Maamuzi mabaya kama yapi? Kukusanya mapato ya serikali na kuyatunza hazina? Kufufua miundo mbinu ya usafiri wa majini? Au maamuzi yapi kwa mfano?
1. Je unakumbuka ripoti ya CAG Assad kuhusu ile 1.5 Trilioni iliyopotea kwenye ofisi na hakukuwa na taarifa yeyote? Assad kiongozi asiye na woga kwa binadamu bali kwa Mola wake aliuweka uwazi juu ya matumizi mabaya ya pesa ile ambayo hadi leo hakuna maelezo ya kueleweka.
2. Unakumbuka Bilions zilizotumika na baadhi ya viongozi kwenda India matibabu enzi hizo akiwemo Sipiker na Makounder? Ni miongoni mwa matumizi mazuri?
3. Kutumia pesa pasipo kupitishwa na bunge ama kinyume cha bajet kwa jinsi tu mtu mmoja anawaza ndio matumizi mazuri ya pesa za umma?
4. Ujenzi wa uwaja wa ndege wa kimataifa kijijini wakati makao makui ya serikali haina uwanja kama huo, unaona hilo ni jambo jema? Huoni huo ni ubinafsi mmaya sana?
5. Watu waliojenga karibu na barabara Dar ni sawa kubomolewa nyumba zao ila wale wa Kanda ya...wao hawatakiwi kuvunjiwa, kwa sababu ni wapiga kura. Unaona hiyo ni haki?
6. Kukandamiza haki za wafanyakazi na za kisiasa ambazo zipo kikatiba na kisheria hiyo nayo ni sawa? Unamnyima mtu stahiki zake za nyongeza ya mishahara ama kumpandishia kiwango cha makato (mfano Loan Board) ili tu uzikusanye na kuzizuia pesa nyingi toka kww mfanyakazi huku yeye akiumia, unaona pia hilo ni sahihi?
7...niendelee??
Kiufupi, tumuache Mama yetu afanye kazi yake kama wale waluopita nao walivyofanya kwa namna wamefanya.
Mh. Rais ameona namna watu wameteseka muda flani na sasa anatibu kwanza vidonda tupone vzr ndipo tuongeze kasi kukuza uchumi.
Mwaka Mmoja lakini amefanya mambo mengi mazuri kww watu. Ukweli tuuseme.