Exile
JF-Expert Member
- Feb 21, 2021
- 1,477
- 3,642
Wanaendelea kupotosha kwamba mkataba huu hauna ukumo, sio kweli! Mkataba huu una ukomo; ibara ya 23 ibara ndogo ya 1 inasema wazi ukomo wa mkataba huu; itakapotokea moja katika haya mambo mawili, kule kwenye mradi wa utekelezaji (ambao haujaanza) mradi ukaisha basi na mkataba huu utakuwa umefika mwisho lakini ikitokea ile mikataba mingine miwili ikisainiwa (HGA na mkataba wa mradi) na utekelezaji wake umeisha basi mkataba huu utakuwa umefika ukomo.