Tunawashukuru sana Marekani kwa kukikata meno kikosi cha Wasiojulikana!

Tunawashukuru sana Marekani kwa kukikata meno kikosi cha Wasiojulikana!

Mulaga akasema anaenda kupumzisha akili wakati akili zenyewe hana.
Kwa hili hilo li "Pompeo" limewafyata mkia barabara. Hamna hata fyoo. kujibu. Halafu kama hujagundua, hadi wakuu wamekuwa wapole siku hizi.

Cha kucheesha ni kwamba siku hizi serikali inakimbia kujieleza kwa Marekani hata kabla hawajaulizwa! Unacheza na Pompeo wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIyo ni sehemu ya siasa. Umeona kwa mfano Marekani Democrats na Republicans wanavyoshambuliana kwa maneno? Na jirani hapa Afrika Kusini? Ulishaona kila Malema wanavyowapasha ANC na hata raisi? Je CCM mara ngapi wanatumia maneno ya kejeli kwa kuwa ni siasa? Juzi hapaolepole kaita wapinzani corovavirus.

Sasa kwa nini kwenye mipasho ya kisiasa chama tawala kikipashwa watu watekwe au kuuwawa? Mkuki kwa nguruwe?

Ukishakuwa mwanasiasa, kubali mipasho na kukosoana. Ndivyo mchezo wa siasa unavyochezwa. Yaani leo hii ndani ya CCM iwe sawa kuwaita mawaziri wajinga na wapumbavu, lakini siku ukisema Raisi ni dikteta uchwara basi hukumu yako ni kifo kwa SMG?
Nani alishakosoa kwa lugha nzuri hata kama ni mipasho akauliwa?
 
HUwezi kulinganisha suala la mauaji ya kisiasa na janga la kitu kama Coronavirus. Adjust your thinking.
My thinking doesn't need no adjustment, hao wamarekani ni watu wa kutazama uhalali wa maslahi yao. Mauaji ya kisiasa duniani msingi wake ni CIA, walimuua Lumumba kwa maslahi ya Belgium na ya kwao pia.

Wameuua wanasiasa wengi amerika ya kusini kwa maslahi yao ya kibepari. Hawana uhalali wa kimaadili wa kuongelea mauaji ya ndani ya nchi moja tu ya afrika.
 
Mtamteka? Na akina nani? Nchi hii inafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi acha kubwabwaja.
Unanijua Katiba au unajua jina tu la Katiba?
Hivi mkuu ni sheria ipi ilimpa haki Makonda kuvamia Clouds Media au Tundu Lissu kupigwa risasi?
MUNGU IBARIKI USA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI POMPEO
 
Wamarekani ni watu fulani wanafiki tu, tusiwaogope sana na kuwapapatikia kupita kiasi.

Wakati wa furaha wamarekani wanajifanya marafiki wa karibu wa nchi za ulaya ikiwemo Italia.

Limekuja balaa la corona husikii wamarekani wakisikitishwa na vifo vya Italy. Cuba ambayo ni nchi iliyowekeza kwenye masuala ya tiba ndio madaktari wake wanakwenda kusaidia uokoaji Italy.

Tunajua wamarekani ni wanafiki, ila hatujali hilo, ili mradi wanatetea watu wanaokandamizwa na walevi wa madaraka hapa nchini tunawaunga mkono. Bora kujipendekeza kwa mmarekani mnafiki kuliko kiongozi wetu mkatili.
 
Nani alishakosoa kwa lugha nzuri hata kama ni mipasho akauliwa?
Kulinganisha wapinzani na corona ni lugha nzuri? Kusema Zitto auwawe ni lugha nzuri? Hebu nambie ni extreme zipi zisizovumilika katika lugha ambazo wapinzani walitoa hadi kuhukumiwa kifo? Yale anayosema Tundu Lissu? Yale aliyosema Ben Saanane humu JF?

