Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aanza kuwaletea maendeleo na haki Watanzania hata kabla ya Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aanza kuwaletea maendeleo na haki Watanzania hata kabla ya Uchaguzi

Ondoa huo ujinga.

Kutangaza ajira kipindi cha kampeni ni RUSHWA.

Rais KUAMURU Kuitisha tenda ya ujenzi wa barabara na FEDHA za kujengea AULIZWE YEYE NI RUSHWA.

KAMA ILIKUWEMO KWENYE MPANGO, WAZIRI LAZIMA AJUWE FEDHA ZILIPO.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TOENI UFAFANUZI,

ANGEAHIDI KUJENGA BAADA YA UCHAGUZI TUNGEMWELEWA.

KWA SASA NI RUSHWA.
 
Malipo yako ni kuwapigia kampeni wapinzani, maana bila hivyo, jiwe akipita tena anaweza watenda tena, huyo jamaa hana utu kabisa, ni ibilisi mwenye madaraka.
Mimi ni mtumishi wa Umma, siruhusiwi kupiga kampeni waziwazi. Huyu jamaa atanitumbua. Ila kwenye sanduku la kura ni dhahiri kwamba nitamchagua Lissu, apite asipite hiyo kwangu hainipi shida. Sitaki Jiwe apite na kura yangu ikawa ni mojawapo ya kura zilizompa madaraka. Katu sitafanya uchuro huo. Nimpe kura yangu kwa lipi?
 
Kuwanyima watu ajira na ujira bora ni adhabu ya kifo.

Je, watanzania wako tayari kuendelea kupewa adhabu ya kifo na Magufuli?
Hivi serikali inauwezo wa kuajiri watu wangapi?
 
Tume inamtangaza Magufuli. Matokeo yakishatangazwa hayapingwi popote.

Patamu hapo.
Nikweli tume ya kuchunguza sababu ya kwanini ccm ilichapisha fom moja ya uenyekiti, itamtangaza.

Lkn Lissu ndiye atatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuwa ndiye rais aliye chaguliwa na watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu unakutana na takataka inakwambia inapenda bora upinzani ufe, wana bahati kuua ni dhambi la sivyo yangekuwa mengine.
Juzi asubuhi asubuhi nikapigiwa simu na litumishi moja la umma eti linajitapa habari ya Magufuli ameahidi kuwajengea barabara kutoka Bariadi sijui mpaka Singida, pumbavu nililitimua mapema sana! Kuna matakataka hayajitambui!
 
Hata watumishi karbu ata tamka wapewe nyongeza ya mishahara Kaza uzi Lissu.
 
Nikweli tume ya kuchunguza sababu ya kwanini ccm ilichapisha fom moja ya uenyekiti, itamtangaza.

Lkn Lissu ndiye atatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuwa ndiye rais aliye chaguliwa na watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya Uchaguzi Lissu itatakiwa arudi tena Ulaya maana Magufuli safari hii ataenda kutuma vijana wa risasi zisizozidi tatu tu wamalize kazi iliyonshinda Makonda
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka, kazi ni msingi wa maisha. Akunyimaye kazi amekupa adhabu ya kifo.

Serikali ya awamu ya 5 imefanya jitihada kubwa sana ya kuwanyima kazi Watanzania. Yaani imefanya jitihada kubwa ya kuwapa Watanzania adhabu ya kifo

Awamu ya 5 iliwaondoa maelfu ya wafanyakazi kwa kisingizio cha vyeti fake licha ya Watanzania hao, walio wengi wakiwa na vyeti halisia vya umahiri wa weledi wao kwenye ngazi za juu za elimu zao. Wengi waliondolewa kwa kukosa vyeti halali vya kidato cha 4 wakati ukweli ni kuwa miaka hiyo nyuma fursa za elimu zilikuwa finyu sana kama hukuchaguliwa kuingia shule za serikali hata kama ulikuwa umefaulu vizuri masomo yako.

Kuna madaktari na manesi wengi ambao wameokoa maisha ya maelfu ya Watanzania, waliondolewa na kufukuzwa kama mbwa koko bila hata ya kulipwa mafao yao. Kuna walimu, wahasibu, n.k. Hawa wote walipewa adhabu ya kifo na utawala wa awamu ya 5, kwa tafsiri ya Baba wa Taifa.

Utawala wa Rais Magufuli uliua biashara na uwekezaji kwenye sekta karibu zote. Maelfu ya Watanzania wakakosa kazi. Hao nao, kwa tafsiri ya Mwalimu, utawala wa awamu ya 5 aliwapa adhabu ya kifo.

Rais Magufuli aliamuru kuvunjwa maelfu ya nyumba ambazo Watanzania walikuwa wakiendesha biashara mbalimbali kwenye nyumba hizo, tena nyumba zilizokuwa na hati, na kukiwa na zuio la mahakama. Hawa nao, kwa tafsiri ya Baba wa Taifa, Rais Magufuli aliwapa adhabu ya kifo.

Kutokana na uwekezaji kudondoka toka ukuaji wa 28% mpaka 4%, maelfu ya wahitimu wa vyuo walikosa kazi. Hawa nao wamepewa adhabu ya kifo, kwa tafsiri ya Baba wa Taifa.

TUNDU LISU AWAOKOA WATANZANIA KUTOKA ADHABU YA KIFO
Kutokana na Tundu Lisu kurejea nchini, na kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, amekuwa akiibua wazi udhaifu wa utawala wa awamu ya tano, hasa kuhusu kupuuza haki za raia, uhuru na maendeleo ya watu.

Kampeni zikiwa zinaendelea, Serikali ya awamu ya 5, imetangaza ajira 13,000 za walimu. Bila Lisu, nina hakika kwa 100%, serikali ya awamu ya 5 isingetangaza hizi ajira. Watakaoajiriwa, wautambue kwa namna ya pekee mchango wa Lisu na upinzani katika ustawi wa Taifa, ustawi wao binafsi na familia zao.

Kwa zaidi ya miaka 3, wakulima wa pamba, walinyimwa malipo yao. Baada ya Tundu Lisu kueleza wazi kuwa Serikali inawaonea na kuwaibia wakulima wa pamba kwa kutowalipa fedha za mauzo ya pamba yao, Serikali ya awamu ya 5 imetangaza kuwa itaanza kuwalipa madeni wakulima wa pamba. Wakulima hawa, bila Tundu Lisu, walikuwa wamepuuzwa na kusahaulika na Serikali ya awamu ya 5.

Sijui mpaka Kampeni kwisha, ni wananchi wangapi watafaidila kwa ujio wa Tundu Lisu.

Watanzania tuuenzi na kuulinda upinzani. Bila upinzani, ukiwa na uongozi kama huu wa awamu ya 5, tutajuta. Titakamatwa na kurundikwa magerezani, tutauawa hovyo, tutatekwa ovyo, tutapotezwa ovyo, tutaonewa hovyo, tutanyimwa uhuru na haki zetu hovyo, tutapuuzwa na kudhalilishwa utu wetu na hawa viongozi miunguwatu kwa namna isiyoelezeka.

Nina imani mpaka kwisha kwa kampeni, Watanzania wengi watanufaka na Tundu Lissu kugombea nafasi ya Urais. Watanzania tuupe nguvu kubwa upinzani, ili wanaoshika madaraka watutendee haki.
Hauchoki kuandika maana kama umetumiwa vile.
 
Back
Top Bottom