Kiongozi, ili kujua nabii wa uongo hakikisha unafanya ya fuatavyo
1. Muamini Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wa maisha yako, (iwapo bado.. Ila naamini tayari ushaokoka)
2.Ujazwa na Nguvu ya Roho Mtakatifu(kama bado, maana huyu ndio anaetuongoza ktk kujua Yesu Kristo kwa sahihi na ndio mtenda miujiza halisi)
3. Soma neno la Mungu kwa kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu, hapa ndio utaweza kupata maarifa ya kutambua Roho anafanya kazi ndani ya nabii yoyote, maana nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yako atakukumbusha neno la Mungu lililo sahihi kwa kila neno atalohubiri Nabii(nguvu ya kupambanua Roho).
4.kabla huja enda ibada yeyote, ya nabii au mchungaji yeyote, ombea ibada hiyo na Muombe Mungu akuongoze kwa kukupa Amani kama ni Sawa kupeleka roho yako pale.. Maana Neno la Mungu lina Sema Na Amani ya Kristo iamue ndani yetu, popote ambapo sio Roho wa Kristo anahudumu lazima Ukose Amani kushiriki ibada. Msijipeleke tu kwasababu wameweka ma tangazo ya kimataifa, Paulo anasema, Linda Sana Moyo wako kuliko vyote ulindavyo, maana ukipeleka Roho yako ikaharibiwa umepoteza vyote. 🙏