Tundu Lissu akichaguliwa rais wa Tanzania utafanya nini?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Japo simpigii kampeni, nani ajuaye mipango ya Mungu. Katika gombea gombea ikatokea Tundu Lissu akachaguliwa kuwa rais, utanya nini au utajisikiaje? Nakumbuka. Alimuonya Magufuli juu ya uvunjaji wa sheria za mikataba akataka kumuwahisha kuzima akaishia kuwahi yeye. Alinusurika kuuliwa. Hakuuguzwa kama sheria inavyotaka kuhusiana na haki za wabunge. Hakulipwa fedha yake halali kama mbunge. Alinyang'anywa hata ubunge wake kwenye kejeli ya mwaka 2020 ilioyoitwa uchaguzi. Je anaweza kulipiza kisasi au kusamehe? Piga picha. Lissu akichaguliwa Tanzania itakuwaje?
 
Nitagawa uroda kwa mademu wote wazuri bure
 
Tanzania itakuwa na uraia pacha......Yeeeeiiiiiii
Pia nahisi watumishi wake wataanza kuwanyanyasa watanzania wenye asili ya nje ya Tanzania kama wahindi, waarabu, wasomali na wachina, na hii itakuja upya na gia ya uzalendo......
Wa CCM watawindwa kila kona kama kisasi.....
Lakini kwa kuwa jeshi na polisi limejaa vilaza wenye elimu ndogo na limekuzwa na CCM, baada ya muda mfupi watavuruga nchi......
 
Siyo " kulipiza kisasi", sijui kwa nini umeona maneno hayo ndiyo sahihi kutumiwa. Kama kuna sheria zimevunjwa, hao waliovunja sheria wakifikishwa mbele ya mahakama wewe utaona ni "kulipiza kisasi"?
 
U Rais sio kama viroba unakunywa
Huyo aliye nao sasa hivi unasemaje?
Unaweza kumlinganisha kwa hali yoyote na uelewa alio nao Tundu Lissu?
Watu mnapenda sana kujitoa akili bila ya sababu yoyote ya maana.
 
Katiba mpya tu inatosha pia miaka 5 tu itamtosha kurejesha tanganyika akimaliza hii kazi akapumuzike
Then tunaweza kumpa zitto by that time atakuwa amekua ameacha utoto na udini
 
Kwanza huyo wa kumchagua lisu kuwa rais ni nani? Siamini kama raia wa Tanzania mwenye akili zake timamu anaweza kufanya huo ujinga
 
Kwanza huyo wa kumchagua lisu kuwa rais ni nani? Siamini kama raia wa Tanzania mwenye akili zake timamu anaweza kufanya huo ujinga
Kwani rais wa Tanzania anachuguliwa na kura za raia ile siku ya kura?
 
Hawezi kuchaguliwa hata kua mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji, na kwahivyo nitaendelea na kazi na majukumu yangu ya kuwatumikia wananchi na waTanzania wote kama kawa kama dawa 🐒
 
Tunaenda kutengeza mifumo imara siyo watu imara

Tukiwa na katiba mpya Bora tutarejesha demokrasia ya kweli siyo kama hii ya akina mchengerwa na mkwe wake
Tutajesha ukuu wa bunge, uhuru wa mahakama na uwajibikaji wa serekali

Tutaprpmote uhuru wa habariuhuru wa watu, uhuru wa kiuchumi na kisiiasa.
 
Ndoto mbaya hiyo, amka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…