Kwanza yule mzungu Brian Deacon sio Yesu, na Mtume wa Allah Yesu yuko mbali na matusi anayotukanwa na washirikina na sifa za uongo walizomzushia. Halafu sisi sio wana wa Allah uliyemkejeli hapo, sisi ni waja wa Allah. Sisi ni watumwa wa Allah. Na tunafurahia hilo.
Kufuga ndevu ni jambo la kimaumbile na ni Sunnah ya Mitume wote na kuvaa Kanzu Mtume Yesu na kuachia ndevu ni katika Sunnah ya Mitume, ambao wote walikuwa Waislam. Na ndio maana sisi Waislam tuna haki zaidi na Yesu kuliko wanaojifanya kumfuata ilhali wameacha Dini yake na kutunga dini mpya walioichanganya na upagani wa warumi. Yesu yuko mbali nao, nao wako mbali na Yesu mpaka wafuate Dini yake, Uislam.
64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.
(Qur-an 3 : 64)