Tunazunguka mbuyu hatutaki kusema ukweli

taasisi hizi 3,yaani bunge , serikali , na mahakama , zote ziko chini ya rais na zote kiuhalisia haziko huru . Sasa plus na unafiki , unadhani Nini kitatokea mkuu. anyway muamuzi ataamua ugomvi na kuweka Mambo sawa.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Sauti moja Zanzibar itatoka wapi na mumewaweka vibaraka wenu kwa mtutu wa bunduki na mumejaza wanajeshi kila mtaa kuna Kambi pamoja na usalama wenu wengine wanavaa mpaka rubega Za kimasai
Angalau umekubalu kwamba Zanzibar hawajawahi kutamka kwa sauti moja including viongozi wenu kwamba Muungano uvunjwe., au urekebishwe. Tanganyika tumewahi, bungeni, chini ya Njelu Kasaka. Nyerere akazima madai yetu.

Zanzibar tangazeni kupitia Baraza la Wawakilishi au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwamba hamtaki Muungano.
 
Serikali ya Zanzibar ilikuwepo kabla ya Muungano so siyo huruma ya mwalimu. Huu mfumo ulikuwa ni makubaliano ya pande mbili na siyo Nyerere kuamua
 
Zanzibar ikiamua kujitoa kwenye muungano inaweza hata kesho ikiitisha baraza la wawakilishi wakijadili na kuamua ndio mwisho wa Muungano. Fanyeni hivyo
Mkuu usiwalishe wazenji matango pori. Huwatakii mema jombaa! Ishu ya Muungano sio sawa na chogo kumaliza mapembe (wali) ya wazenji ati!

Huu Muungano hauvunjiki kamwe hadi Nyerere na Karume waliounga nchi wafufuke watamke muungano basi na ule mchanga uliochanganywa utenganishwe.

Wawakilishi wa bunge la stone town zenji wakitamka kuvunja muungano wanakuwa na kosa la uhaini na watatakiwa kunyongwa hadi kufa wote!

Zenji ni koloni letu milele na jeshi la wananchi liko imara kule kufagia chokochoko.

Sababu za muungano ni Siri kubwa! UDSM tumefundishwa ila sijawahi kusikia msomi yoyote wa pale akiropoka popote!
 
Ongezea: Wanasema ni IGA lakini kwa nini upande mmoja kasaini waziri na upande mwengine Mkurugenzi wa DPW?
Halafu tuna msemo unasema Serikali haifanyi biashara lakini tumeingia makubaliano kukabidhi bandari kwa serikali ya dubai
 
Hizo taasisi za kiserikali wakuu wote wa hizo taasisi ni wateule wa rais. Sasa hapo unategemea nini??

KATIBA MPYA NI MUHIMU SANA NA KATIBA MPYA NI SASA
 
Ninyi wazenj mnachekea tumboni!! Kila siku mnaomba huyo sleeping giant(Tanganyika) asiamke!! Mmeigeuza T/nyika kuwa shamba la bibi!! Mnasema hivi: "Cha Tanganyika ni cha wote lakini cha Zenj ni chenu!!" Mzenj anaruhusiwa kuomba na kufanya kazi huku Tanganyika!! Lakini matangazo ya kazi huko Zenj hatujawahi hata kuyaona!!
 

Halafu CCM wanakataa kwamba siyo mkataba wa zaiai ya miaka 100 ambapo muda wa uangalizi ni miaka 33 baada miaka 33 kuisha wapewe hati ya kukodisha ardhi ya miaka 99, (land lease for 99)
 
Baraza la wawakilishi hili lilowekwa na wanajeshi wa Tanganyika na usalama wa Taifa ??
 
Jussa juzi Pemba kasema mkutanoni kuwa sikuizi hakuna kupiga hesabu kwamba Zanzibar inastahiki kiasi gani cha pesa katika mgao, kasema sikuizi Rais anaamua tu hili fungu liende Zanzibar. Wote watoto wa Amani.
Wacha kumpakazia Jussa , weka hiyo clip kama kweli
 
Two different nations at different stages of growth
 
Ongezea: Wanasema ni IGA lakini kwa nini upande mmoja kasaini waziri na upande mwengine Mkurugenzi wa DPW?
Halafu tuna msemo unasema Serikali haifanyi biashara lakini tumeingia makubaliano kukabidhi bandari kwa serikali ya dubai
πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Hawa ndio walioko ikulu ya Tanganyika.
Huyo uliyeweka clip yake ni msomi wa haja. Humpati na wasomi unaowaategemea hawampati hata chembe.


Wakati nyie mnaikumbuka Tanganyika leo, yeye kishaenda jela kwa kuikumbusha Tanganyika miaka mingi sana nyuma.

Mtafute umsikilize ndiyo utaelewa umuhimu wa Sheikh Farid kwenye jamii.
 
Huogopi hata nikileta list ya wasaga na kukoboa wa nchi? Kwanza njoo nkupe soda afis kuu tuongee 🀣
Mzee mimi siogopi, wewe lete tu. Umesema uko serikalini SMZ lkn huwa munasema Watanganyika hamuajiriwi Zanzibar. Nyinyi ni waongo na wachonganishi tu. Endelea kufaidi matunda ya mapinduzi. Sisi Waswahili huwa tunasema "fadhila ya punda ni mateke".
 
Na Tunauzunguka kweli kweli

Tunauzunguka kwerikweri. Wapinzani Pekee ndiyo wanomsema kaboronga.

Eti Mbarawa. Who is Mbarawa. Tatizo nI SAMIA. Ndiyo chanzo cha Takataka zote hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…