Tunda gani la asili umelikumbuka na halipatikani ulipo kwa sasa?

Unatoka unyamwezini nini?. Jina la ntalali linatumika sana Tabora na nsungwi ni Usukumani huko lkn hizo ndati Tabora manispaa zipo nyingi vibaya mno vitunda vidogo vidogo hivi ukubwa wa karanga na Nadhani Tabora ndio sehemu pekee ambapo kila aina ya tunda utalikuta.
 
Ni mengi mm yalinishinda kula Yani yametapakaa chini nilivosogea Njombe mjini nikakuta yanauzwa nikatamni ningebeba kiroba😂😂😂
 
Piches and suse, zilikuwa zinapatikana sana Moshi Marangu huko
 
Ule ukwaju ulikua unaota kwenye michongoma ndani una vitunda vyeusi... Maeneo ya msasani na mikocheni yalikua mengi sana miaka ya 90 mpaka 2000...View attachment 2790121
haya mikoa mingi yapo, shinyanga wanayaita matunda kunigwa, dar yanaitwa matunda mifensi pia nimeyaona mwaka jana chunya mbeya, haya ayajapotea, hapa kuna matunda yamepotea kabisa sikuizi ndio yanatakiwa kupata hata mbegu kuotesha kwani ni matunda asili
 
Kuna tunda wakazi wa kanda ya ziwa victoria wanaita limbe, kama bado yanapatikana tufahamishane nije ninunue hata mbagu maana sijui kama yana jina jingine niyatafute maana ilo jina hata mtandaoni sipati picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…