi ya kushindwa daima. Hiyo ni kanuni. Ndio maana kwenye siasa ukiingia lazima uwe na hesabu kali hasa kwenye pigano au pambano la kwanza kwa sababu hilo ndio limebeba msingi wako. Unaweza mtazama Raila Odinga, Edward Lowasa na wengineo.

Mange kimambi tayari anarekodi ya kushindwa kuhamasisha maandamano zaidi ya mara mbili.
Hakupaswa kwenye maandamano haya awe kinara. Yeye angetakiwa atokee pembeni.

Kuongozwa na kiongozi aliyeshindwa kwenye siasa lazima ushindwe tuu. Labda muujiza utokee lakini siasa hazitegemei mara nyingi miujiza.

6. Kukosa Mkakati wa Baada ya Maandamano.

Wengi hushindwa kujibu swali rahisi: “Baada ya maandamano, tunataka nini hasa, na tutafikaje huko?”

Mara nyingi viongozi na wanaharakati wengi wenye kelele zaidi mtandaoni hawana mpango wa kisera, mikakati, bali huongozwa na mihemko na matumaini hewa kwa kujidanganya.

Hivyo, hata kama watu wangetoka barabarani, hakuna hatua za kimfumo za kufuatilia matokeo na kutekeleza mpango wenye tija ili kulinda maslahi na haki za watu wote.

Embu fikiria maandamano yamefanikiwa. Unafikiri nini kitatokea? Ngoja nikudokeze kwa sehemu nini kitatokea
a) Mauaji na visasi kwa viongozi wa serikali.
b) Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwani viongozi nao watakuwa wanajitetea kwa kutumia pesa zao na ikiwezekana kukimbia nchi.
c) uhalifu wa kuiba kwenye mabenki, kuchoma mali za matajiri maarufu waliokuwa wanasapoti mfumo.
d) Wageni na watu jamii ya wahindu na waarabu na machotara watakuwa kwenye wakati mgumu sana. Kwani baadhi ya waandamanaji wana mtazamo kuwa wao ndio wanaiba mali za hii nchi.

e) Kutokuwa na political stability hasa kujua nani anashika nchi kwa muda. Kama ni jeshi nani atashika nafasi hiyo ukizingatia mpaka sasa jeshi lipo upande wa serikali

6. Propaganda zenye kuleta machafuko kati ya Raia na wanajeshi. Kuna propaganda mbili zimetolewa kuhusu majeshi.
a) Majeshi ya Uganda yameingia Tanzania ili kuwapiga watanzania.
b) Majeshi ya Zanzibar yapo bara ili kuwapiga Watanzania.

Propaganda hizo lengo lake ni kuwapiganidha wananchi na wanajeshi. Kwamba wananchi wa Tanzania bara siku ya maandamano ikitokea wamepigwa na polisi au wanajeshi wasishangae kwani hao askari sio watanzania wenzao.

Hivyo wapambane kufa kupona kwani wanatetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya nchi nyingine.

Propaganda hii ingepaswa itolewe siku moja kabla ya maandamano ili kuchochea chuki na hasira ili Lengo la mange kimambi lifikiwe. Lakini halitafikiwa kwa sababu limetolewa wakati ambao sio sahihi ambapo serikali inaweza kuipotosha taarifa hiyo.

Lakini pia kusema kuna wanajeshi kutoka Uganda wamekuja Tanzania ni kulifanya jeshi la nchi liwe macho na kufuatilia kama ni kweli. Kama sio kweli Jeshi hata kama lingekuwa na mpango wa kuunga mkono maandamano mpango huo utafeli.

Kufikia hapo sina la ziada.

Nawatakia Sabato Njema.

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es Salaam

Anafanya kazi ya CCM
 
Huyu Robert Heriel Mtibeli ni content creator. Kila kitu kwake ni fursa anapenda kuandika andika.

Ukisoma mabandiko yake ya nyuma hasa karibia hizi siku za uchafuzi unasoma patterns ni kajamaa kanapenda kuchapisha mabandiko ambayo tunaita contents.

Huwa mabandiko yake marefu nayapuuzaga maana ninayasoma kama content tu za watu wa insta.

