Tunda gani la asili umelikumbuka na halipatikani ulipo kwa sasa?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kuna matunda ya asili mengine yanapatikana kwenye maeneo fulani tu, unakuta umekua ukiyala na baada ya kuondoka hapo kwenda sehemu nyingine huyaoni tena.

Leo nimekaa nimeyakumbuka matunda ya kwetu yanaitwa ndati, sema siwezi yapata hadi nirudi kwetu, ila ili kupoza moyo nitaenda sokoni kutafuta mengine ambayo nilikuwa nakula utotoni yanaitwa ntalali au sungwi kama wengi wanavyoyaita maana huku nilipo yanapatikana.

Kwa bahati mbaya picha ya ndati sina ningewaonesha.


Picha ya sungwi au ntalali kwa msaada wa mtandao
 
Uyole yamejaa tele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…