Uchaguzi 2020 Tundu Lissu abadili upepo, aanza kumsifu Rais Magufuli

Usikivu unaojaribu kuutafuta nikutoka upande gani ,kwani hats Mimi sijakuelewa.
 
mimi nimemuona na kumsikia akimponda Magufuli pale Muheza.
labda kama kahutubia mara 2!
 


Mkipigwa mitama kama Mbasha kwa kumlisha mtu maneno mtasema mnaonewa.
 
Mleta mada umepata mume aliye tayari kukusomesha elimu utakayo ili next time uje kuandika kitu kinachoeleweka.
Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu Elimu
 
Nyerere alikuta mashamba ya mkoloni, mashamba ya katani Tanga, chai Iringa, Kahawa Kilimanjaro na Hai. Ma DC na mabwana shamba wakikoloni walipita vijijini na walugaluga (mgambo) usipoonyesha shamba la pamba unakula viboko, majosho yalichimbwa hadi leo nenda Ndagalu Kabila Mwanhuzi kuna malambo ya mkoloni. Mashamba ya Mkonge yalikufa mikononi mwa nani kama sio Nyerere, hadi Mwinyi anachukua nchi hatukuwa hata na nguo, kijana ukifika usiku anaazima kaniki ya mamake ndio ajifunike.

Leo tunahimizwa kulima chakula mtu mwingine anasema anatukanwa, tunataka kujenga taifa la watu gani? wanaoona kufanyakazi ni manyanyaso
 
Hivi ni Jambo gani liliokamilika, alilolianzisha mwenyewe na kulitekeleza JPM mpaka sasa ?
 

Kwa kisukuma hizi ndoto yako za mchana inaitwa "wishful thinking."

Ungekuwa umemalizia na sentensi moja tu kwenye bandiko lako mkuu kuwa:

"Laiti ingekuwa hivi."

Kusingekuwa na hizi changamoto zote. Siyo za kupumua lakini. Bali za kushindwa kukuelewa.
 
Sawa alikuta fedha kiasi hicho lakini mbona hausemi alikuta huduma za kijamii na elimu vipoje?
Miundombinu ya maji ilikuwaje na yeye aliondoka vitu hivyo vikiwa katika hali gani? Alicha hospital na zahanati ngapi ambazo wakoloni hawakujenga?
Mkoloni alisomesha nje wataalamu wangapi kama wahandisi na daktari?
Nyerere alisomesha hao wataalamu wangapi huko nje?
Mkoloni alisomesha rubani wangapi nje na kununua ndege ngapi za serikali?
Je Nyerere alisomesha rubani wangapi na alinunua ndege ngapi?

Maana wakubwa wanakumbuka Nyerere alijitahidi sana kuweka angalau vyanzo vidogo vya maji au visima vya maji safi karibu kila kijiji cha ujamaa.
Una wakumbuka 'Fini-Water' mradi wa kutoka Finland?
 

Habari mwana usalama wa taifa 😂😂
 
Umesahau Nyerere alisambaza maafisa ugani(Bwana Shamba), Bwana Mifugo kila kata na kulikuwa na mashamba ya bega kwa bega?
Na siyo kweli kwamba mashamba yote yalikufa enzi za Nyerere.
Nyerere alipeleka hadi vifaa vya kilimo mashuleni (primary and secondary schools), alipeleka mafunzo ya ufundi stadi hadi shule maalum za msingi.
Achana na Nyerere mkuu.

Jambo lingine lazima utambue kuna baadhi ya maeneo wakoloni hasa wa waingereza waliacha mashamba ambayo tayari ardhi lilisha choka na mashine au vifaa vya shambani vulikuwa vikuukuu tayari.
Nyerere alianzisha mashamba mapya pia.
Mbona mimi kijana mdogo lakini nakumbuka hivyo vitu? wewe ulikuwa wapi?
Au ni mapenzi yaliyopitiliza kwa Mh. Magufuli hadi unajivika upofu wa kumbukumbu?
 
Kaka mie nimejiajiri, nashughuli zangu ndogondogo kando ya barabara na sasa hivi aa mgambo ya jiji wala hawanisumbui tumekuwa marafiki
Kwakweli magufuli kawapa nafasi machinga ya kujitafutia bila bughudha na kudhurumiwa na migambo wa jiji.
Ukienda mjini cinty centre unafurahi mji msafi na machinga wapo wanapiga kazi.
 