Au tukukumbushe lugha za Wabunge dhidi ya wapinzani Bungeni ambazo wabunge wa chama tawala wanakenulia meno na spika hakemei? Huo ndio ustaarabu wainzani wanakosa?
 
Unanijua Katiba au unajua jina tu la Katiba?
Hivi mkuu ni sheria ipi ilimpa haki Makonda kuvamia Clouds Media au Tundu Lissu kupigwa risasi?
MUNGU IBARIKI USA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI POMPEO
Jinai haina mwisho,ipo siku hao waliompiga Tl risasi dola itawapata. Lakini hata huko Usa askari wanapiga raia weusi risasi na maandamano kila mara kulaani haya matukio. Kwa hiyo Pompeo haoni hayo?
 
Tunajua wamarekani ni wanafiki, ila hatujali hilo, ili mradi wanatetea watu wanaokandamizwa na walevi wa madaraka hapa nchini tunawaunga mkono. Bora kujipendekeza kwa mmarekani mnafiki kuliko kiongozi wetu mkatili.
HUyo huyo mnafiki unayemjua wewe hawezi kuwa na hizo sifa nyingine ulizozitaja, huo unafiki peke yake unapingana na hizo sifa nyingine ulizompa mmarekani.
 
Mtamteka? Na akina nani? Nchi hii inafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi acha kubwabwaja.

Tuna uwezo wa kutambua sheria na katiba zinapofanya kazi, na matumizi mabaya ya madaraka. Hilo kundi la watu wasiojulikana linapewa nguvu na viongozi wanaotumia vibaya madaraka fullstop.
 
My thinking doesn't need no adjustment, hao wamarekani ni watu wa kutazama uhalali wa maslahi yao. Mauaji ya kisiasa duniani msingi wake ni CIA, walimuua Lumumba kwa maslahi ya Belgium na ya kwao pia.

Wameuua wanasiasa wengi amerika ya kusini kwa maslahi yao ya kibepari. Hawana uhalali wa kimaadili wa kuongelea mauaji ya ndani ya nchi moja tu ya afrika.
You still need to adjust your thinking. Wajerumani kwa kuwa waliwaua Wayahudi basi leo hii tuamue Wajerumani si watu wazuri?
 
Wape ndukum sasa
Marekani walijua kabisa kwamba kulikuwa na kikosi kilichobatizwa jina la "Wasiojulikana" hapa nchini, kikosi ambacho kilijikita katika kuteka watu na hata kuua. Na Marekani waliona wazi kwamba wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana walikuwa ni kutoka vyama vya upinzani pamoja na waandishi na wananchi kwa ujumla walioikosoa serikali. Pia kulikuwa na wafanya biashara wakubwa ambao walionekana kutenda kinyume na matakwa ya serikali,

Na jambo jingine Marekani waliloona wazi ni kwamba siku zote Polisi hawakuonyesha nia ya dhati ya kushughulikia na kupepeleza kesi au matukio yaliyofanywa na hiki kikosi cha Wasiojulikana. Mara nyingone Polisi walitoa matamko ya kuwalaghai na kuwapoteza lengo wananchi pale ilipohusu matukio ya Wasiojulikana.

Ndipo Marekani wakaamua kuingilia na kuwaokoa watanzania walioendelea kuwa wahanga wa kikosi hiki cha Wasiojulikana. Wakatuma ujumbe. Wakatoa onyo.

Tunawashukuru sana Marekani kwa jambo hili. Ni wazi kuingilia kwenu kumeokoa maisha ya Watanzania wengi na kutoa ahueni kubwa. Tunajua watu wegi walikuwa kwenye "hit list" ya hiki kikosi cha Wasiojulikana na kama sio kuingilia kwenu wengi wangeumizwa au kutoweshwa. Lakini bado tunaomba mwende mbali zaidi na kufunua wazi nani waliohusika na kikosi cha Wasiojulikana, na kiliundwa kwa amri ya nani. Damu za waliopota zinatulilia tuwafanyie hilo.
 
Back
Top Bottom