Tunaweka rekodi sawa, Hayati Magufuli alikuta ukusanyaji mapato upo chini akakusanya na kuyatumia vyema. Je sasa? Voyages

Tunaweka rekodi sawa, Hayati Magufuli alikuta ukusanyaji mapato upo chini akakusanya na kuyatumia vyema. Je sasa? Voyages

Inasikitisha sana kwa nini watu wanakuwa na tafsiri tofauti juu ya mtu kuzungumzia ukweli wa suala husika. Lakini mtu anakuwa na povu ambalo halihusiki kabisa.

Nani asiyejua kuwa hayati JPM ndio alianzisha mfumo kuwa mapato yote ya serikali yawe centralized na pesa zote ziingie hazina. Huko nyuma ilikuwa ni upigaji tu. Pesa nyingi zilipotea mikononi mwa wajanja wachache.

Alipoingia madarakani tu pesa nyingi akakukusanya na zikatumika bila kificho kwa manufaa ya umma. Mapato ya serikali yakapanda kutoka bil 700 mpaka tril 1.7 kwa mwezi.

Leo hii baada ya mapato kupanda pesa za umma zinafanyiwa anasa kwa safari za ughaibuni zisizokwishwa.

Wapuuzi wachache na wajinga sana wakisikia tunasema kweli wanaleta kebehi za kipuuzi.
wapuuzi sana hao wanaokuletea kebehi!chuma JPM kilifanya kazi kubwa pamoja na mapungufu yake makubwa ya kubana demokrasia ambayo hata mimi nilimchukia katika hilo!ila katika kupiga kazi hakika chuma alitutendea haki sana katika sekta hyo!ila tu uminywaji wa demokrasia ndo doa kubwa sana aliloacha!
 
Kwa kifupi kabisa, ni kwamba, Nchi ipo mikononi mwa MBWA MWITU wasio na huruma hata kidogo.
Nchi haiwezi kujengwa kwa kusafiri kila uchao kwenda Ughaibuni.
 
..alikuwa haambiliki.

..alijiona anajua kuliko kila mtu.

..matokeo yake ni maamuzi mabaya yanayolitia taifa hasara.

Una mfano wa Rais gani ambaye ana record nzuri ya kushaurika na alifanya vizuri wakati wa utawala wake hapa nchini?

Jaribu kuwaelewa vizuri washauri wa viongozi wetu. Wote wanasukumwa na personal interests zao.

Wapo ambao ni chawa. Hawa approach yao ni kumsoma kiongozi anataka nini na kumshauri hivyo hivyo anavyotaka. Baada ya hapo wataulinda huo uamuzi kwa gharama yoyote, kwasababu huyo kiongozi ndiyo mtaji wao.

Wale ambao sio chawa nao wana personal interests zao ambazo hawataki ziumizwe na uamuzi fulani wa kiongozi. Kwa hiyo, hawa watatoa ushauri ambao hata ukikubaliwa na kiongozi unaweza usiwe na manufaa yoyote kwa nchi. Watakaonufaika ni hao waliompotosha kiongozi ili kulinda au kuboresha maslahi yao binafsi.

Katika mazingira kama haya, winner ni yule kiongozi ambaye ana good judgment, with or without advice from anyone. Yule ambaye washauri ndiyo everything, hana cha maana anachoweza kukifanya kwenye nchi hii ya washauri wanaosukumwa na personal interests zao!
 
..alitumia fedha alizokusanya vibaya.

..mfano mmoja ni manunuzi ya midege inayotutia hasara kila mwaka.

..au kutumia fedha zetu kujenga mji mkuu dodoma halafu anakwenda kukopa WB kwa ajili ya elimu.
Ndege hazina usimamizi mzuri ndio maana zinaonekana zinaleta hasara.
 
Mwendazake alikuta mapato bil.825 hadi anakufa ilikuwa bilion 1500 ambayo ni sawa na ongezeko la bil.675 kwa miaka 5 sawa na ongezeko la mapato la bilion 135 kila mwaka..

Rais Samia amefikisha bilion 1800 kutoka bil.1500 sawa na ongezeko la Bil.300 kwa mwaka mmja..

Alienda kwa trend hii inamaana hadi 2025 atakuwa kaongeza bil. 1200 kwa miaka 4 hivyo kuzidi kufunika legacy uchwara.👇
Hizo hela si ndio wanazotukwapulia kwenye simu na benki kwa jina la "TOZO"?

Hamna miujiza humo kabisa na tena awamu hii uongo wa kumsifia bibi tozo utakuwa maradufu
maana amebariki wezi. Kama hela nyingi anakusanya tozo ni za nini sasa?
 
Hizo hela si ndio wanazotukwapulia kwenye simu na benki kwa jina la "TOZO"?

Hamna miujiza humo kabisa na tena awamu hii uongo wa kumsifia bibi tozo utakuwa maradufu.
Lipa tozo acha blaa blaa..Wakati nyie mnakwapua kwenye accounts za Wafanyabiashara na vitambulisho feki vya machinga mbona hukuropoka?

Hukwapuliwi bali unakatwa Kodi..
 
..alitumia fedha alizokusanya vibaya.