Ni kapuuzi sana haka kajamaa.
Kalidhihaki sana harakati ,halafu kanajikuta kana akili za ajabu sanaa.Leo kapuuzi.
 
Kalidhihaki sana harakati ,halafu kanajikuta kana akili za ajabu sanaa.Leo kapuuzi.
Shida inakuja pale mtu anapojiona ana akili a ni mchambuzi mzuri kuzidi wengine.

Watu wapo mbele ya muda na hawapendi kuandika andika. Ukipita kwenye nyuzi za huyu jamaa Kuna muda unaishia kutikisa kichwa kwa kusikitika na kupita kimya kimya.
 
..mambo yaliyofanywa na POLISI dhidi ya waandamanaji sio ugaidi?

Ni ugaidi.
Yaani ulikuwa ugaidi kuzuia ugaidi.
Yaani ugaidi square.

Ni kama pale Gaza.
..matukio ya kuteka na kupoteza wanaharakati sio ugaidi?

Ni ugaidi
..Ni lazima watendaji wa vyombo vya dola, Polisi, Msajili wa vyama, Tume ya uchaguzi, Mahakama, waliotufikisha hapa wawajibike halafu ndio tutafute muafaka.

Swali linakuja,
Kwa hasira watu walizonazo, unafikiri ni rahisi hao watendaji wa vyombo vya dola, polisi, msajili wa vyama na tume, mahakama kukubali kujisalimisha ili wapewe haki yao?

Hapo lazima upande mmoja ukubali kujishusha kisha upande mwingine utake makubaliano ya usalama ili matakwa ya upande uluoonewa upewe mambo wanayoyadai.

Lakini vinginevyo tukubali tuendelee kusokomezana hivihivi mpaka pale wanaofanya uovu waishiwe nguvu.

Swali linakuja, hiyo STAMINA ipo?
 
Mkuu hao aatu wanawajibishwa na nani? Mkuu kweli hujui maelekezo yanavyotolewa? Nani atawagusa hao watu?
Wanastaafishwa na nani ikiwa boss wao yupo pamoja nao?

..Ukitenda kosa na Raisi na ikalazimisha sheria ichukue mkondo wake wewe usiye na kinga utachukuliwa hatua.

..Wawajibishwe na Raisi hata kama aliwapa maagizo kutenda uovu huo.

..Hii nchi ni kubwa kuliko IGP, Mkuu wa usalama, etc.
 
..mambo yaliyofanywa na POLISI dhidi ya waandamanaji sio ugaidi?

Ni ugaidi.
Yaani ulikuwa ugaidi kuzuia ugaidi.
Yaani ugaidi square.

Ni kama pale Gaza.
..matukio ya kuteka na kupoteza wanaharakati sio ugaidi?

Ni ugaidi
..Ni lazima watendaji wa vyombo vya dola, Polisi, Msajili wa vyama, Tume ya uchaguzi, Mahakama, waliotufikisha hapa wawajibike halafu ndio tutafute muafaka.

Swali linakuja,
Kwa hasira watu walizonazo, unafikiri ni rahisi hao watendaji wa vyombo vya dola, polisi, msajili wa vyama na tume, mahakama kukubali kujisalimisha ili wapewe haki yao?

Hapo lazima upande mmoja ukubali kujishusha kisha upande mwingine utake makubaliano ya usalama ili matakwa ya upande uluoonewa upewe mambo wanayoyadai.

Lakini vinginevyo tukubali tuendelee kusokomezana hivihivi mpaka pale wanaofanya uovu waishiwe nguvu.

Swali linakuja, hiyo STAMINA ipo
Wewe si ndio wazazi wako walikuasa usiwatete Watanzania ,imekuwaje tena?!

Walininyang'anya simu.
Lakini yalikuwa maoni yao tuu Mkuu.

Kuna tatizo?
 
Hamjambo wakuu!

Poleni wote kwa yote yaliyotokea. Waliopoteza wapendwa wao, waliopata majereha, waliopoteza mali iwe kwa kuibiwa au kuchomwa moto. Na zaidi Mungu awape pumziko linalowastahili waliopoteza maisha.

