Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Tangu nimsikie Mbwana Samatta katika jukwaa la kimataifa sijamsikia tena mzawa mwingine Mtanzania akiwa maarufu hapa Africa au duniani kwa ujumla katika sekta ya michezo.
Huenda sababu mojawapo kubwa ni serikali na raia kuelekeza nguvu zao na focus yao yote katika vilabu viwili zaidi vya Kariakoo vya Simba na Yanga. Sasa ukiangalia kwa sasa wanaowika zaidi katika hivi vilabu kwa sasa karibia wote ni wageni kutoka nje. Wazawa wamepoteana kabisa wamebaki kuwa wasindikizaji tu.
Tanzania ni kubwa sana, haiawezekani watu wote wenye vipaji wakapata nafasi ya kucheza katika vilabu viwili vya Kariakoo vya Simba na Yanga. Ni vyema serikali na wadau wakahakikisha angalau kila kanda inakuwa na timu imara za michezo au kutoa kipaumbele kwa michezo mingine kama riadha, rugby, tennis, golf n.k kama nchi nyingine majirani zetu walivyofanya na kuwapa wazawa wa nchi zao fursa kubwa zaidi ya michezo.