Jambo moja ambalo linanisikitisha sana ni kwamba viongozi wakuu wastaafu walielewa nini kilikuwa kinatokea, lakini waliamua kukaaa kimya wakiona kila tunda na msimu wake. Huo ulikuwa ni usaliti mkubwa sana kwa Watanzania, na wao pia wanastahili kila aina ya lawama. Walikuwa na uwezo wa kukutana pamoja na kuamuru jambo hili likomeshwe mara moja.
Lakini pia, watu kama Membe, ambaye amesema wazi kwamba ana source zake zinamjulisha kila kitu, ni wazi sana walijua kinachoendelea. Je hawakuwa na uwezo wa kuingilia kati, hata kama ni kwa njia ya ki-covert? Labda juu ya Membe tusiseme mengi, lakini yeyote atakaepata fursa kuongea na Membe amuulize hili suala - je, hukujua kilichokuwa kinaendelea, na kama ulijua ulifanya nini?