Adamu hakuwa mtu wa kwanza nawe ndiyo umepotoka mzee, kivipi Adamu na Eva hawakuwa sio watu wa kwanza, wakati Mungu alipomuumba Adamu akasema ninaona nikulete msaadizi ambapo Eva alitoka ubavuni mwa Adamu, au unataka kuniambia Eva uzao wake ulitoka wapi
Adam hakuwa mtu wa kwanza KUUMBWA, yeye alikuwa mtu wa kwanza kuongea na Mungu, alikuwa mtu wa kwanza kupewa ufunuo wa kiroho kuwapelekea watu wake katika zama hizo, kifupi Adam alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuonyesha njia ya kufuatwa na watu kumuelekea Mungu hivyo unaweza kusema Adam alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa kiroho.
Eva kutoka ubavuni kwa Adamu; hilo ni tamathali ya kiroho, kama katika elimu mbalimbali tunaweza kuona lugha za elimu hizo zikitumika ndivyo hivyohivyo katika dini pia kuna lugha zake, sio kila andiko katika dini huwa linatafsiriwa "moja kwa moja" (literally) kuna baadhi ya maneno ukiyatafsiri kwa njia hiyo utapata maana za hivyo zisizoingia hata kwenye akili ya mwendawazimu, mfano katika Injili Yesu kajiita mzabibu!!!, je ni kweli yeye ni mzabibu??!, hapo ni lazima tutafute tafsiri ya mzabibu kiroho.
Inaposemwa kwamba Eva (Hawa) alitoka ubavuni mwa Adamu maana yake ni kwamba tabia za Eva zililandana na Adam kiasi kwamba kwa kuoana wangeweza kuenenda pamoja katika hali nyingi, hiyo lugha ni sawa na neno la kiingereza linalosema; "We are made out of the same wood" maneno hayo kwa maana ya literally ni:- sisi tumetengenezwa kutoka katika ubao mmoja, tafsiri yake ni :- Sisi tuna sifa na tabia zinazofanana.
Unaposema kwa maana ya mojakws moja kwamba Eva alitoka ubavuni kwa Adamu maana yake ni sawa na kusema Eva alizaliwa na Adam na kisha akaolewa naye!!!, je Adam alioa mwanaye??, kama hakuoa mwanaye, je alioa kiungo chake??, hayo ni maswali ambayo hayana majibu, hivyo dhana ya Eva kutoka ubavuni kwa Adamu haina maana ya moja kwa moja isipokuwa maana yake ndiyo hiyo niliyoieleza hapo juu.
Adamu aliishi takriban miaka 6,000 iliyopita lakini dunia hii ina umri wa bilions ya miaka na watu wa kale waliishi milions ya miaka kabla ya Adamu, sasa huwezi sema kwamba Adam ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuumbwa, juu ya yote Biblia imetaja juu ya kisa cha kaini na Habili, kaini akamuua Habili na kisha akatorokea katika nchi ya Nod na huko akaoa, sasa jiulize huko alioa mtu au jini bila shaka alioa mtu, je huyo mtu alitokea wapi wakati kipindi hicho walikuwepo watu watatu tu duniani???.
Adamu hawezi kuwa mtu wa kwanza kuumbwa.