Nyerere amekaa madarakani miaka mingapi na Magufuli amekaa miaka mingapi, halafu ndo uweze kuwatofautisha. Au je, Magufuli angekaa miaka ambayo Rais Nyerere alitawala, yaani apewe leo miaka hyo, je tutakuwa tumefika katika maendeleo gani?
 
eddy nataka nikuambie jambo lingine alilofanya Nyerere ambalo Magufuli hajaweza.
Serikali ilikuwa inagawa bure lishe na maziwa kwa watoto wanaohudhuria kliniki na wamama wajawazito pia.
Walikuwa wanapewa elimu au mafunzo kuhusu watoto na ujauzito kisha mwishoni wanapewa hivyo vitu bure kabisa.

Mama yangu alikuwa coordinator wa afya akisambaza na kusimamia vitu hivyo hadi vijijini ndani huko. Mwache Nyerere aitwe Nyerere, huyu Mh. Magufuli anajitahidi sana sana lakini bado. Nahisi tutaelekea huko kwa baadhi ya yale mazuri ya Nyerere kama Magufuli atashinda awamu ya pili, tumpe muda na nafasi tu.
 
Marupurupu ya usafiri sekondari! Mnapewa tiketi za mabasi na treni pamoja na mikate wale wanaoishi mbali! Vyakula vya kubadili ie nyama na samaki, wali, ugali na makande. Na hii tumeikuta bado inaendelea kwenye serikali ya Mwinyi
 
Nyerere amekaa madarakani miaka mingapi na Magufuli amekaa miaka mingapi, halafu ndo uweze kuwatofautisha. Au je, Magufuli angekaa miaka ambayo Rais Nyerere alitawala, yaani apewe leo miaka hyo, je tutakuwa tumefika katika maendeleo gani?
Ninyi hamsomi mnakimbilia kujibu, nimeshajibu mara tatu hii hoja yako.
Endelea kusoma comments utapata jibu chini.
 
Marupurupu ya usafiri sekondari! Mnapewa tiketi za mabasi na treni pamoja na mikate wale wanaoishi mbali! Vyakula vya kubadili ie nyama na samaki, wali, ugali na makande. Na hii tumeikuta bado inaendelea kwenye serikali ya Mwinyi
Yes Mwinyi aliendeleza vingi tu hata madaftari ya bure aligawa shule za msingi.
Mikate na hivyo vyakula vilikuwepo shuleni na vyuoni hadi miaka ya mwishoni mwa Mwinyi.
Yale yanapugwa chapa za Halmashauri Ya Wilaya husika.
 
Mkuu, ukimuuliza mwanachadema anachopinga term hii hakuna anayeweza kutoa hoja ya Msingi zaidi ya kuibua za watu wanatekwa, wanapigwa risasi, Pesa hakuna mtaani, Lissu alikuwa ubelgiji alipokuwa akitibiwa(Mungu ampe wepesi), kwa hiyo alikuwa hajatembelea mikoa kujionea yaliyofanyika maadam kaona hivyo hana budi kumuunga mkono Jpm.
 
Nawashauri watetezi wenzangu wa Magufuli acheni kabisa kujaribu kuwafananisha Nyerere na Magufuli kwa namna ya kutaka kuonesha Magufuli hadi miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake amemzidi Nyerere.

Kama ninyi ni vijana wadogo rudini vitabuni, maktaba, na mkawaulize wazee wenu wakulungwa, Nyerere alikuwa mbali sana kimaendeleo.
Yuel mtu hapewi sifa bure bure tu, he was a man of high standards, far ahead of others.

Tukianza kuandika hapa mambo yake mazuri au aliyofanya moja baada ya lingine tutajaza kurasa nyingi mno kabla hatujamaliza.
Tulimkanya Lissu kumzungumzia vibaya Nyerere na sasa tuna wakanya ninyi pia, huyo mtu hachafuliki au hashindi kirahisi hivyo, ukimchukia au ukimpondea ndivyo unavyo ijongezea maadui ndani ya chama chako au mashabiki wako.
 
Mtoto wako habebi kwanja anasoma Shaban Robert Nini? Huwezi just yanayo tokea huku kwa wanyonge kaa kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…