..mfano mmoja ni manunuzi ya midege inayotutia hasara kila mwaka.

..au kutumia fedha zetu kujenga mji mkuu dodoma halafu anakwenda kukopa WB kwa ajili ya elimu.

Inasikitisha sana,,,,kuna vijiji miaka 60 ya uhuru maji shida unaenda kununua mindege isiyokua na faida baada ya kumaliza tatizo la maji kwanza,,,yan sisi hatuna vipaumbele kabisa!
 
Inasikitisha sana,,,,kuna vijiji miaka 60 ya uhuru maji shida unaenda kununua mindege isiyokua na faida baada ya kumaliza tatizo la maji kwanza,,,yan sisi hatuna vipaumbele kabisa!
Hata Yesu na Muhammad katika nchi zao wapo waliowapinga na waliowakubali japo walitumwa na Mungu hiyo ndio hulka ya binadamu Sasa JPM ni nani hata akubalike na Kila mtu

Mbona haukusema kuwa Kuna vijiji tokea tupate uhuru havikuwahi kuwa na umeme lakini JPM alipeleka umeme
 
Sawa kijana kamfufue... Naimani TZ itakuwa nchi ya viazi zaidi chini ya katiba hii.
Wewe ni sehemu ya wapuuzi na ungekuwa kiungo cha mwili wala sio siri unafaa luwa nyama ya Tako.
 
..alitumia fedha alizokusanya vibaya.

..mfano mmoja ni manunuzi ya midege inayotutia hasara kila mwaka.

..au kutumia fedha zetu kujenga mji mkuu dodoma halafu anakwenda kukopa WB kwa ajili ya elimu.
Wewe unaeongea hivi..hizoo ndege zilikutia hasara je uliacha kula? Kuvaa?, matibabu? Hivi vyote hukupata? Jee hizo ndege umewahi kuzichangia hata kwa kupanda kuzungukia mikoani au unaongea kwasababu ni propaganda? Je unajua hata hao waingereza na wamarekani,kina uchina huko hawamiliki mashirika yao binafsi ya ndege bali wanaingia ubia na mikataba ya kufanya kazi. Amka kifikra mtanzania cha kwenu ni kwenu tuu usitake kujifananisha na ugenini
 
..alikuwa haambiliki.

..alijiona anajua kuliko kila mtu.

..matokeo yake ni maamuzi mabaya yanayolitia taifa hasara.
Alionesha uthubutu wa serikali yake pia maamuzi yake yalikuwa imara leo hii ATCL ipo inafanya kazi ila wachache kama nyie hamtaki kuikubali nchi yenu...
 
..kununua midege isiyohitajika na kuishia kuliingizia taifa hasara.

..kuelekeza fedha nyingi ktk ujenzi wa mji mkuu Dodoma, wakati nchi tayari inao mji mkuu, na ina mahitaji mengine muhimu.

..ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake ambako hukana abiria wa ndege. Kulazimisha Tanapa ijenge hoteli ya kitalii kijijini kwake.
Toa evidence kuwa tanapa ililazimishwa kujenga hoteli ya kifahari chato. Uwanja wa ndege sio swala la kuongelea kabisa tena kaa kimya. Ilipaswa hadi kufikia sasa nchi yetu kuwa na viwanja vya ndege vya kimataifa ktk kila mkoa uliopewa hadhi ya jiji.. magufuli qlifanya jitihada zake binafsi kuhakikisha wananchi wanaoana fursa ktk taifa lao. Huko chato hujawai kufika huwezi ukajua au ukaona fursa zilizopo kwao ndio maana alisema watanzania tutumieni fursa zinatolewa na serikali kuukwepa umasikini...alituambia tutembee vifua mbele Tanzania ni tajiri...unatokwa povu kisa uwanja chato mbona huongelei mambo ya tozo kuwa juu na ugumu wa maisha kukithiri mawaziri kuwa na kauli za kibabe kwa wananchi wanapopewa ushauri
 
Inasikitisha sana kwa nini watu wanakuwa na tafsiri tofauti juu ya mtu kuzungumzia ukweli wa suala husika. Lakini mtu anakuwa na povu ambalo halihusiki kabisa.

Nani asiyejua kuwa hayati JPM ndio alianzisha mfumo kuwa mapato yote ya serikali yawe centralized na pesa zote ziingie hazina. Huko nyuma ilikuwa ni upigaji tu. Pesa nyingi zilipotea mikononi mwa wajanja wachache.

Alipoingia madarakani tu pesa nyingi akakukusanya na zikatumika bila kificho kwa manufaa ya umma. Mapato ya serikali yakapanda kutoka bil 700 mpaka tril 1.7 kwa mwezi.

Leo hii baada ya mapato kupanda pesa za umma zinafanyiwa anasa kwa safari za ughaibuni zisizokwishwa.

Wapuuzi wachache na wajinga sana wakisikia tunasema kweli wanaleta kebehi za kipufedhauzi.
Bro thingz kwa ground ni Different!
Hv unajua kuwa TRA walikuwa wanalazimishwa na mazingira takwimu za uongo?
 
Back
Top Bottom