Upande wangu mambo yalikuwa magumu sana ukizingatia ninapoishi na karibu kabisa na barabara kuu ya Morogoro road ambapo hekaheka zilikuwa zikiendelea tangu siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho. Risasi, fataki na mabomu ya machozi vilirindima mara kwa mara katika nyumba yetu.

Hakika watoto walipata tabu hasa siku ya kwanza kwani ndio mapambano yalikuwa makali. Moshi wa mabomu ya machozi ulikuwa ukiingia ndani. Usiulize kuhusu vioo kwani unaelewa nini kilitokea.

Umeme ulikatika so siku tatu tangu tarehe 29-31 tulikuwa giza. Watu kadhaa walipigwa risasi nikiwa nashuhudia dirishani. Mmoja kati yao alifariki.

Haya yote nazungumzia ili kuonyesha hatari, matokeo au madhara ya mambo kama haya. Kwamba wapo walioathirika moja kwa moja tangu siku ya kwanza, wapo waliopoteza maisha, wapo walioibiwa, walioharibiwa mali na biashara zao, kisha na wale ambao wamelala njaa kwa kukosa pesa ya kula

Wapo ambao walikuwa wamefika stendi kutokea mkoani hawa nao moto uliwawakia kwa hapakuwa na usafiri. Barabara zilitawaliwa na doria ya kufa mtu zilizofanywa na polisi.

Nikiacha stori sasa maana kila mtu anastori yake na tutakesha hapa.

Mambo ninayoyaona;

1. Ni kweli bado watu wana hasira. Hilo nimefuatilia kwa kupita huku na huko.
Hizi hasira za hawa watu zinapaswa zitafutiwe suluhu bora yenye kulileta taifa pamoja.

2. Mbinu mpya zitafutwe. Mbinu za nguvu zinaonekana kugonga mwamba. Matumizi ya nguvu yanalundika chuki, hisia za maumivu katika mioyo ya watu jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi.

3. Kuna haja ya kutafuta maridhiano na suluhu ya kweli hasa inayogusa wananchi wa kawaida ambao wengi ndio walioandamana na kuleta machafuko.
Tusijidanganye kuwa tutawadhibiti siku zote

Kilichotokea wote tunakiri hakijawahi kutokea. Na limekuwa jambo kubwa sana kwetu.

4. Uundwe mkakati wa kuing'oa mbegu ya chuki inayomea baina ya Wananchi wa chini na Watawala ambayo naona inahamia kwa Polisi.

5. Kutunishiana misuli hakutakuwa na mshindi zaidi kila mtu atapoteza hasa taifa letu. Kwani itakuwa kama vita ya gangs ambazo hazinaga mwisho wala hazinaga mshindi.
Hekima na busara na muhimu sana.

6. Hekima na Busara ni zipi sasa?
Kuna njia mbili;
a) Haki itendeke.
Kwamba maovu yaliyofanyika na yaliyopitiliza lazima yalipwe kwa haki.

b) Kusubiri Watu wasahau ikiwa ni wasahaulifu.
Kikawaida watu wasio na haki ni wasahaulifu. Yaani hawana kisasi.
Mbinu ya kupoteza muda na kuwasahaulisha zikitumika tutarudi kama zamani.

Kutenda haki najua ni ngumu hasa kwa watawala wa kibinadamu. Kwamba mtu alikuwa kiongozi leo akanyee debe au afungwe kifungo cha maisha au kuhukumiwa kunyongwa. Kwa kweli ni binadamu wachache wenye nafasi ya mamlaka atakubali kitu kama hicho.

Kwenye biblia Binadamu aliyeweza kujihukumu akiwa na mamlaka tena hukumu ya kuuawa Baada ya kulala na mkwewe ni Yuda mtoto wa YAKOBO.
Na hiyo ndio Legacy kuu ya Yuda mpaka hivi leo na hata Yesu kuitwa Simba wa Yuda.

7. Ni kweli watu wamekufa. Tunafanyaje?
Tuwaache wafe kama panya? Kwa sababu tutasanganya mataifa mengine lakini vipi sisi wenyewe humu ndani tutajidanganya? Tutapuuza?
Hali iliyotokea tutaona ni kawaida?

Jibu ni kuwa sio kawaida.

