Mropoka Hovyo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2023
- 446
- 1,253
Unatoka unyamwezini nini?. Jina la ntalali linatumika sana Tabora na nsungwi ni Usukumani huko lkn hizo ndati Tabora manispaa zipo nyingi vibaya mno vitunda vidogo vidogo hivi ukubwa wa karanga na Nadhani Tabora ndio sehemu pekee ambapo kila aina ya tunda utalikuta.Kuna matunda ya asili mengine yanapatikana kwenye maeneo fulani tu, unakuta umekua ukiyala na baada ya kuondoka hapo kwenda sehemu nyingine huyaoni tena.
Leo nimekaa nimeyakumbuka matunda ya kwetu yanaitwa ndati, sema siwezi yapata hadi nirudi kwetu, ila ili kupoza moyo nitaenda sokoni kutafuta mengine ambayo nilikuwa nakula utotoni yanaitwa ntalali au sungwi kama wengi wanavyoyaita maana huku nilipo yanapatikana.
Kwa bahati mbaya picha ya ndati sina ningewaonesha.
View attachment 2790027
Picha ya sungwi au ntalali kwa msaada wa mtandao