Tunda gani la asili umelikumbuka na halipatikani ulipo kwa sasa?

Furu na nduwau
 

Kwetu kule tunayaita MASUKU, lakini kwa watani zangu wa kujinyonga yanaitwa MAKUSU

 
Makende ya nyau siyaoni kabisa siku hizi

Mazingafuli nayo yamepotea sana
 
Maviru, Sambia na mafyoksi haya matumda nime ya miss sana yapo huko milimani kwa wasambaa, ( mafyoksi nadhani ndio cherry ila sina uhakika)
 
NDILOLO hili tunda sijaona sehemu nyingine zaidi ya kyela na hilo jina lake sidhani kama na kiswahili linatamkwa hivyo.Kuna mtu aliwahi kuniambia ni mzaituni kwa kiswahili lkn nikagundua sio kweli, lingine ni KOKOA japo yapo morogoro ila ni adimu sana sehemu nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…