8. Huu sio muda wa kulaumiana kwamba nani kasababisha haya.
Upande wa serikali unasema waliosababisha haya ni wachochezi wa maandamano, na serikali inasema itachukua hatua kali. Lakini swali linakuja je hiyo ndio suluhu?
Tangu nimeanza kuona waandika mtandaoni wakifuatilia na kukamatwa mpaka sasa ni zaidi ya miezi sita. Je imesaidia kuzuia kilichotokea. Jibu ni hapana! Zaidi sana imechochea.

9. Waandamanaji wao wanasema serikali na askari wapo responsible n kilichotokea kwa madai kwamba wao walikuwa wanadai haki ya kuzuia uchaguzi kwa kuhitaji reforms. Na kudai haki za waliotekwa na kuuawa.
Lakini bahati mbaya zaidi kwenye maandamano ambayo kwa hakika uhalifu ulitokea wa kuvunja, kuiba na kuchoma vilitokea. Jambo ambalo halikuwa sahihi kufanywa na waandamanaji.
Wakati upande wa pili askari nao wakifanya makosa kwa kutumia nguvu kubwa mpaka kupelekea kuua watu wengi..

10. Ni muhimu viongozi wakuu wa juu wakitoa matamko watao kwa uangalifu mkubwa sana tena ikibidi. Sio lazima wazungumze hasa kama wanajijua wanaweza kuzungumza kauli tata au zenye kuleta hisia za mihemko kwa wasikilizaji.

11. Tatizo la haki ni kuwa inakata yoyote. Watekaji na wauaji wapewe haki zao. Na waliofanya uhalifu kwenye maandamano wapewe haki zao kwa mujibu wa sheria.

12. Sishauri tujifanye kama hakijatokea kitu. Haitakuwa nzuri huko baadaye. Tusipuuze.
Tumeona huu mwanzo ulivyokuwa. Hatujui na haitabiriki huko mbele nini kitatokea.

13. Tusi-bet. Tusitumie mabavu. Tulipofikia sio sehemu ya kutumia mabavu tena.

14. Tunaweza kuwapa wananchi wanachotaka kwa makubaliano ya usalama. Najua ni ngumu lakini ndio njia salama ya kuokoa pande zote mbili.
Hapa kuna mambo kadhaa.
Baadhi ya viongozi wanahofia usalama wao na mali zao iwe walizichuma kihalali au kifisadi.
Wakati wananchi wao wanahitaji katiba mpya itakayowapa wananchi haki sawa hasa kwa upande wa vyama vyote vya siasa kuwa na haki sawa.

15. Maridhiano ya amani yanayohusu kusameheana yanatakiwa yawe ya dhati na kuwe na mabadiliko ya. Kikatiba yatakayozuia matukio ya utekaji na mauaji.
Kiburi kisiwe wala kushiriki katika meza ya mazungumzo kila mmoja afike akiwa na lengo la kutaka amani sio tuu ya utulivu wa nchi bali amani ya Moyo wake.

16. Unajua maandamano ya chuki ya kuhamasisha sijui nyumba ya fulani iko wapi, sijui mali ya fulani iko wapi, ni hatua kamili ya kufikia ugaidi. Kama taifa hatutakiwi kufikia huko. Ugaidi hauondolewi na vitisho.
Ugaidi ni imani iliyokomaa kwa mtu aliyeona hana njia nyingine zaidi ya kujitoa mhanga kufanya uhalifu bila kufuata Sheria za kiungwana.

17. Kilichotokea tumeona. Ule ni uhalifu ambao unadhuru watu wote. Waliomo na wasiokuwemo. Hata hatua ya kukabiliana na ugaidi ni hatari zaidi kwani lazima utajikuta unawapiga hata wasiohusika. Na kuongeza kama sio kupanua maadui.

18. Ninaomba watu washushe mioyo yao. Najua maumivu ya kuonewa yakoje, kudhulumiwa, kutekwa, na kuondokewa na mwenza. Serikali nanyi msikaze shingo mkifikiri kuwa nguvu mnayo. Jishusheni. Meza ya mazungumzo mkae.
Kisha mjadili haki itendekeje bila ubinafsi.

Hofu na mihemko ikiamua haki huleta madhara makubwa sana. Kwani kisasi kinachoendeshwa na mihemko na hofu kinadhuru wahusika na wasiohusika.

