Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani na ni bara lililobarikiwa kuwa na utajiri mkubwa ulimwenguni. Afrika pia inatajwa kuwa ni bara muhimu la kimkakati katika maendeleo ya dunia, Lakini Afrika ina historia ambayo ni giza tupu na imejawa majonzi, manung’uniko,jasho na damu. Historia ambayo hadi leo inatuumiza waafrika kwa kuwa nchi zetu zilitumika na wakoloni kama sehemu za kuzalishia malighafi tu na watu hao hawakufanya jitihada zozote zile za kuboresha nchi na maeneo walioyatawala zaidi tu ya kuchukua malighafi na hata walipoondoka waliacha nchi zetu zikiwa katika nafasi mbaya za kusimama zenyewe na kujiendesha.
Nchi zetu ziliachwa tupu na ukiwa ambapo hatukuwa na ujuzi ,miundombinu na idadi ya watu ya kutosheleza ambapo jambo hili liliongeza ugumu wa nchi za Afrika kuweza kujijenga na kukua. Na jambo hili liliweka ugumu kwa wale waliopata madaraka ikiwemo mifano ya Mwl J.K. Nyerere, Nkwame Nkurumah, Samora Machel, Patrice Lumumba, kuweza kuziendeleza nchi za Afrika ambazo zilikuwa zinaanza maisha mapya kama nchi zinazojitegemea.
Safari hii mpya haikuwa rahisi na ilihitaji kizazi cha viongozi wenye moyo wa uvumilivu, maono na mikakati ili kuweza kutuvusha katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi za Afrika tulikumbwa na umasikini, njaa, magonjwa na idadi kubwa ya watu hawakujua kusoma na kuandika. Tunamshukuru Mungu alitupa viongozi ambao walitutia moyo na kutupigania na hata ambao walikuwa tayari kufa kwa ajili ya wananchi wao. Hakika kilikuwa kipindi cha matengenezo na tukaweza kusimama na kusonga mbele.
Kama ambavyo kila kitu maishani kina majira yake hata na mashujaa wa Afrika walikuwa na muda wao na hatimae , ilibidi muda wao ufike wa kuachia watu wengine washike usukani kuongoza nchi zetu kwa kuwa changamoto mpya ziliinuka na ambazo zilihitaji mtazamo tofauti ili kuweza kuzitatua. Hapa ndipo mzigo mwingine uliiangukia nchi nyingi za Afrika ambao umeacha hasara kubwa na maumivu yasio na kifani kwa waafrika, Janga ambalo kama lisingekuwepo leo Afrika ingekuwa ni bara la mfano ulimwenguni kwa uchumi mzuri, mshikamano na utamaduni uliotukuka na hizi sifa zingependezeshwa na uzuri wa bara la Afrika. Janga la Uongozi likaibuka. Baadhi ya viongozi hawakutaka kuachia madaraka, wengine wakaendekeza ukabila, wengine wakaendekeza rushwa na udikteta.
Kipindi hiki Afrika tulijiroga wenyewe na kipindi hiki ndicho kilichozaa majanga ambayo yanatutafuna hadi leo kama ukabila ulivoua takribani watu milioni 1 kule Rwanda mwaka wa 1994. Walizuka viongozi vibaraka kama Mobutu Seseseko ambaye alimtoa Patrice Lumumba ili apate nafasi ya uraisi nchini Congo. Akanyanyuka Idd Amin Dada ambae alikuwa dikteta nchini Uganda ambae aliua watu. Nchini Zimbabwe akakaa Robert Mugabe ambae hakutoa nafasi kwa watu wengine kuwa viongozi na kuiongoza nchi hiyo, Mugabe alikaa kwenye kiti cha Uraisi kwa takriban miaka 37!, Hata baada ya Mugabe kuacha uraisi Zimbabwe bado inateseka na changamoto ambazo zilisababishwa na Mugabe hususan kwenye uchumi.
Hadi leo hii nchi za Afrika zinazoteswa na Uongozi mbovu au mfumo mbaya wa Uongozi ni nyingi sana. Ambapo wananchi wanakuwa waathirika wa kwanza wa matatizo yote yanayosababishwa na serikali zao. Jambo ambalo sio zuri, nikisema niendelee kuandika mifano ya nchi zilizoathirika na zinazoathirika na mifumo mibovu ya uongozi bila shaka Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi hizo. Hakuna changamoto yenye madhara hasi makubwa kwenye nchi kama kuwa na Uongozi mbovu au mifumo mibaya ya Uongozi kwa sababu shida zingine zitajengwa kutokea hapo kama Rushwa, wananchi hawatopata huduma bora za afya, hakutokuwa na uhuru kwa wananchi na vyombo vya habari, shida za maji, hakutokuwa na elimu bora, uchumi mbovu,ukosefu wa ajira n.k. Changamoto zote hizi zinatokana na kuwa na Uongozi mbovu.
