Tunawashukuru sana Marekani kwa kukikata meno kikosi cha Wasiojulikana!

Tunawashukuru sana Marekani kwa kukikata meno kikosi cha Wasiojulikana!

Ndipo Marekani wakaamua kuingilia na kuwaokoa watanzania walioendelea kuwa wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana. Wakatuma ujumbe. Wakatoa onyo.
Kama walifanya hivi wanastahiri pongezi na shukrani.

Ni dhahiri kwamba ni lazima palikuwepo na msukumo toka sehemu fulani kuhusu haya mambo.

Hiyo sehemu iliyotoa tahadhari inaweza ikawa ni toka humu humu ndani au nje.
 
Wasiojulikana wana umuhimu wake hata marekani wapo

Wanasawazisha wasaliti wa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasiojulikana ni mafala Tu mbona sikuhizi wamepoa Ile mipango Yao ya kishamba IPO ya kutekana iko uchi duniani kote wanajua aliyekuwa nyuma Yao....
Kama wao ni wajanja waambie watuteke tena alafu utaona jinsi watanzania watakapoanza Kula nyasi
 
Watu wamejifunza kutumia lugha za staha. Maana bila action baadhi yenu hamuelewi.Huwezi kukosoa kwa matusi eti kisa unatumika.
Kumbe ndio chanzo cha kuua,kupoteza na kuteka? Basi huyu aliewaita watu mashetani na mwingine anawaita corona asubuli muda wowote mtamteka.
 
Kumbe ndio chanzo cha kuua,kupoteza na kuteka? Basi huyu aliewaita watu mashetani na mwingine anawaita corona asubuli muda wowote mtamteka.
Mtamteka? Na akina nani? Nchi hii inafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi acha kubwabwaja.
 
Hawalali kwa kijitolea au hawalali kwakuwa kazi wanayolipwa nayo mshahara ndio inavyotaka? Unaongeza kama vile hawalali kwakuwa wanampenda sana na hii nchi na sio mshahara.
Hii kazi wanaifanya kwa uzalendo na kuipenda nchi yao. Sio mshahara hata kidogo.
 
Who killed JFK??
An individual that was not happy with JFK as President. So what are you suggesting, we emulate that when we are not happy with our president? We are not that satanic like that individual or some people in this country, and we will never kill because we dont like a political figure. Sorry.
 
Wamarekani ni watu fulani wanafiki tu, tusiwaogope sana na kuwapapatikia kupita kiasi.

Wakati wa furaha wamarekani wanajifanya marafiki wa karibu wa nchi za ulaya ikiwemo Italia.

Limekuja balaa la corona husikii wamarekani wakisikitishwa na vifo vya Italy. Cuba ambayo ni nchi iliyowekeza kwenye masuala ya tiba ndio madaktari wake wanakwenda kusaidia uokoaji Italy.
 
HUwezi kulinganisha suala la mauaji ya kisiasa na janga la kitu kama Coronavirus. Adjust your thinking.
 
Marekani walijua kabisa kwamba kulikuwa na kikosi kilichobatizwa jina la "Wasiojulikana" hapa nchini, kikosi ambacho kilijikita katika kuteka watu na hata kuua. Na Marekani waliona wazi kwamba wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana walikuwa ni kutoka vyama vya upinzani pamoja na waandishi na wananchi kwa ujumla walioikosoa serikali. Pia kulikuwa na wafanya biashara wakubwa ambao walionekana kutenda kinyume na matakwa ya serikali,

Na jambo jingine Marekani waliloona wazi ni kwamba siku zote Polisi hawakuonyesha nia ya dhati ya kushughulikia na kupepeleza kesi au matukio yaliyofanywa na hiki kikosi cha Wasiojulikana. Mara nyingone Polisi walitoa matamko ya kuwalaghai na kuwapoteza lengo wananchi pale ilipohusu matukio ya Wasiojulikana.

Ndipo Marekani wakaamua kuingilia na kuwaokoa watanzania walioendelea kuwa wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana. Wakatuma ujumbe. Wakatoa onyo.

Tunawashukuru sana Marekani kwa jambo hili. Ni wazi kuingilia kwenu kumeokoa maisha ya Watanzania wengi na kutoa ahueni kubwa. Tunajua watu wegi walikuwa kwenye "hit list" ya hiki kikosi cha Wasiojulikana na kama sio kuingilia kwenu wengi wangeumizwa au kutoweshwa. Lakini bado tunaomba mwende mbali zaidi na kufunua wazi nani waliohusika na kikosi cha Wasiojulikana, na kiliundwa kwa amri ya nani. Damu za waliopota zinatulilia tuwafanyie hilo.
Kweli kabisa maana hao ndiyo walikuwa corona yetu
 
Watu wamejifunza kutumia lugha za staha. Maana bila action baadhi yenu hamuelewi.Huwezi kukosoa kwa matusi eti kisa unatumika.
HIyo ni sehemu ya siasa. Umeona kwa mfano Marekani Democrats na Republicans wanavyoshambuliana kwa maneno? Na jirani hapa Afrika Kusini? Ulishaona kila Malema wanavyowapasha ANC na hata raisi? Je CCM mara ngapi wanatumia maneno ya kejeli kwa kuwa ni siasa? Juzi hapaolepole kaita wapinzani corovavirus.

Sasa kwa nini kwenye mipasho ya kisiasa chama tawala kikipashwa watu watekwe au kuuwawa? Mkuki kwa nguruwe?

Ukishakuwa mwanasiasa, kubali mipasho na kukosoana. Ndivyo mchezo wa siasa unavyochezwa. Yaani leo hii ndani ya CCM iwe sawa kuwaita mawaziri wajinga na wapumbavu, lakini siku ukisema Raisi ni dikteta uchwara basi hukumu yako ni kifo kwa SMG?
 
Kwahiyo watu wa night club nao wanafanya kazi zao kwa kuipenda nchi na sio mshahara? Hivi unaona unaongea na watoto ama?
Siwezi jibu swali ambalo sijalielewa. Unamaanisha wahudumu wa night club au?
 
Back
Top Bottom