Hata hayo mambo ya utekaji ni matokeo ya kile kile kiitwacho hofu.
Sasa njia pekee ya kuondokana na hofu ni kukaa na kuzungumza kwa dhamiri.

Kwa sababu bila kufanya hivyo wote tunajua kuwa tutaumizana sana hata kama wengine wataumia kwa kuchelewa lakini kila mtu atafikiwa na maumivu kwa wakati wake. Ni suala la muda bila kujali ni mkubwa au mdogo. Muonewa au unayeonea.

Kwa sababu ugomvi unatanuka na wahusika wanaongezeka.

Kufikia hapa sina la ziada.
Tulinde nchi yetu.
Tutende Haki.
Tupendane.
Tusikamiane na kuviziana. Hakunaga mshindi kwenye vita za ndugu.


TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Huyu Robert Heriel Mtibeli ni content creator. Kila kitu kwake ni fursa anapenda kuandika andika.

Ukisoma mabandiko yake ya nyuma hasa karibia hizi siku za uchafuzi unasoma patterns ni kajamaa kanapenda kuchapisha mabandiko ambayo tunaita contents.

Huwa mabandiko yake marefu nayapuuzaga maana ninayasoma kama content tu za watu wa insta.

Ni kapuuzi sana haka kajamaa.
Anafanya kazi ya CCM
Huyu ni Kama mange tu. Mange siyo wa kuaminiwa kabisa, Mimi nimepoteza Imani nae kabisa.
Yale madongo ya Raisi yameniuma sana.

Wale wote wenye Roho za kweli za kudai haki TRUST NOBODY BUT YOUR PLAN AND BE PATIENT.
 
Kwa sasa chuki kati ya police na Raia imekuwa kubwa sana, hili linahitaji tiba ya haraka.
Wote waliotekwa wapatikane, kama na kama.waliuawa tuambiwe na waliohusika wawajibishwe.
Wawachie viongozi wakuu wa chadema.
Tuandike katiba mpya, na utaratibu wa uchaguzi ubadilishwe.
Tuhuma zote za kifisadi zichunguzwe na wahusika wapelekwe mahakamani.
 
..mambo yaliyofanywa na POLISI dhidi ya waandamanaji sio ugaidi?

Ni ugaidi.
Yaani ulikuwa ugaidi kuzuia ugaidi.
Yaani ugaidi square.

Ni kama pale Gaza.
..matukio ya kuteka na kupoteza wanaharakati sio ugaidi?

Ni ugaidi
..Ni lazima watendaji wa vyombo vya dola, Polisi, Msajili wa vyama, Tume ya uchaguzi, Mahakama, waliotufikisha hapa wawajibike halafu ndio tutafute muafaka.

Swali linakuja,
Kwa hasira watu walizonazo, unafikiri ni rahisi hao watendaji wa vyombo vya dola, polisi, msajili wa vyama na tume, mahakama kukubali kujisalimisha ili wapewe haki yao?

Hapo lazima upande mmoja ukubali kujishusha kisha upande mwingine utake makubaliano ya usalama ili matakwa ya upande uluoonewa upewe mambo wanayoyadai.

Lakini vinginevyo tukubali tuendelee kusokomezana hivihivi mpaka pale wanaofanya uovu waishiwe nguvu.

Swali linakuja, hiyo STAMINA ipo
Wewe si ndio wazazi wako walikuasa usiwatete Watanzania ,imekuwaje tena?!

Walininyang'anya simu.
Lakini yalikuwa maoni yao tuu Mkuu.

Kuna tatizo
Ulisema hakuna wa kuandamana, haya unaandika sasa yanatoka wapi??

Nilisema kwa sababu mimi nakaa barabarani. Mpaka kufikia saa nne kulikuwa na utulivu wa kutosha. Ndipo nikaandika kile nilichoandika.
Lakini kufikia saa nne unusu mambo yalibadilika kwa ghafla sana hasa maeneo ya Kimara. Hakuna yoyote aliyefikiria tungefika kiwango hiki.
 
Ni ugaidi.
Yaani ulikuwa ugaidi kuzuia ugaidi.
Yaani ugaidi square.

Ni kama pale Gaza.


