Kazi ya udalali inafanywa na watu ambao hawana elimu na wanafanya kama sehemu ya kujiingizia kipato na sio watoa huduma ndio maana hata ukikutana nao mnapozungumza unaona kabisa yeye anakazania kupata faida na sio kukuhangaikia wewe kupata huduma au bidhaa bora.
Mfano kwenye biashara ya nyumba za kupangisha. Dalali anaweza kukuzungusha siku nzima ili apate posho yake ya kukuzungusha ila sio kukupatia mazingira mazuri ya nyumba ya kuishi unayoitaka.