Wanabodi,
Kwenye hii IGA, hoja za Prof. Shivji zina mashiko, kuwa mkataba umeegemea upande mmoja, serikali yetu ndio yenye wajibu, na sio DPW!. Tumeingia makubaliano na Dubai, ambayo sio sovereign, kukitokea mgogoro wa kushitaki kimataifa, Tanzania tunaweza kushitakiwa kwa international instruments, kwasababu Tanzania ni member wa Geneva Convention, Vienna Convention of the law of treaties lakini Dubai sio member, haipo kwasababu Dubai sio nchi. Kama DPW ndio watatukosea, Tanzania tutawashitaki wapi wakati Dubai sio member wa Geneva Convention, sio signatories wa international treaties?!. Member kule ni UAE!. Kwenye ile IGA, hakuna popote UAE, imetoa Power of Attorney kwa Dubai!, hivyo Tanzania kama nchi, tumeingia mkataba na an entity which has no capacity to contract an international treaty!. DPW wangesainiana tuu na TPA na kumalizana juu kwa juu!.