Ni ugaidi


Swali linakuja,
Kwa hasira watu walizonazo, unafikiri ni rahisi hao watendaji wa vyombo vya dola, polisi, msajili wa vyama na tume, mahakama kukubali kujisalimisha ili wapewe haki yao?

Hapo lazima upande mmoja ukubali kujishusha kisha upande mwingine utake makubaliano ya usalama ili matakwa ya upande uluoonewa upewe mambo wanayoyadai.

Lakini vinginevyo tukubali tuendelee kusokomezana hivihivi mpaka pale wanaofanya uovu waishiwe nguvu.

Swali linakuja, hiyo STAMINA ipo?

..Mbona wakati wa Mwalimu Nyerere aliwatimua wakina Siyovelwa, Kisumo, Mzena, na wenzao.

..Tutakuwa tunatoa mfano gani kwa Ma-Igp, Wakurugenzi wa Usalama,...wanaofuatia ikiwa hawa hawatachukuliwa hatua?
 
Miaka inavyokwenda naona sura zile zile...

Viongozi wale wale tokea wakati nipo shule. mpaka sasa...

Usicheze na siasa, siasa ni mchezo mchafu...

Wanataka umaarufu...

Wanasiasa wabongo wengi waongo...

Mmmh! Hii verse au ndio maoni unatoa mkuu?

Wabongo wengi sio waaminifu hasa waliojiingiza na siasa. Wengi wanawatumia watu wa chini vibaya.
Leo anasema hiki kesho anasema kile.
Leo yupo huku kesho yupo kule
 
Hili swali nalijibu kila siku. Mimi nipo upande wa Haki.
Kila mtu anatafuta haki si ndio?
Swali linakuja nani anaamua hii ni haki na hii sio haki?

Hapo ndipo watibeli tunapoingia. Hatupo kumuonea mtu wala kumpendelea mtu.

Unataka nimuonee mtu au nimpendelee mtu?
Tunahitaji katiba mpya ambayo inahakikisha nguvu ya rahisi ina punguzwa

Pillar za government ziwe independent.
Judiciary, parliament na executive ziwe separate

Nyerere ametuponza Sana. Katiba imetengenezwa raisi awe mungu
 
Kwa iyo ulivoshuhudia kwa kuchungulia dirishani ndo unajiona shujaa?Maku wewe

Kwani ilikuwa mashindano ya ushujaa?

Ninapokuambia nimeshuhudia maandamano elewa nimeshuhudia maandamano kuanzia Kimara, ubungo, Manzese, Magomeni, Buguruni. So hakuna utakachonidanganya.

Sasa ukiulizwa kilichokufanya utukane ni nini utajibu nini? Au ndio hasira za kijinga?
 
Tunahitaji katiba mpya ambayo inahakikisha nguvu ya rahisi ina punguzwa

Pillar za government ziwe independent.
Judiciary, parliament na executive ziwe separate

Nyerere ametuponza Sana. Katiba imetengenezwa raisi awe mungu

Tulipofikia ni pagumu sana kwa sababu chuki ikikomaa huleta machafuko.
Waliopo madarakani wenyewe wanahofu kuwa wakisikiliza madai ya wananchi kisha wakaachia madaraka watu watalipa kisasi. Jambo ambalo ni hakika wala sio uongo
 
Plan zozote zile kama lengo ni kutunishiana misuli hakunaga mshindi hapo nakuambia.

Kila mtu atataka afanye kumkomoa mwingine. Na binadamu akiamua lake kumzuia ni ngumu yaani huwezi kupambana naye. Ni suala la muda tuu.

Ulikuwepo field lakini mkuu? Hasa kwenye statement yako ya mwisho?
Sio kuwapo tu, bali nime shuhudia udhalimu wa hali ya juu sana.
 
..Ukitenda kosa na Raisi na ikalazimisha sheria ichukue mkondo wake wewe usiye na kinga utachukuliwa hatua.

..Wawajibishwe na Raisi hata kama aliwapa maagizo kutenda uovu huo.

..Hii nchi ni kubwa kuliko IGP, Mkuu wa usalama, etc.
Mkuu wawajibishwe na Raisi?
Mkuu naona huelewi kuwa hata mambo yanaenda vipi.
 
Back
Top Bottom