Tunazeeka, ukipata nafasi fanya mambo yako kwa haraka

Tunazeeka, ukipata nafasi fanya mambo yako kwa haraka

Kwa mujibu wa WHO uzee sio umri bali ni ugonjwa.
Kuna watu leo wana umri mdogo sana ila ni wazee.Wengi siku hizi wanaugua ugonjwa wa uzee wakiwa na miaka thelathini na tano na kuendelea.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mi nina 39 na kichwa asilimia 50 ni cheupe, mimi ni mzee?
Kuna tofauti kati ya kuzeeka (growing old) na kukua (growing up). Kuzeeka kunahusisha zaidi kuchakaa kwa mwili (wear and tear of body) kwa kasi kubwa. ilhali kukua kunahusha kuongezeka kwa umri/miaka ya kuishi. Unaweza ukawa na umri mdogo kmf miaka 39 lakini ukawa umezeeka kwa maana ya mwili kuchakaa kulinganisha na mwenye umri mkubwa kmf 60+ lakini akiwa na afya na siha nzuri. Muhimu ni kutunza miili yetu na kuepuka magonjwa na uchakavu usioendana na umri wetu. So grow up, don’t grow old.
 
KADA, leo umeongea jambo la maana kabisa.
 
kweli uwe na pesa tu but pia uwe na nidhamu fulani mfano:
1.usiende kwenye mabaa au mapub ya vijana
2.usivae nguo za vijana
3.uwe unatoka mara moja kwa wiki na utoke na mkeo au wake zako
4.chunga lugha unayotumia kuongea
5.ukitaka kuchepuka vuta mdada wa uhakika,nenda nae mahali pa class ya juu na usiwe na papara kwenye sex,sex kwa utulivu,comfidently na very expertly na tumia kinga maana usimpelekee mkeo au wakezo magonjwa
6.usichukue vibinti kabisa
Vibinti vina tatizo gani?
 
Hicho utakachofanya kwa haraka kitakusaidia nini, au kitazuia usizeeke?
 
Pole, sasa mimi mwanzo watoto nikikutana nao wananiita babu shikamoo, Dah nilikuwa naumia nafsi sana,wengine mama zao walikuwa wanawambia wee! Sio babu muite baba,


Sasaivi nishazoea,maana miaka 40 plus, katoto kalichozaliwa na mama mwenye miaka 20 au 22 ni haki kuniita babu.
😃 😀 😄 😁 eti babu shkamoo. Vitoto muda mwingine vikiona mwanaume Ana kitambi vinajua anaweza kumzaa mzazi wake
 
Back
Top Bottom