Kabla sijafika kusema suluhu ya changamoto hii ya uongozi mbovu Afrika na kwenye jamii zetu, lazima tujue kiongozi ni mtu wa namna gani kiongozi ni mtu yeyote sio lazima awe serikalini ambaye analo jukumu la kuongoza kikundi cha watu kwenye jamii yake husika. Afrika tunahitaji viongozi kwenye kila nyanja. Kiongozi lazima avutie watu kwa jitihada zake za kuiboresha jamii yake na si kuidumaza. Tumeona mfano wa watu hawa kwenye jamii zetu watu ambao wanajitolea kufanya jitihada ambazo ni bora kwa jamii inayowazunguka. Wewe unaweza kuwa kiongozi na mimi naweza kuwa kiongozi katika jamii zetu husika.Mfano wa viongozi kwenye nyanja tofauti tunae Mbwana Samata kwenye mchezo wa mpira wa miguu, Vijana wengi wanajituma kufikia na hata kuvuka alichokifikia mchezaji huyu na pia kuifanya Tanzania kuzidi kupaa kimchezo, Benjamin Fernandes ameonesha ulimwengu kuwa teknolojia inaweza kutoka Tanzania na ikasambaa duniani naye pia amehamasisha vijana waamini kuwa Tanzania inaweza ikauza bidhaa zake kimataifa na pia ametoa ajira kwa vijana wa kitanzania na wageni. Tunao viongozi wengi ambao wapo katika sekta za michezo, burudani,teknolojia, kilimo n.k.
Katika takwimu zilizotolewa na UN zinasema mwaka 2035 bara la Afrika litakuwa na nguvukazi kuliko bara zingine zote . Ikimaanisha bila kazi yoyote ya msingi Afrika inaweza ikawa na idadi ya watu ambao hawana ajira rasmi zaidi ya bilioni 1 kutoka idadi ya watu milioni 432 kutoka 2015. Nikisema 2035 unadhani ni mbali la hasha ni siku 4714 zimebaki!. Tunahitaji viongozi kutoka kwenye michezo hadi kwenye kilimo ili waweze kusaidia kumudu ongezeko hili la watu. Tunaweza kuanzisha vyuo kama African Leadership University( ALU ) ili tujenge ufanisi wa wanafunzi kutatua changamoto zinazowazunguka , Mwanafunzi anafundishwa mambo ya msingi kuhusu uongozi, namna anavoweza kuongoza watu na yeye binafsi kujiongoza na anaruhusiwa kutafuta changamoto moja anayoona anaweza kuitatua na anaunganishwa na mtandao wa watu wenye dhamira moja ya kutatua changamoto aliyochagua iwe Afya, Ajira, Michezo,Maji taka, Njaa, Mabadiliko tabia nchi , nishati na anajenga suluhu juu ya changamoto hizo na baadae anakuja kuleta manufaa kwenye jamii yake kupitia changamoto aliyotatua. Na hivi ndivo tutajenga viongozi bora kwenye jamii za Afrika.
Kwa namna hii tutatengeneza viongozi kwenye nyanja mbalimbali kuanzia kwenye elimu hadi kwenye siasa, na hii ndio itaifanya elimu kutokuwa kioo bali dirisha la fursa kwenye nchi yetu hii pendwa na bara letu la Afrika, Na pia itasaidia kufanya mapinduzi makubwa barani kwetu. Kwa sababu ninaamini ukiwa Kiongozi Afrika ni rahisi kuleta mabadiliko kuliko bara lingine lolote lile duniani, Mfano wewe ni Rais wa marekani na unataka kuongeza miaka kwenye katiba ya nchi kinyume na matakwa ya katiba na sheria, tuna uhakika seneti na congress watakukatalia. Lakini Afrika kuna viongozi wamejiongezea miaka na hakuna mtu anaeuliza kwa sababu kila kitu kimeelekezwa kwa mkuu wa nchi. Tukiweza kuelimisha jamii yetu kuhusu uongozi kila mtu atafanya nafasi yake.
Nelson Mandela aliwahi kusema “Never doubt that a group of thoughtful committed citizens can change the world, Indeed it’s the only thing that ever has”.

Upvote
0