Tundu Lissu achukua fomu kugombea Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Wewe ni tatizo linalojitegemea,bora wakakubadilishe kwa debe la mahindi mnadani
Tundu Lisu na DJ si ndio walio nunuliwa na maMvi kwa vipande vya fedha na yule aliyehoji ujio wa maMvi ali furushwa kwenye chama. Leo hii Nyumbu wana kushangilia wanaona wanapiga hatua za kisiasa. Kwa hakika aliye waita nyumbu hakukosea hata kidogo.
 
Amechukulia fomu wapi kwani amekanyaga ardhi yetu?
Kwenda huko! Bladibasketi boli! Chuma kinafanya mambo yake very calculated, nahofia habari hizi zisije zikaleta mtafaruki kama ule uliotokea baada ya ziara ya Ruangwa.
Ee baba uliye juu tuepushe na tafurani ile iliyotokea wakati ule mpaka mshusha bendera kuwa nusu mlingoti alisha jiandaa au kwa kimombo wanasema he was standby
 
Aisee sikujua kuwa kuchukua fomu ni tukio la kishujaa.??

Any ways I hope hiyo fomu imejazwa vyema sio kama zile za Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ni ushujaa ndio, kama maelfu watakapo msindikiza Bernard Membe 2020 pale Dodoma kuchukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama chake CCM alichokitumikia siku nyingi.
 
Kwenda huko! Bladibasketi boli! Chuma kinafanya mambo yake very calculated, nahofia habari hizi zisije zikaleta mtafaruki kama ule uliotokea baada ya ziara ya Ruangwa.
Ee baba uliye juu tuepushe na tafurani ile iliyotokea wakati ule mpaka mshusha bendera kuwa nusu mlingoti alisha jiandaa au kwa kimombo wanasema he was standby

Bendera yetu irushwe nusu mlingoti sababu gani?
 
Mbowe ametumua akili nyingi na kiufundi wa hali ya juu sana. Kumfanya lissu naibu wake, kumlazimisha Abdallah Safari ajitoe na apishe nafasi.

Lakini Mbowe asitudanganye sisi sio wale nyumbu wake.
1. Hakuwa na nia ya kuachia kamba, bali mbinu za kisiasa za kiafrika. Japokuwa mie siyo mwana cdm, lakini ni mmoja wa watu waliopendelea aendelee kwa wakati, kwani Mbowe hana madhara makubwa kwa chama changu CCM.
2. Kumleta Lissu, kitakisaidia chama changu kurudia misingi yake ya kiutendeji, na atatusaidia kuwaumbua hawa maMBUMBU walio kiteka chama chetu.
3. Mbowe ndiye aliyemjengea mizingwe Sumaye, na amefanya vizuri sana, na tunaomba asirudi nyumbani, CCM sio ward ya hospitali.

Naiombea Chadema uchaguzi tulivu na watuletea siasa zenye tija na kuwaamsha CCM Asilia usinginzini.
 
Hiyo nafasi ya makamu mwenyekiti ilipaswa kupewa mzanzibari Ina maana Chadema sio Chama Cha kitaifa Tena ? Ni Cha Tanzania bara tu?
 
WanaJF

Habari za hivi Punde ni kwamba Jabali la kisiasa Tanzania na Afrika Tundu Antipas Lissu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa na tayari amekwisha jaza fomu na kuzirejesha.

Akihutubia mkutano mkuu wa Kanda ya Kaskazini hivi Punde,Mwenyekiti wa chama Taifa Freeman Aikael Mbowe ameeleza kuhusu tukio hilo la kishujaa alilofanya Tundu Lissu.

Mbowe amesema Makamu Mwenyekiti wa sasa Professor Abdallah Safari ameomba kupumzika na hivyo Lissu ameona ni wakati muafaka kwake kuomba nafasi hiyo.

Wakati huo huo, Freeman Aikael Mbowe amekubali maombi ya vijana nchi nzima ya kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti Taifa na amerejesha fomu yake kwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa.

Akirejesha fomu hiyo huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe wa mkutano mkuu Kanda ya Kaskazini Mbowe amesema alichukua muda mrefu kutafakari ombi hilo la vijana na alikuwa na nia ya kutogombea tena nafasi hiyo.Hata hivyo amesema alirudisha moyo nyuma baada ya kutizama imani kubwa waliyo nayo wanachadema kwake na kuona akikataa maombi yao itakuwa ni kuwasaliti.

Akizungumzia yaliyotokea katika uchaguzi Kanda ya Pwani Mbowe amesema amesikitishwa na mambo ya uongo yanayoandikwa na baadhi ya watu na akasema kwenye mambo haya ya uchaguzi huwezi kuzuia ajali za kisiasa.Hata hivyo amewahakikishia watanzania kwamba Mhe Sumaye anahitajika ndani ya Chadema kama walivyo wanachama wengine na amesema yaliyotokea yatamalizwa kwa upendo na nidhamu ya hali ya juu ndani ya chama.

Drama!!!
 
Attachments

  • 5E3D86C3-21B0-45BA-B8E6-88A1E3291633.jpeg
    5E3D86C3-21B0-45BA-B8E6-88A1E3291633.jpeg
    16.3 KB · Views: 1

Uongozi wa juu utakuwa wagalatia watupu........kama ACT wazalendo!
 
Lisu kama mwanaume kweli asimame na aseme tena kuwa nchi hii kuna 'dictator uchwara'..
 
Kwa hiyo safu inayotarajiwa, Kuna wengine hawataiona ni safu kali, bali wataiona ni safu ya wabara na kidini. Pia kuna muonekano wa Mbowe ameamua kuwaweka watu wake ,kwenye sehemu muhimu.

Matarajio ye wengi inaweza kuwa safu kali na muhimu, itakayoweza kupambana na CCM ya sasa.
 
Back
Top Bottom